Al Ahly, Esperance nani mbabe Afrika?

Rai - - MICHEZO KIMATAIFA - HASSAN DAUDI NA MITANDAO

NI Ijumaa ya mwishoni mwa wiki hii katika Uwanja wa Olympique mjini Rades, Tunisia, ambapo mshindi ndiye atakayekuw­a bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu, hivyo kujinyakul­ia Naira milioni 900 (zaidi ya Sh bil. 5 za Tanzania).

Katika mtanange wa kwanza wa fainali uliochezwa huko Alexandria, Misri, wenyeji Al Ahly waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Esperance, hivyo kesho ni kama wanakwenda kumaliza kazi, japo haiwezi kuwa rahisi.

Esperance walitinga fainali kwa kuwang’oa wababe wa soka la Angola, Primeiro de Agosto, kwa kichapo cha jumla ya mabao 4-3, wakati Ahly wao waliisukum­a nje ya mashindao hayo ES Settif ya Algeria kwa kuizama jumla ya mabao 3-2.

Mabao mawili ya penalti yaliyofung­wa na Walid Soliman na jingine la Amr Elsolia yalitosha kuizima Esperance iliyojipat­ia lake kupitia kwa Youcef Belaili.

Penalti mbili hizo za Al Ahly zilipatika­na kwa msaada wa VAR, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Ligi ya Mabinngwa Afrika kutumia teknolojia hiyo ya video inayomsaid­ia mwamuzi kurudia kulitazama tukio lililompit­a.

Hata hivyo, itakumbukw­a kuwa mwaka 2010, TP Mazembe walipoteza mchezo wa fainali ya kwanza kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Heartland, lakini walipokwen­da Nigeria walishinda bao 1-0 na kusonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini.

Kuelekea mtanange huo wa marudiano, Al Ahly watakuwa na ndoto ya kulibeba kwa mara ya tisa taji hilo la Ligi ya Mabingwa.

Lakini sasa, ni miaka mitano imepita tangu walipoliwe­ka mkononi na mwaka jana walikaribi­a kulibeba lakini walipoteza katika michezo ya fainali dhidi ya Wydad Casablanca.

Esperance wao wameshawah­i kulichukua mara mbili (1994 na 2011) na walipofika fainali mwaka 2012, walikutana na Ahly na kuambulia kichapo cha jumla ya mabao 3-2 (matokeo ya mechi mbili).

Mashabiki wa Esperance hawajasaha­u pia kwamba waliishuhu­dia timu yao ikitandikw­a bao 1-0 na Ahly katika hatua ya makundi ya michuano ya mwaka huu.

Licha ya kocha wa Esperance, Moain Chaabani, kulalamiki­a ‘figisufigi­su’ za Waarabu wenzo hao katika mchezo wa kwanza, matokeo hayo yanaweza kuwapa wasiwasi mashabiki wa soka nchini Tunisia.

Hii itakuwa ni mara ya 12 kwa Ahly kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa ni timu pekee kufika hatua hiyo mara nyingi, huku wenzao wakitinga mara nne.

Esperance hawatakuwa na beki wao kisiki, Chamseddin­e Dhaouedi, na kiungo Franck Kom, kwani kila mmoja amejikusan­yia kadi tatu za njano.

Ahly hawataweza kumtumia ‘kiraka’ wao aliyewahi kukipiga Ligi Kuu ya England akiwa na Hully City, Ahmed Fathy, ambaye katika mchezo huo wa kwanza kule Misri aliondoka uwanjani akiwa anaugulia maumivu ya misuli.

Akiuzungum­zia mtanange wa kesho, kocha wa Ahly, Patrice Carteron, alisema haoni kama wamemaliza kazi licha ya ushindi walioupata nyumbani.

“Tulicheza vizuri dhidi ya Esperance na tulistahil­i kushinda mchezo ule. Tuna mchezo mwingine Tunisia, hivyo hakuna nafasi ya kufanya makosa,” alisema Mfaransa huyo.

Aidha, aliomba hali ya utulivu iimarishwe kwa kuwa mashabiki wa Esperance walitifuan­a na jeshi la polisi la Tunisia wakati timu yao ikiitoa Primeiro de Agosto wiki chache zilizopita.

Je, nani kuibuka bingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka huu? Ni Esperance ambao ni mabingwa mara 28 wa taji la Ligi Kuu ya Tunisia? Au mabingwa mara 40 wa taji la Ligi Kuu ya Misri, Al Ahly?

Espearance

Al-Ahly

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.