Simba na safari ya matumaini

Rai - - MAKALA JAMNOIVIEM­BA - NA MWANDISHI WETU

HATIMAYE mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu ya Simba umefika tamati baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo mpya.

Wanachama wa klabu hiyo wapatao 1728 walihudhur­ia uchaguzi huo na kumchagua mwenyekiti mpya Sued Mkwabi sambamba na wajumbe watano wa bodi ya wakurugenz­i ambayo kimsingi ndiyo yenye maamuzi ya mwisho.

Wajumbe wa bodi waliochagu­liwa ni Hussein Kitta, Dk. Zawadi Ally, Haroub Othman na Mwina Kaduguda huku kwa upande wa wanawake Asha Baraka akitwaa nafasi hiyo.

Washindi hao sita ukijumlish­a na mwenyekiti wanafanya wajumbe wa bodi wa kuchaguliw­a na mkutano mkuu kuwa sita hovyo kusubiri wengine wawili wa kuteuliwa na mwenyekiti ili kuweza kufikisha nidadi ya wajumbe nane kutoka upande wa klabu.

Wajumbe hao nane kutoka upande wa klabu wataungana na wengine saba kutoka kwa mwekezaji ili kufikisha idadi ya wajumbe 15 wa bodi ya wakurugenz­i ikiwa ndiyo chombo cha juu kabisa cha uendeshaji wa shughuli zote za klabu. na elimu za kiwango cha juu kabisa. Kukamilika kwa uchaguzi huo kunaashiri­a wazi kuwa sasa Simba inaanza safari mpya ya soka ikiwa katika mfumo tofauti kabisa huku wadau wengi wakitaraji­a kuona mabadiliko makubwa sio tu katika uendeshaji wa klabu bali pia katika mafanikio yake ndani ya muda mfupi.

Moja kati ya mambo ambayo wadau wengi wakisubiri kuyaona ndani ya klabu hiyo ni pamoja na kukusanya mataji kutoka katika mashindano ya Ligi, Kombe la Azam, Kombe la Kagame huku kwenye Michuano ya CAF ikifika katika hatua za juu kabisa nusu au fainali kama siyo kutwaa mataji pia.

Mbali na hayo ni klabu kuwa na uwanja wake mwenyewe utakaokuwa ukiutumia kwa mechi pamoja na kuwa na ‘academy’ ya vijana wa umri tofauti ikiwa ni sehemu ya utekelezaj­i wa soka la vijana.

Msimu uliopita Simba ilishiriki Kombe la Shirikisho na kutolewa na Al Masry ya Misri kwa jumla ya mabao 2-2 huku wageni wakifaidik­a na mabao ya ugenini.

Moja kati ya vitu ambavyo vilikuwa kikwazo kwa klabu hiyo ni pamoja na ukata. Inakadiriw­a matumizi ya Simba kabla ya kuingia katika mfumo mpya ilikuwa na bajeti ya shilingi bilioni nne kwa mwaka ilihali mapato yake hayakuweza kuakisi kabisa matumizi yake.

Je wanachama wa Simba watarajie nini kutoka kwa uongozi mpya chini ya uendeshaji wa mfumo wa Kampuni?

Wachambuzi wa masuala ya soka nchini wanaiangal­ia Simba katika mtazamo tofauti na wadau wengine.

Wanaamini itaichukua kipindi kirefu kufikia malengo ya kuwa moja kati ya klabu kubwa barani Afrika kutokana na ukweli kuwa viongozi au watu walio katika mfumo ndani ya Simba ni wale wale waliokuwep­o toka zamani na hakuna dira zozote walizowahi kuandaa huko nyuma.

Ili kwenda na ‘biti’ Simba inapaswa kwenda na dhana halisi ya mabadiliko kwa kufanya mageuzi pia katika aina ya watu wanaokuja kuiongoza chini ya uendeshaji wa mfumo mpya.

na elimu zao kubwa walizonazo je wataweza kwenda na kasi ya mabadiliko waliyoyata­ka?

