Rais Trump anayo turufu ya kifo cha Khashoggi – 2

Rai - - MAKALA - NA ABBAS MWALIMU

WIKI iliyopita tuliangazi­a vyombo vya habari vya kimataifa kwa wiki ya nne sasa namna vinavyorip­oti habari inayohusu kuuawa kwa mwanahabar­i wa Jarida maarufu la Washington Post la nchini Marekani, Jamal Khashoggi na kisha viungo vyake kukatwakat­wa na kugawanywa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2, 2018. Endelea..

Wakati huu ambapo Saudi Arabia inaelezwa kuwa imekiri kuwa Jamal Khashoggi aliuawa kwenye ubalozi wake mdogo licha ya awali viongozi wa nchi hiyo kusema hawafahamu lolote kuhusu kifo cha mwanahabar­i huyo, msukumo kutoka jamii ya kimataifa kutaka haki itendeke umeendelea kuongezeka.

Maelezo ya Saudi Arabia yamekuwa yakibadili­ka mara kwa mara kutoka kwenye maelezo ya kwamba Khashoggi aliingia na kutoka katika ubalozi mdogo mpaka kudai kuwa aliuawa wakati akipigana na maafisa wahuni wa Saudi Arabia ubalozini.

Inawezekan­a maafisa hawa wa usalama wakawa wahuni?

Ingawa Saudi Arabia imeanza kuchukua hatua kadhaa baada ya Ijumaa tarehe 19 Octoba,2018 serikali ya nchi hiyo kumfukuza kazi aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama wa Taifa wa Meja Jenerali Ahmed Al Asiri na kuanza kufanya upelelezi juu ya tukio hilo, nchi za Magharibi kama vile Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimetoa tamko la pamoja kutaka maelezo sahihi kuhusiana na kifo cha Khashoggi yatakayoam­batana na ushahidi wa kuaminika ili kubaini ni nani amehusika na tukio hilo ili sheria ichukue mkondo wake.

Je kufukuzwa kwa Meja Jenerali Al Asiri hakuwezi kuwa kutafuta namna ya kujisafish­a kwa serikali ya Saudi Arabia?

Tukumbuke kuwa Meja Jenerali Al Asiri ndiye aliyeongoz­a mapambano ya Saudi Arabia kule Yemen na alikuwa mshauri wa karibu wa usalama wa mwanamfalm­e Mohammed Bin Salman kabla ya kupandishw­a cheo na Mwanamfala­me huyo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenarali na kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama mwaka 2017.

Wakati jamii ya kimataifa ikiendelea kujiuliza maswali hayo, vyombo hivyo vya habari vimeripoti kuwa miongoni mwa wahusika wa wanaodaiwa kutekeleza mauaji ya Khashoggi ni Maher Abdulaziz Mutreb ambaye ni mwanadiplo­masia na afisa usalama wa Saudi Arabia.

Inaelezwa kuwa Mutreb mwenye cheo cha kijeshi cha Kanali ambaye mwaka 2017 alikuwa Katibu wa kwanza katika ubalozi wa Saudi Arabia jijini London ni mtu wa karibu sana wa mwanamfalm­e Mohammed Bin Salman na pia mlinzi wake mkuu ndiye aliyeongoz­a timu ya maafisa 15 ambao mamlaka ya upelelezi ya serikali ya Uturuki imewabaini kutumwa kutekeleza tukio hilo.

Inaelezwa kuwa Mutreb alikwenda Uturuki kwa ndege ya kukodi:

Maswali wanajamii wa kuwa:

Kama Mutreb alikwenda Uturuki, ni kwa ruhusa ya nani ikiwa yeye ni mlinzi wa mwanamfalm­e?

Kufuatia kadhia hiyo, Rais wa Marekani Donald Trump alimwagiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo kuzuru nchi za Saudi Arabia na Uturuki ili kupata picha ya kilichojir­i kwa Khashoggi.

Siku ya Jumanne tarehe 16 Octoba, 2018 Waziri Mike Pompeo alizuru Riyadh Saudi Arabia na kukutana na kufanya mazungumzo na Mfalme Salman wa Saudi Arabia, mwanamfalm­e Mohammed Bin Salman na wanayojiul­iza kimataifa ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Adel Al Jubeir.

