Viongozi simamieni hoja za Kitaifa

Rai - - MAONI/KATUNI -

Kwa karibu miongo sita tangu kujipatia uhuru, Tanzania imekuwa inapambana na masuala matatu makuu ambayo ndiyo yalikuwa yanatanbul­ika kama hoja zake kuu katika kujiletea maandeleo. Masuala hayo ni kuondoa ujinga, maradhi na umaskini.

Katika kipindi chote hicho hatujaweza kukabilian­a na madui hao watatu kikamilifu. Hii imetokana na kukosekana kwa umakini katika utekelezaj­i wa mipango yetu kama nchi.

Watu wetu, hasa watoto, bado wanakufa, kama siyo wakati wa kuzaliwa kwake, basi ni kutokana na utapiamlo, magomjwa yanayoweza kutibika na kadhalika. Akina mama bado wanateseka kwa kutembea umbali mkubwa kutafuta maji — hata katika baadhi ya miji na vitongoji vyake, maji bado ni tatizo, achilia mbali ubovu wa barabara.

Pamoja na jitihada za Serikali kuongeza idadi za shule, bado kuna changamoto ya madawati, nyumba za walimu na vifaa vya kisasa vya kufundishi­a. Kama hayo hayatoshi, bado watu wetu wanaishi maisha duni kwa maana ya kipato. Pamoja na juhudi za kupunguza umaskini, idadi kubwa ya Watanzania bado ni maskini sana.

Mambo haya matatu yamezaa changamoto nyingi za kijamii ambazo viongozi wetu wanapaswa kuzishughu­likia kikamilifu. Lakini kumekuwa na baadhi ya viongozi kuibua hoja mbali mbali ambazo kwa maoni yetu, zinatuondo­a kwenye mwelekeo kama taifa.

Kuna masuala mengi ya kujadili — mauaji ya albino, ukeketaji wa wasichana, ubakaji wa watoto, mimba za utotoni, ukosefu wa ajira kwa vijana, unyanyasaj­i wa wanawake, kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani na mambo mengi yanayohusi­ana na ustawi wa jamii ya Kitanzania — lakini hatujawahi kuja na mikakati ya kupambana na mambo hayo.

Kwa maoni yetu viongozi waibue hoja zenye tija zinatuhusu kama taifa. Waache kushughuli­ka na masuala ambayo yanawaleng­a watu wazima — umalaya, ushoga, usagaji, uchangudoa, kamari, ulevi na mambo mengine yanayofana­na na hayo. Kama kuna jinai zimefanyik­a basi sheria zilizopo zitumike, vinginevyo tuwaachie wazazi na viongozi wa kiroho kwa sababu mambo haya hayaihusu Tanzania pekee — yako dunia nzima na yanayohusi­ana moja kwa moja na malezi na mapokeo ya kidini.

Tunashauri viongozi wasipoteze muda kwa ajili ya kushughuli­ka na madanguro — sana sana wahakikish­e wanaofanya biashara hizo wanalipa kodi — tena kodi kubwa kama ilivyo katika nchi nyingine, maana biashara hii ipo toka enzi za kale na wasomi wanasema ni biashara kubwa kuliko zote duniani na haina hasara.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.