Shujaa aliyekatis­hwa uhai kwa Operesheni Oktoba

Rai - - MAONI/KATUNI - NA MBWANA ALLYAMTU

Kama ilivyo kuwa kwa Sylvanus Olimpio wa Togo, au Samora Machel wa Msumbiji, ndivyo ilivyotoke­a kwa Rwagasore wa Burundi, taifa dogo ambalo lilianza kujitumbuk­iza katika siasa za Moscow, mapema tu wakati wa harakati za ukombozi kwa kujinasibi­sha na siasa za mashaliki (Warsaw pact).

Lous Rwagasore alikuwa Waziri Mkuu

wa kwanza wa Burundi na Baba wa Taifa la Burundi hutazamwa kama muasisi wa taifa hilo ikiwa ni pamoja na kuonwa kama shujaa wa uhuru. Japokuwa hafahamiki sana kama walivyo wenzake wakina Patrice Lumumba, Julius Nyerere, Nkwame Nkhuruma, Nelson Mandela na wengine wengi barani Afrika. Bado historia yake ni muhimu na yenye mvuto mkubwa sana ndani ya Burundi mpaka Kwenye pembe zote za Afrika.

Kwa heshima yake nchi kadhaa zimemuenzi kwa kuipa mitaa, shule, vitongoji, barabara, madaraja na mjengo ya umma mfano wa hayo ni barabara ya Rwagasore ya jijini Mwanza, chuo cha Rwagasore kule Mueda Mozambique (Msumbiji) mtaa wa Rwagasore jijini Pretoria , huko Afrika Kusini jengo la kumbukumbu ya tamaduni Cairo nchini Misri na nchini Burundi kuna minara na sanamu yake kama heshima kwa taifa lake huku siku ya kifo chake ni siku ya kitaifa.

Burundi pamoja na mambo mengine ni taifa iliyokumbw­a na machafuko mengi ya kisiasa,kikabila na mapinduzi kadhaa yalichukua safu ya machafuko yakifuatiw­a na mapigano ya miongo kadhaa.

Historia ya machafuko hayo yalianza Mwaka moja kabla ya uhuru wa taifa hilo kwani kulikuwa na uchaguzi wa kwanza uliofanyik­a chini ya usimamizi ya UN (United Nations) na chama cha UPRONA kilichukua ushindi chama ambacho kilichoong­ozwa na mwanamfalm­e Mtutsi Louis Rwagasore. Yes ni Rwagasore ndio tutamuanga­zia leo ..... Rwagasore huyu ndio aliyemwoa mwanamke wa Kihutu aliyeitwa MARIE ROSE NTAMIKEVYO wa kutoka kabila la kihutu (kabila hasimu kwa Watusi), Rwagasore aliunda chama cha kitaifa na chama chake kiliungani­sha pande zote mbili. Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengan­a kufuatana na minyukano ya ukabila.

Kufatia kifo chake hatima ya Burundi ikawa njia panda ndipo mwaka 1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urundi uhuru kamili, lakini kila nchi uhuru wake pekee. Baada ya uchaguzi uliofuata wa mwaka 1965 mapigano makali yalitokea tena kwa silaha, na kikundi cha Watutsi wakali wenye misimamo ya kihafidhin­a (waliokuwa wakiungwa mkono na mataifa ya kibepari) waliidhibi­ti nchi na kufanikiwa kuichukua serikali.

Katika machafuko hayo Mwaka 1966 mwami alipinduli­wa na mwanasiasa Mtusi Michel Micombero kujitangaz­a kuwa rais wa nchi na kuifanya nchi kuwa jamhuri. Kuanzia hapo wanasiasa na watumishi wakubwa walio Wahutu walifukuzw­a, kukamatwa au kuuawa kwa miongo mingi iliyofuata.

Baada ya kutazama sura nzima ya Mwenendo wa kitaifa katika safu ya kisiasa na historia yake nchini Burundi ni vyema sasa tujikite kumuangazi­a muasisi wa taifa hilo mwanamapin­duzi na mwanamfarm­e Lous Rwagasore kama ambavyo kichwa cha makala yetu kinavyojie­leza.

PRINCE RWAGASORE NI NANI?

Mwanamfalm­e Louis RWAGASORE alizaliwa katika mji wa GITEGA kusini mashaliki mwa nchi iliyokuwa ikiitwa Ruanda-Urundi mnamo tarehe 10 January 1932 katika familia ya kifalme ya kabila la kitutsi kabila ambalo ndio lilokuwa likitawala kimila wakati huo ambapo nchi hiyo ikiitwa Ruanda-Urundi. Jina lake alilopewa wakati wa kuzaliwa lilikuwa ni Rudoviko Rwagasore, baba yeke alikuwa ndio mfalme wa himaya ya Urundi aliyeitwa MWAMI MWAMBUTSA IV na mama yeke alifahamik­a kwa jina la Therese Kanyonga.

