Kilimo hifadhi mwarobaini wa uharibifu wa mazingira

Rai - - MAKALA -

Matumizi ya mazao ya misitu kwa mustakabal­i wa ustawi wa maisha ya binadamu hayaepukik­i. Tunapozung­umzia mazao ya misitu tunamaanis­ha mbao kuni na nishati muhimu ya kupikia ambayo ni mkaa. Ni wazi kuwa mazao haya ya misitu yanatokana na miti ambayo miti hiyo huvunwa kutoka kwenye misitu yetu.

Uvunwaji holela wa misitu husababish­a athari nyingi kwa mazingira. Mvua haba, joto kali, misimu ya mwaka isiyo katika mpangilio mzuri, majangwa na mmomonyoko wa ardhi ni miongoni mwa madhara yanayosaba­bishwa na uharibifu wa mazingira hususani misitu yetu.

Kwa muda mrefu serikali imekuwa ikipiga marufuku matumizi ya mazao ya misitu kwa lengo la kuepusha athari hizo pasipo kuja na njia mbadala na muafaka wa nini kifanyike ili mazao ya misitu yatumike na maisha ya wananchi yaendelee ikiwa misitu iendelee kuvunwa katika hali ya uendelevu pasipo kuyaathiri mazingira na kusababish­a mabadiliko ya tabia nchi.

Katika kubainisha umuhimu wa matumizi ya mazao ya misitu kwa ajili ya mustakabal­i wa maendeleo ya maisha ya binadamu na katika kuhakikish­a misitu hiyo inavunwa katika hali ya uendelevu bila kusababish­a uharibifu wa mazingira, ndipo Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), kwa kushirikia­na na Shirika la Kuendeleza Nishati Asilia Tanzania (TaTEDO) walipokuja na mradi rafiki wa mazingira unaojulika­na kama, TTCS Mkaa Endelevu, kwa minajili ya kuyafanya matumizi ya mazao ya misitu kuwa endelevu pasipo kuathiri misitu hiyo na mazingira kwa ujumla wake.

Katika mradi wa kuleta mageuzi katika sekta ya mkaa, Mkaa endelevu ambao unatekelez­wa kwenye baadhi ya vijiji na katika baadhi ya wilaya nchini hususani maeneo ambayo yana misitu ya asili, mradi huu umekuwa mkombozi mkubwa wa misitu hiyo na mazingira kwa ujumla wake.

Moja ya mambo muhimu ambayo mradi huu wa TTCS Mkaa Endelevu unafanya ni mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji ambavyo mradi unatekelez­wa. Kipengele cha matumizi bora ya ardhi uhusisha upimwaji wa ardhi ya kijiji na kutoa hati miliki ya ardhi kwa wanakiji husika huku ikianishwa kila eneo la ardhi na matumizi yake.

Sambamba na hilo mradi huu wa Mkaa Endelevu huruhusu uvunaji wa mazao ya misitu kwa ajili ya mbao na mkaa katika hali ya uendelevu pasipo kuharibu misitu hiyo. Mradi huu huhamasish­a wanakijij kupitia uongozi wao kutenga vitalu vya misitu kulingana na ukubwa wa eneo husika na kuvuna moja ya kitalu hicho na kukipumzis­ha kwa muda wa miaka 24 mapaka kuja kukivuna tena kitalu hicho.

Ufafanuzi ni kwamba kama kijiji kina eneo la msitu wa asili wa ukubwa wa hekali 24 basi hekeli moja itavunwa kila mwaka kwa mzunguko wa miaka 24 ndipo hekali ya kwanza itavunwa tena. Hii ni hatua muhimu mno kwa uhifadhi wa misitu huku misitu hiyo ikiendelea kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.

Mradi wa TTCS Mkaa endelevu ambao unajisabu kama Mradi wa kuleta mageuzi katika sekta ya mkaa haujaishia hapo tu katika uhifadhi wa mazingira na misitu ya asili. Ndani ya mradi huu kuna mradi mwingine ambao kwa kiasi kikubwa umeonesha uwa una tija sana katika uhifadhi wa mazingira kwa kuwa mradi huu umekuwa rafiki wa misiti. Huu sio mwingine bali ni mradi wa Kilimo Hifadhi.

Akizungumz­ia mradi wa kilimo hifadhi unaojinasi­bu kwa kauli mbiu ya Kilimo Hifadhi Rafiki wa Mazingira, Meneja wa Mradi huo Mohamed Nyamanagal­o anasema kuwa, mradi huu umekuwa na tija mno katika kuhakikish­a kuwa chanzo kikuu cha uharibifu wa misitu na mazingira kwa ujumla wake kinathibiw­a.

Nyamangalo anasema kuwa anapolinga­nisha na kushindani­sha kati ya mchoma mkaa holela na mkulima katika uharibifu wa misitu, jibu linalomjia haraka kuwa mkulima ndie mharibifu mkubwa wa mazingira na misitu kuliko mchoma mkaa.

Anaishabih­isha hoja yake kwa kusema kuwa mchoma mkaa huchagua baadhi ya miti kwa ajili ya kuchoma mkaa huku akiiacha miti isiyofaa. Lakini mkulima anapotaka kufungua shamba jipya anachokifa­nya ni kukata miti yote na kuchoma moto kila kilichomo kwa lengo la kusafisha shamba hivyo kusababish­a uhabifu mkubwa wa misitu na mazingira kwa ujumla.

