Ligi Kuu ya Tanzania Bara vigogo wakabana

Rai - - MICHEZO - NA MWANDISHI WETU

LIGI Kuu ya Soka Tanzania Bara inazidi kushika kasi, huku vita ya kukaa kileleni ikiwania na vigovo vya soka nchini.

Ligi hiyo ambayo ambayo wiki hii itasimama kupisha kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kuwa wazi kuanzia Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu inasimama ikiwa imecheza mechi katika raundi kati ya 10 na 13 tu.

Michuano ya Ligi Kuu inasimama kwa takribani mwezi mbali na kutoa nafasi ya usajili drisha dogo lakini pia itapisha kufanyika kwa mechi za kuwania kufuzu fainali zijazo za Afcon ambapo taifa Stars itacheza na Lesotho ugenini Novemba 18 mwaka huu.

Vilevile ligi hiyo inapisha kufanyika kwa mechi za awali za michuano ya kimataifa inayoandaliwana Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), ambapo Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa barani Afrika huku Mtibwa wao wakiwakilisha katika Kombe la Shirikisho.

Mpaka sasa Azam ndio aliyekamata usukani wa ligi hiyo akiwa na pointi 30 kutokana na mechi 12 huku akifuatiwa na Simba yenye pointi 26 kwa mechi 11, Yanga ikiwa ya tatu kwa pointi 26 kutokana na michezo 10.

Mtibwa Sugar wao wanakimbiza wakiwa katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 23 kwa michezo 13 huku Coastal Union wakiwa katika nafasi ya tano kwa pointi 19 kutokana na mechi 13.

Kusimama kwa ligi hiyo dhahiri kunaweza kuiacha Azam kileleni mpaka hapo Desemba mwaka huu itakapoendelea tena kutokana na ukweli kuwa wanaomfuatilia kwa karibu nao hawatacheza hadi kumalizika kwa mapumziko hayo mafupi kwa timu.

Kati ya timu hizo, tishio ni Simba naYanga kwani zina mechi pungufu kufikia idadi ya mechi ilizocheza Azam japo timu kama Mtibwa naye ana uwezo wa kumpiku kinara kileleni kama atashinda mechi zake zijazo huku akiziombea mabaya zilizo juu yake kupoteza michezo yao.

Licha ya ukweli kuwa ushindani wa kukalia kiti ikiwa ni safari ya kulisaka taji la ligi hiyo linaloshikiliwa na Simba ni mkali laki ni hata hivyo msisimko umebaki kuwa mdogo kwa baadhi ya timu tu kutokana na changamoto kadhaa zinazoikabili.

Hata hivyo Ligi hiyo ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto ya ratiba kwa mechi kuahirishwa kutokana na kugongana na program ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ inayojiandaa na mechi za kufuzu fainali za Afcon mwakani imepunguza mvuto kwa kiasi kikubwa.

Moja kati ya changamoto kubwa ni ratiba ambayo inatoa mwanya kwa baadhi ya timu kucheza mechi nyingi ilihali zingine zikiwa na mechi chache.kati ya 10 na 14 ambazo kimsingi hata nusu ya mechi za ligi bado kwani .

Kwa mfano wakati ligi inasimama kuna timu zitakuwa zimecheza mechi hadi za raundi ya 14 wakati zingine bado zina viporo kati ya vitatu hadi vinne.

Wakati mechi za Simba, Yanga na Azam zinasimama kutokana na timu hizo kutoa wachezaji wengi katika timu ya taifa timu zingine wao wiki hii watamalizia kucheza mechi za raundi ya 14 kabla ya kusimama kupisha dirisha dogo.

Changamoto nyingine ni ukata unaozinyemelea timu nyingi kiasi cha kukwama kusafiri na kuishia kutembeza bakuli huku zingine zikikopa kwa TFF.

Ufanisi wa timu nyingi umepungua kutokana na ligi kukosekana kwa mdhamini mkuu hivyo kuzifanya timu kupungukiwa na moja kati ya chanzo kikuu cha fedha.

Licha ya changamoto hizo, hata hivyo bado timu za Azam, Yanga na Simba zinaonyesha kuwa na uchu wa kulitwaa taji hilo kutokana na tofauti ndogo ya pointi zilizopo kati yao.

Ukweli Azam inalitaka taji hilo lililoitema misimu minne iliyopita huku Yanga wao wakitaka kulirejesha pia kutoka kwa mtani wake kama ambavyo alinyang’anywa nao msimu uliopita.

Wakati Ligi itasimama kupisha mechi za CAF, dirisha dogo, Bodi ya Ligi Kuu inapaswa kuiangalia kwa jicho la tatu ratiba hiyo ili kuepuka baadhi ya timu kumaliza mechi zake huku zingine zikiwa na viporo hali ambayo itaondoa haki sawa ya kupambana.

Kikosi cha Yanga

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.