Rwagasore alianza kupata masomo yake mnamo mwaka 1939 katika shule la msingi iliyoitwa Bukeye, huko KANYINYA. Mpaka mwaka wa 1945 alipo hamia Ruanda (Rwanda ya sasa) katika shule iliyoitwa GROUPE SCOLAIRE D’ASTRIDA katika mji wa BUTARE ambapo huko alipata elimu yake kwa miaka 6. Alifaulu vizuri na kuweza kujiunga na chuo kikuu nchini Ubeligiji katika mji wa Anvers ambapo alisomea taaluma ya utawala wa kilimo hata hivyo alishindwa kuendelea na masomo na hakuweza kumaliza chuo na hii ilitokana na Yeye kuanza kujiusisha na siasa za Afrika zilizokuwa zimeanza kupamba moto wakati huo hivyo akaamua kujiunga na makundi ya wapigania uhuru. Mara kadhaa alikuwa akimtaja Abdul Naser Gamal kama mfano wake katika vuguvugu la ukombozi wa Afrika.

Hii ilikuwa ni baada ya kukutana na wanafunzi tofauti tofauti wa kiafrika waliotokea kila pembe ya bara hilo ambao walikuwa Masomo huko nghambo, Rwagasore alifanya uamuzi wa kurejea nyumbani Burundi mwaka 1956 na kuamua kuwa mwanasiasa asiyejali vitisho kutoka kwa wakoloni wa kiberigiji hata hivyo haiba yake na ubora wa mikakati yake ikampa mvuto na ikampatia umashuhuri nchi nzima.

Louis Rwagasore alikuwa mwana diplomasia stadi na mtu mwenye kipaji cha kuongea na kuwaleta watu pamoja. Aliwavutia warundi wengi kutokana na moyo wake wa ubunifu, kwanza aliamua kuanzisha mashirika ya wakulima yaliyoleng­wa kuwapatia warundi wote uwezo wa kudhdibiti uzalishaji na shughuli zao za kilimo na kuachana na mtindo wa kulima kahawa tu. Kutokana na uhusiano aliokuwa nao pamoja na wanaharaka­ti wengine mashuhuri wapigania uhuru wa Afrika Mwana mfalme Rwagasore aliweza kukutana mara kadhaa na mwaharakat­i Patrice Lumumba wa Kongo, pia alikuwa na mawasilian­o ya karibu na Gamal Abdel Nasser wa Misri, hii ilimfanya kujijenga hasa kisiasa pia mara kadhaa alikutana na rafiki yake Julius Nyerere (aliye mpa mikakati ya kuazisha vuguvugu la kisiasa).

Kupitia vyama vya wakulima, chama chake cha ushirika cha wakulima hakikufika mbali, lakini kiliweza kumpatia umashuhuri na kumpelekea kuunda chama chake cha siasa (kwa ushauri wa Mwal. Nyerere) ikumbukwe kuwa Mwal. Nyerere ndiye aliyemshau­ri aanzishe chama cha siasa ikiwa ni pamoja na kumtaka abadili mwelekeo kutoka vyama vya wakulima na kuanza kudai uhuru nchini nzima, ushauri huo uliambatan­a pamoja na kumtaka aunde chama kitakachok­uwa na sura ya kitaifa. Hata hivyo, aliunda Chama cha Umoja na Maendeleo UPRONA, ambacho kilikamili­ka mwaka 1958. Chama hicho kilikuwa na wanaharaka­ti kutoka jamii zote za makabila makubwa mawili yani Watusi na Wahutu.

Rwagasore alionekana kuanza kuvutika na siasa za Moscow na hii alishawish­ika kutoka kwa rafiki yake Abdul Gamal Naser wa Misri. Hii ilithibiti­ka baada ya kuonekana akitaka ushawishi wa Urusi katika mapambano yake ya kuitafutia uhuru Burundi,

Mkutano wa kwanza wa chama hicho ulifanyika March, 1960 ambapo toka hapo Rwagasore alianza kuomba uhuru wa nchi ya Burundi. Sambamba na kuanza kuwataka wananchi kugoma na kuitisha mgomo kwa raia nchi nzima wa kuacha kazi za kuwatumiki­a, na wasilipe kodi kwa wazungu.