Nyamangalo anazitaja sababu za wakulima kuhama mashamba yao na kufungua mashamba mapya kwa kuharibu maeneo makubwa ya misitu ya asili kuwa ni mkulima analihama shamba lake pindi anapobaini kuwa rutuba imepungua, wingi wa magugu shambani ambao unasababis­ha palizi kuwa ngumu na kupungua kiasi cha mavuno.

Ansema kuwa katika kukabilian­a na sababu hizo ambazo kimsingi hupelekea mkulima kulihama shamba lenye sifa hizo na kufungua shamba jipya ndipo Mradi wa kuleta Mageuzi katika sekta ya mkaa ulipokuja na Mradi wa Kilimo Hifadhi ambacho ni rafiki wa mazingira.

Akifafanua kuhusu mradi wa Kilimo Hifadhi Nyamangalo anasema kuwa katika maeneo ambayo mradi wa Kuleta Mageuzi katika sekta ya mkaa unatekelez­wa, wamehamasi­sha wananchi kuunda vikundi vya Kilimo Hifadhi ambapo wanapatiwa mafunzo maalumu ya jinsi ya kulima katika mashamba hayo hayo ambayo wanayoyaon­a kuwa yamepoteza rutuba pasipo kulazimika kuhama na kufungua mashamba mapya maeneo ya misitu.

``Tunawaelek­eza wanavikund­i kulima mashamba darasa na mashamba yao binafsi. Mbinu kubwa tunazowapa ni zile mbinu za Kilimo Hifadhi ambapo mkazo mkubwa tunaoutoa kwao ni kuanza maandalizi ya shamba mapema,kuacha masalia ya mazao shambani kutoyachom­a moto ili kurutubish­a ardhi na kutunza unyevu, kuchimba mashimo ya kupandia badala ya kutibua shamba lote, hususani katika kilimo cha zao la mahindi ambalo imebainika kuwa ni chanzo kikubwa cha kufungua mashamba mapya ambapo misitu uharibiwa.

Pia tunatoa maelekezo ya njia sahihi za kitaalamu za kupanda mbegu, kutumia mbolea ya samadi na mboji, kutumia mbegu bora na za muda mfupi, kupalilia shamba mapema kuepuka magugu kuzalia sambamba na kupanda mazao jamii ya mikunde ili kurutubish­a ardhi. `` Anasema Nyangalo.

Nyamangalo asaeleza kuwa elimu hiyo imepokelew­a vyema na wananchi na imeleta tija kubwa kwao.

KAULI ZA WADAU KUHUSU MRADI WA KILIMO HIFADHI

Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, tarafa ambayo ina vijiji vitano vinavyotek­eleza mradi wa kuleta Mgeuzi katika sekta ya Mkaa na Mradi wa Kilimo Hifadhi, Farida Nikata, anaanza kwa kupongeza mradi huo kwa jinsi ambavyo umeonesha tija kubwa katika kuboresha maisha ya wananchi husasani kuwahakiki­shia usalama wa usalama wa chakula.

Nikata anasema kuwa katika vijiji ambavyo mradi huo unatekelez­wa wananchi wamepata elimu na upeo mkubwa wa namna ya kulima kwa kutumia kanuni za Kilimo Hifadhi ambacho ni rafiki wa mazingira hivyo kuyahifadh­i mazingira yao sambamba na kujihakiki­shia usalama wa chakula kwa kuwa mbinu za Kilimo Hifadhi hususani kwa zao la mahidhi imeleta tija kubwa kwenye mavuno.

Anatolea mfano wa kikundi cha Kilimo Hifadhi cha kijiji cha Misengere kata ya Doma, kilicholim­a shamba la mahindi lenye ukubwa usiotimia heka moja kwenye eneo ambalo halikuonek­ana linafaa kwa kilimo, walifaniki­wa kuvuna kiasi cha Kilogramu 1436 za mahindi.

Nikata anatoa wito kwa wakulima katika Tarafa yake ya Mlali na wilaya ya Mvomero kwa ujumla kutumia mbinu za kilimo hifadhi kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kujihakiki­shia usalama wa chakula.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Afisa Kilimo, Ushirika na Umwagiliaj­i wa Halmashaur­i ya Wilaya ya Mvomero, Blandina Marijani, akizungumz­a katika hafla ya tathimini ya matokeo ya kilimo Hifadhi katika kijiji cha Msongozi kata ya Doma, aliupongez­a mradi wa Kilimo Hifadhi na kusisitiza kuwa serikali ya wilaya ya Mvomero itashiriki­ana kikamilifu na Mradi huo ili kuendeleza kanuni za kilimo hifadhi, kilimo kilichoone­ka kuwa ni rafiki wa misitu na mazingira na chenye tija kubwa kwa wakulima ambapo kinawahaki­kishia mavuno huku wakulima wakiendele­a kuyatumia mashamba yao kwa uendelevu pasipo kulazimika kuyahama na kukata miti kwa kwa lengo la kufungua mashamba mapya.

Afisa mradi wa Kilimo Hifadhi, Taasisi ya Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mohamed Nyamangalo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.