Soda ya bosi yamponza mfanyakazi wa ndani

Rai - - MAKALA AFRIKA - NA HASSAN DAUDI

KABLA ya kuanza kuusimulia mkasa huo, nikufahami­she tu kuwa soda chupa moja nchini Nigeria inapatikan­a kwa kiasi cha Naira 100 (Sh 600 za Tanzania) tu.

Kwamba siku hizi hicho ni kiasi cha fedha kisichowez­a hata kukuwezesh­a kupata mlo mmoja na aghalabu kimekuwa sehemu ya matumizi ya watoto.

Hata hivyo, hiyo haikumzuia mwajiri aliyefaham­ika kwa jina la Sarah Eteigbe kumtendea unyama mfanyakazi wake wa ndani, ambaye cha kusikitish­a zaidi, ni kijana mwenye umri wa miaka 12 tu.

Tukio lilikuwa hivi, mwanamama Sarah anayeishi Bariga, Lagos, aliiweka soda yake aina ya 7up kwenye friji, akitarajia kuikuta ikiwa na ubaridi wa kutosha hapo baadaye.

Hata hivyo, alipokwend­a kuichukua baada ya kuisikiliz­ia kwa saa kadhaa, hakuikuta soda yake na ndipo alipogundu­a kuwa ni Obi ndiye aliyeinywa.

Kwa mujibu wa gazeti la Vanguard Nigeria, kitendo hicho kilimkera mwanamke huyo na kilichofua­ta ni kumchoma kwa pasi ya moto dogo huyo.

Siri hiyo ilifichuka baada ya mwalimu wa Obi kugundua kuwa shati la Obi lilikuwa na michirizi ya damu na alipomuuli­za, ndipo dogo huyo aliposema amefanyiwa unyama huo, tena akiitaja sababu kuwa ni soda.

Obi aliendelea kumfunguki­a mwalimu wake akisema tangu siku alipoinywa soda hiyo bila ruhusu ya Sarah alikumbana na vipigo vya hapa na pale.

Mmoja kati ya majirani wa Sarah alisema walishitus­hwa na namna Obi alivyokuwa akiibuka na majeraha ya mara kwa mara yaliyotoka­na na adhabu na hawakufura­hia kuona akizuiwa kucheza na wenzake.

Akisimulia mateso mengine anayosema yalitokana na hasira za soda ile, hapa Obi analiambia jeshi la polisi baada ya majirani kumfikisha bosi wake mbele ya sheria.

“Alikuwa akinipiga mara kwa mara. Kuna kipindi aliwahi kunichana na wembe,” alisema Obi aliyeanza kuishi na Sarah tangu mwaka 2014.

Hapa Obi anafichua kilichomsu­kuma kunywa soda ya Sarah na kujikuta akiingia katika mateso ambayo anasema ameyapata kwa miaka minne sasa. “Siku hiyo nilichelew­a kutoka shule, hivyo hakukuwa na chakula. Hapo ndipo nilipoamua kunywa soda kupoza njaa,” anasema.

Kutokana na ufedhuli wake huo, Sarah ameswekwa katika gereza la wanawake akisubiri Desemba 3, mwaka huu, siku ambayo kesi yake itasikiliz­wa.

Huenda angetolea kwa dhamana lakini ameshindwa kukidhi vigezo vya mahakama, yaani kuwa na kiasi cha Naira 200,000 (zaidi ya Sh mil. 1.2 za Tanzania).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.