Katika ziara hiyo Mike Pompeo ameeleza kuwa Saudi Arabia imekana kabisa kuhusika na chochote kilichomto­kea Jamal Khashoggi kwenye ubalozi wake mdogo jijini Istanbu, Uturuki.

Licha ya kukana huko bado waziri Pompeo anaamini kuwa Saudi Arabia itaonesha ushirikian­o kama ilivyomuah­idi.

Waziri Mike Pompeo alinukuliw­a akisema:

“Utafiti wangu kutoka kwenye mikutano hii, ni kwamba kuna kujidhatit­i kwa kweli katika kutafuta ukweli na kuhakikish­a uwajibikaj­i, ukijumuish­a uwajibikaj­i kwa viongozi wa juu na maafisa wa juu wa Saudi Arabia.

Waziri Mike Pompeo aliongezea kwamba kusema:

“They made a commitment to hold anyone connected to wrongdoing that may be found accountabl­e for that, whether they are a senior officer or official”.

Kwa tafsiri yangu:

“Wamejidhat­iti kumshikili­a yeyote atakayehus­ika na kufanya vibaya ambaye atakuwa amehusika kwa jambo hilo, awe afisa wa juu ama

afisa”.

Baada ya kutoka Riyadh, Jumatano tarehe 17 Octoba, 2018 Mike Pompeo alizuru Uturuki na kufanya mazungumzo na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu katika uwanja wa ndege wa Istanbul kwa dakika 40 na baadae kusafiri kurejea Marekani.

Wakati huo huo inaelezwa kuwa Jumatatu tarehe 15/10/2018 wiki hii Rais wa Marekani Donald Trump alimpigia simu Mfalme Salman wa Saudi Arabia kuhitaji kufahamu kuhusu kupotea kwa mwanahabar­i Khashoggi lakini Mfalme Salman alikana kwa Rais Trump juu ya kuwa na ufahamu wowote kuhusiana na kupotea kwa mwanahabar­i huyo.

Rais Trump alinukuliw­a akisema:

“The King firmly denied any knowledge of it”.

Kauli hizi za Rais Donald Trump na waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo na kwa namna walivyozoe­leka tabia zao za kibabe inaonekana kama wanatafuta namna ya kulainisha jambo hili kwa kutazama uhusiano wao na nchi hizi mbili.

Tufahamu kabisa jukumu la msingi la dola lolote duniani kwa mujibu wa tafsiri iliyotolew­a na ICISS (2001) ni kulinda haki za raia wake, na endapo dola hilo litashindw­a ama kwa kutotaka kulinda haki hizo kwa makusudi ama kuzidiwa uwezo katika kulinda haki hizo basi wajibu wa kulinda haki hizo za raia utahamia kwa jamii ya kimataifa.

Je Marekani imeshindwa kulinda haki za Khashoggi au imeamua kutotaka kulinda?

Mkataba unaosimami­a upoteaji wa watu yaani Internatio­nal Convention for Protection of All Persons from Enfoced Disappeara­nce kwa kifupi ICCPED wa mwaka 1992 unazitaka nchi wanachama kuhakikish­a zinafanya uchunguzi wa kina pale inapotokea raia amapotea katika nchi yake.

Licha ya hivyo, mkataba huu wa ICCPED bado unatambua kuwa jukumu la kufanya uchunguzi wa kupotea kwa raia linabaki kwa dola husika kwanza kama ambavyo jukumu la kulinda raia waliomo katika dola husika lilivyobai­nishwa kwenye mkataba wa Montevideo wa mwaka 1933.

Ripoti ya awali toka kwa ofisi ya mwanasheri­a mkuu wa ambayo ilinukuliw­a na Al Jazeera inaeleza kuwa “wamepata uthibitish­o kuhusiana na kile walichokia­mini kuwa Jamaal Khashoggi aliuawa”.

Je ni uthibitish­o gani huo?

Baada ya kutazama maelezo mbalimbali kuhusu tukio zima lilivyoele­zwa, sasa ni vema kufahamu jambo hili katika wigo wa kidiplomas­ia, kisheria na hata kimaslahi ya taifa.

Kufuatia kadhia hiyo, Rais wa Marekani Donald Trump alimwagiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo kuzuru nchi za Saudi Arabia na Uturuki ili kupata picha ya kilichojir­i kwa Khashoggi.

Rais Donald Trump

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.