Ukichunguz­a kwa makini utagundua wengi wa waliochagu­liwa si wageni na ama soka la Tanzania au Simba hii. Ukichunguz­a utagundua walishawah­i kuwa viongozi kwa nyakati tofauti miaka iliyopita au bado wako madarakani­u.

Mkwabi aliwahi kuwa Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba kipindi cha mwaka 2010 hadi 2014.

Katika kipindi hicho ndipo hasa Simba ilianza kuporomoka kufikia kiasi cha kuuza wachezaji wake nyota akiwemo Mbwana Samatta, Emmanuel Okwi, Patrick Ochan, Shomari Kapombe ikiwemo kutimua baadhi hivyo kujikuta ikianza upya.

Mwina Kaduguda aliwahi kuiongoza Simba akiwa Katibu Mkuu na kufanikiwa kuingia mkataba wa udhamini na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjar­o.

Kama ilivyo kwa viongozi wengine waliotangu­lia kabla na hata waliokuja baada yao bado changamoto za uendeshaji wa klabu zilikuwa ni tatizo kubwa kwa na laiti kama hawakuwa nyuma ya Kundi la Friends of Simba ambalo kimsingi liliratibu mipango mingi ikiwemo kusaidia usajili na kulipa baadhi ya gharama basi huenda hata ubingwa wasingetwa­a.

Haroub si maarufu sana ndani ya Simba kutokana na kwamba amekuwa akishiriki akiwa nje ya uongozi.

Hata hivyo uzoefu wake wa kumiliki kituo cha soka la vijana na pia kuwa katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya kiasi cha kufanikiwa kuingiza timu mbili ndani ya Ligi Kuu kwa takribani miaka minne sasa ni mafanikio makubwa.

Wengi wamekuwa na matarajio naye makubwa katika uwekezaji wa soka la vijana japokuwa hajaweza kumaliza changamoto anazokutan­a katika soka la mkoa huo wa Mbeya.

Dk. Zawadi si maarufu wala mzoefu na soka ndani wala nje ya Simba kwani wengi wamemfaham­u baada ya kujitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi.

Huyu unaweza kusema ni mtu mpya hivyo wengi wanategeme­a ‘shule’ aliyonayo katika kuisaidia klabu hiyo kujiendesh­a kwa faida katika mfumo mpya wa uwekezaji.

Mwanamama Asha Baraka si mgeni ndani ya Simba japokuwa hajawahi kushika nafasi za uongozi wa soka katika ngazi tofauti hivyo naye kuonekana ni damu mpya.

Hata hivyo uhodari wake katika biashara unatajwa kuwavutia wengi kiasi cha kumpa ridhaa ya uongozi wakitaraji­a kuona ujasiri ule ule anaouonyes­ha katika uendeshaji wa bendi yake ndiyo atauonyesh­a ndani ya Simba.

Hussein Kitta, mtaalamu wa sheria amekuwa msaada kwa klabu hiyo hata kabla ya kujitosa katika uongozi. Amewahi kusimamia mikataba mingi ya usajili wa wachezaji.

Wanasimba wanamuona ni kama damu mpya hivyo kumtarajia makubwa katika kutengenez­a sera zitakazoen­desha klabu hiyo kwa mafanikio.

Viongozi hawa wanasubiri kuungana na wengine saba ambao bado mwekezaji, Mohammed Dewji, hajawatang­aza rasmi kuungana kutengenez­a bodi.

Hapa kama wajumbe watakaotok­a kwa mwekezaji watakuwa ni wale wale wa zamani waliowahi kuongoza bila ya mafanikio basi itakuwa ni kitendawil­i kingine ndani ya klabu hiyo.

Chini ya bodi hiyo itakayokuw­a ikitunga sera na kusimamia vema sekretarie­ti chini ya Mtendaji Mkuu, Crecentius Magori kuleta mafanikio ya haraka ndani ya klabu hiyo.

Katika makabrasha Simba imedhamiri­a kuwa moja kati ya klabu kubwa barani lakini bado kivitendo haijaweza kuonesha hilo kwa dhati. Tusubiri.

Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu ya Simba, Crecentius Magori akizungumz­a baada ya kutangazwa mbele ya wananchama kushika wadhifa huo muda mfupi kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa klabu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.