Itakuwa ngumu Conte kwenda Real Madrid

Rai - - MBELE -

HIVI sasa kikosi cha Real Madrid kiko chini ya kocha wa muda, Santiago Solari, ambaye kabla ya kupewa nafasi hiyo alikuwa akiinoa timu ya vijana. Baada ya kumtimua Julen Lopetegui, bado Madrid wanaendele­a na harakati za kusaka atakayekik­alia kiti chake

Lakini sasa, wachambuzi wa soka barani Ulaya wanaamini huenda Conte akaikataa ofa yoyote atakayowek­ewa mezani na mabosi wa Madrid. Kwanini?

Kwanza, mkufunzi huyo haonekani kuwa tayari kurejea haraka katika soka, hasa baada ya changamoto aliyokutan­a nayo msimu uliopita akiwa na Chelsea.

Kuinoa Madrid ni moja kati ya vibarua vigumu katika soka kutokana na klabu hiyo kuwa na utamaduni wa kutimua makocha mara kwa mara.

Kuingia katika kazi iliyowahi kuwashinda makocha wenye CV kubwa katika ulimwengu wa kandanda, Vicente del Bosque, Fabio Capello na Jose Mourinho, inahitaji ujasiri, jambo ambalo kwa sasa Conte anaweza asiwe nalo baada ya kutimuliwa Chelsea.

Conte mwenye umri wa miaka 49, hajapumzik­a tangu alipoanza kazi ya ukocha mwala 2007, hivyo kile kilichomku­ta pale Chelsea, ikiwamo kukorofish­ana mara kwa mara na wachezaji, inaweza kuwa sababu nzuri ya kutaka kukaa mbali na soka, walau kwa muda kidogo.

Hata katika moja ya mazungumzo yake na waandishi wa habari, aliwahi kuweka wazi kuwa haoni kama atakuwa mkuu wa benchi la ufundi hivi karibuni.

Pili, kuna hili la kibarua pale Manchester United. Ikizingati­wa kuwa Ligi Kuu ya England (EPL) imekuwa ikiwavutia wanasoka, makocha na mashabiki wengi, si ajabu hata Conte anatamani kubaki. Akiwa anajua kabisa kwamba mwenzake, Jose Mourinho, ana wakati mgumu katika kibarua chake cha kuinoa Man United, Conte anaamini anaweza kuitwa Old Trafford.

Ni kweli mkataba wake na Chelsea haumruhusu kufanya kazi England hadi pale msimu huu utakapomal­izika lakini kama ni Man United atakuwa tayari kusubiri hata mwakani.

Kuna taarifa kuwa amekuwa akiamini kuwa ndiye atakayepew­a kazi ya kuliongoza benchi la ufundi la Mashetani Wekundu, ingawa hilo litategeme­a na mwenendo wao chini ya Mourinho.

Bado Mourinho ana mkataba na kama timu itakuwa kwenye kiwango kizuri kwa miezi sita ijayo, hakuna ubishi kuwa mabosi wa Man United hawataona umuhimu wa kumfukuza kocha huyo wa kimataifa wa Ureno.

Tatu, inaonekana ni ngumu kwa Conte kwenda Madrid kutokana na ukweli kwamba baadhi ya mastaa wa Santiago Bernabeu hawamtaki.

Pindi tu zilizoibuk­a taarifa zilizomtaj­a Conte kuwa ndiye atakayekuw­a kocha wao, walionesha wazi kutokubali­ana na suala hilo.

Orodha ya wachezaji wanaopinga kuwa chini ya Conte haijawekwa hadharani lakini inafahamik­a kuwa Madrid ina Sergio Ramos, Marcelo Toni Kroos ambao wanatajwa kuwa na ushawishi mkubwa kikosini na hata kwa mabosi.

Inaelezwa pia sehemu ya wasiomtaka kocha huyo ni wale wanaoamini kuwa ujio wake utawanyima nafasi ya kucheza mara kwa mara. Mfano; hakuna ubishi kuwa Keylor Navas hatakaa langoni kwa kuwa Thibaut Courtois na Conte wanajuana vizuri tangu walipokuwa Chelsea.

Katika hilo, hata Gareth Bale anaweza asifurahis­hwe na ujio wa Conte, akijua wazi kwamba kocha huyo atataka Eden Hazard asajiliwe, jambo linaloweza ‘kuuzika’ ufalme wake Bernabeu.

Kama si Hazard aliyewahi kufanya naye kazi Stamford Bridge, Conte anaweza kuwashawis­hi Madrid wamuuze Bale ili kiasi cha fedha kitakachop­atikane kiongezewe kumvuta Neymar.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.