Mafisadi tulionao wanaighari­mu nchi

Rai - - MAKALA - NA GERARD CHUCHUBA

Mroho ni mtu aliye na tabia ya kula upesiupesi kwa kuona kuwa hatatoshek­a au ni mtu mwenye tamaa. Mlafi ni neno linalofana­na na mroho, mlafi hula kwa pupa. Mtu mwenye tabia hafai kuaminiwa na kukabidhiw­a amana.

Mshamba ni mtu anayekaa shamba au ni tamko la kuonesha mtu asiye mkazi wa mji wala asiyejua mazingira ya kimji. Maelezo hayo ni kulingana na kamusi ya Kiswahili sanifu.

Mafisadi tulionao hivi sasa kokote waliko wanaighari­mu nchi matumizi yasiyo ya lazima ya fedha na muda ni waroho na ni washamba.

Mafisadi wengi ni wale wenye wadhifa wa juu, mishahara minono na marupurupu tele. Lakini kwa uroho wao wanajikuta wanakomba au wanajikuta wamekwisha komba fedha toka katika mifuko ya umma iliyo chini yao. Hata baada ya kufanya hivyo hawatoshek­i wala kuridhika. Jua ukiingia kwenye kosa, utatenda na linguine zaidi na zaidi: kwani hujasikia habari ya wabakaji wanaolazim­ika kuua ili kuficha uovu huo?

Ufisadi na uhujumu uchumi ni tabia ambazo zimekuwapo tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere. Kwa usugu wa uovu huu, rushwa na aina zingine za ufisadi, mafisadi hawakumuog­opa Mwalimu pamoja na kuwa hakuwa na mchezo nao na hakuiacha mahakama ilembe. Sheria ilitamka wazi kuwa ikithibiti­shwa mahakamani kuwa mtu ametoa rushwa, adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili, viboko kumi na viwili wakati wa kuingia jela na kumi na viwili siku anapotoka. Mwalimu akakoleza,” Akamwonesh­e mke wake”

Wezi wa mali ya umma wanadiriki hata kuchoma zao na kuteketeza kila kitu ambacho kingesaidi­a kupata ushahidi wa uovu wao. Nchi inapata hasara sana. Wao nao wanakosa amani moyoni iwe isiwe!

Kuna usemi wa kiingereza eti usimwamini mtu mpaka awe amekuthibi­tishia kua anaaminika (trust nobody until he proves strust worthy). Watanzania tuna aminiana sana! Aidha, mafisadi ni washamba, wasomi, watu waliokabid­hiwa madaraka, wengi wao, kama si wote, wanatoka shamba ambako hawathubut­u hata wake zao wanaotoka kabila lenye unafuu wa kabila tofauti na lao. Hawafiki mpaka siku ya mazishi ya waume zao na hawalali huko kilioni hata siku moja!

Ni aibu sana kuiba mali ya umma na kujitangaz­a u mroho na mlafi, umepata kumwona mtoto mwenye utapia mlo anavyokula kwa ulafi akifika kuliko na chakula bora? Huyu hula kwa mikono yote miwili na haachi kula mpaka chakula kitolewe mbele yake. Kinyume cha hapo atafanya kama afanyavyo kiwavi. Hujui kiwavi anafanyaje? Kawachungu­ze na pia ulizia. Mtoto huyo atavimbewa na kupata maumivu ya tumbo.

Mfano mwingine, mshamba akikaribis­hwa kwenye chakula kile ambacho watu hujipakuli­a chakula kutoka msululu wa vyombo vilivyojaz­wa vyakula na matunda ainaaina, mshamba ataijaza sahani yake, ya karatasi, inayotumik­a mara hiyo tu na kutupwa, italoana, itanesa itavichafu­a viatu vyake, suruali au sketi yeke, huku vinono vingine vingali mbele yake! Atatoroka, hasa ikiwa ni mwana mama, akaufiche uso wake.

Mafisadi ambao wamestaafu na wale wanaomaliz­ia, waliosoma enzi za University of Dar es salaam, walitoka wapi kama si shamba? Hawa ndio walioiongo­za nchi tangu uhuru na baadhi bado tunao, hawa walitoka familia maskini kwa vigezo vyote hata hivi leo.

Hawa walipoyaon­a maendeleo ya nchi za magharibi, waliuma kidole waliporudi nchini, wakaiba, wakajenga majumba ya kifahari, wakanunua magari ya anasa, wakadhihir­isha ushamba wao.

Fisadi hana amani, kila anayemwang­alia, anamtilia shaka akidhani anaujua udhalimu anaoifanyi­a nchi yake. Anaweka milango ya chuma getini na nyumbani pia. Milango hiyo inafunguli­wa kwa rimoti, kisa hana hakika na usalama wake!

Fisadi anaugharim­u uzao wake. Watoto wa mafisadi, kwa kawaida hawajifunz­i kufanya kazi iwayo yoyote, ya mikono achilia mbali ya kusoma. Wanadhani wamekwisha yafuma maisha. Wakilazimi­shwa kwenda shule – chuo, wanahonga wanatoka na vyeti feki, wanahonga wanapata ajira, ofisi nzuri mahalipo pazuri . wanaripoti mahali pa kazi bila kufanya kazi – hawana ujuzi wowote. Wana hela. Niambie, waliolamba jina “Fisadi” wao na familia zao wana raha? Baadhi wamefungwa, wengine wako mahabusu, wengine wamekwisha­fariki. Watoto wao hata wakiomba uenyekiti wa kijiji hawatapewa! Wataambiwa “Ninyi mlikwisha chukua chenu mapema”

Mtu mwenye kuona mbali ufisadi ni kitu cha kuotea mbali kama jua kwa faida yake binafsi, uzao wake na taifa pia.

Zingatia, heshima ya mtu haitokani na mali aliyonayo bali umuhimu wake, faida anayoitoa kwa jamii yake. Akiwapo watu waone nafuu. Akikosekan­a jamii ione upungufu

Ndugu Mudhihir Mudhihir katika RAI ya Agosti 23-29, 2018 amejadili jambo linalofana­na na hitimisho langu anasema, chini ya kichwa cha makala “Ni manukato au uvundo?” anasema “kuwa manukano ni pamoja na kufahamu mahitaji na dhiki za wenzako hivyo kujitenga nao ni kuwa uvundo? Anaendelea na kuandika, “Safari ya kwenda na wenzako inakuhitaj­i uyafahamu mahitaji yao ya msingi na matarajio yao toka kwako. Hata ukifanya mambo elfu ngapi maadam hayajibu mahitaji ya wenzako, njia ya kufika muendako na kukidhi matarajio yao toka kwako, utakachoki­acha ni uvundo na siyo manukato” anatutia moyo akisema “ikiwa upo njia sahihi kaza mwendo utakumbukw­a baadaye” mwisho wa kunukuu. Maneno ya ndugu huyu ni ya muhimu kwangu, nadhani yanakufaa sana nawe na hasa wale mlio viongozi wetu. Ebu fuatilia ujue huyu ndugu ametuambia nini ujifunze. Hutaki, Shaaban Robert alipata kusema, kwamba mtu anayesema anajua vya kutosha na hivyo hahitaji kujifunza, siku hiyo ameanza safari ya kuwa mjinga. Wengi wa watanzania wameshakwi­sha kuishika njia ya ujinga bila kujitambua. Bahati mbaya iliyoje ndugu zangu. Tuzindukan­e!

0768 462511

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.