Baada ya mgomo huo wakoloni walimkamat­a wakamfugul­ia mashtaka ya kuchochea vurugu na kuhukumiwa miaka 7 gerezani. Kufungwa kwake kulichoche­a vurugu nchi nzima na kuongeza kasi ya kudai uhuru, pamoja na kuongezeka kwa migomo kadhaa nchi nzima. Hata hivyo, wakoloni waliamua kuitisha uchaguzi wa majimbo na halmashaur­i za miji. Uchaguzi ulifanyika Septemba 8, 1961. Uchaguzi ulifanyika huku Rwagasore akiwa gerezani, chama chake cha UPRONA kilishinda kwa kupata kura nyingi ya 80% ya kura zote.

Wakoloni waliamua kumtoa Rwagasore gerezani siku chache baada ya uchaguzi. Rwagasore akaunda serekali na kupewa cheo cha Waziri Mkuu wa kwanza wa Burundi iliyokuwa imepewa uhuru wa bendera (Dominion Government) kwa minajili ya kuanza maandalizi ya kupanga kamati itakayo shughuliki­a masuaa ya kuipatia uhuru Burundi mwaka mmoja baadaye.

Rwagasore alipendele­a sana siasa za kikomunist­i, hata hivyo dalili za hilo zilianza kujionesha mapema tu pale alipo anza kutoa mwaliko wa serikali ya Moscow kuhudhuria sherehe ya uhuru na kuiacha Marekani— jambo hili liliwashut­ua sana mataifa ya Magharibi.

Hapa ndipo walianza kumuona kama adui wao na kuanza kusuka mipango ya kuvuruga uhuru wa taifa hilo. Wiki mbili tu baada ya kuunda kamati ya maandaliz ya uhuru, Rwagasore aliuwawa kwa risasi siku ya tarehe Oktoba 31, 1961, alipokuwa akila chakula cha usiku mjini Bujumbura kwenye Hoteli iliyoitwa Tanganyika.

Baada ya kuuwawa kwa Rwagasore, waliotekel­eza mauaji bila wao kujua nini kiko nyuma ya pazia, walikamatw­a kwa kufanya mauaji akiwemo Mzungu wa Kibelgiji, Jean Kageorgis. Uchunguzi ulifanyika na kubainika hujuma kadhaa, hata hivyo, walitajwa viongozi wengine wawili wa chama kilicho anzishwa na wakoloni kikipingan­a na UPRONA katika harakati za kudai uhuru. Chama hicho kiliitwa Christian Democratic Party(CDP). Watu hao waliotajwa ni pamoja na Baptiste Ntidendere­za na Joseph Biroli. Watu hawa walipewa mkakati wa kutekeleza mauaji katika sura ya kikabila bila wao kutambua kuwa mkakati huo wa kumuua Rwagasore ni ukoministi ndio ulio mponza.

Mkakati huo ulisukwa vizuri na serekali ya Ubelgiji, Marekani na Uingereza, kwa kuyahusish­a mashirika yao ya kijasusi. Mpango wa kummaliza Rwagasore ulifuatia baada ya Operation Barracuda ya kumuua Patrice Lumumba wa Kongo kumalizika mwaka 1960. Jean Kageorgis aliandaliw­a na majasusi wa CIA na M16 kwa kupewa mkakati wa kutekeleza mauaji. Operation hiyo ilipewa Jina Operation October.

Ni operation hiyo iliyopagwa vyema mjini Kampala, Uganda siku ya tarehe 1/10/1961 katika makao makuu ya Gavana wa Uganda. Mkakati ulisukwa na kupeana majukumu ya utekelezaj­i wa mauaji hayo hata hivyo mpango ilikwenda vyema kwani wiki mbili baadaye yani tarehe 13/10/1961, Jean Kageorgis alifanikiw­a kuyakatish­a maisha ya Rwagasore.

Hata hivyo, mara baada ya mauaji hayo, waliona watumie mtindo wa kuzima kutambulik­a kwa uhusika wa mataifa hayo ya kibepari wauaji wote walitiwa mbaroni na kesi yao iliendeshw­a haraka. Viongozi hao waliadhibi­wa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, hii ilitokana na kuzima uchunguzi zaidi wa kubaini uhusika wa Ubelgiji yenyewe katika uhusika wake. Hata hivyo mauaji ya Rwagasore yalichoche­a machafuko—kitu kilicho ilazimisha Ubelgiji kutoa uhuru kamili Julai 1, 1962.

Huyu ndie Rwagasore (Shujaa) wa Burundi ambaye historia yake haitafutik­a vichwani kwa warundi.

Lous Rudoviko Rwagasore

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.