NI MATUMIZI GANI TUNAYOYABANA?

Rai - - MBELE -

Novemba mwaka 2015 wakati Rais John Magufuli akitoa hotuba ya kulizindua Bunge, alifafanua vizuri vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano.

Mojawapo ya eneo alilolifafanua kwa kina ni suala la matumizi mabaya ya fedha za umma. Rais alifafanua kwa mifano ni jinsi gani nchi ilivyokuwa ikipoteza fedha katika matumizi yasio ya lazima nitanukuu sehemu ya hotuba ile nanukuu.

Mheshimiwa Spika;

Nitataja baadhi tu ya maeneo ambayo tutayasimamia kwa lengo la kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za Serikali:

Kwanza, safari zote zisizo za lazima nje ya nchi Serikalini tutazidhibiti na badala yake tutawatumia mabalozi wetu kutuwakilisha kwenye mikutano ya aina hiyo. Na pale inapolazimu kiongozi au mtumishi mwandamizi kusafiri tutahakikisa kwamba haandamani na msururu wa watu wengi ambao hawana umuhimu wala shughuli za kufanya katika safari hizo.

Katika kusisitiza hili napenda niwape takwimu za fedha zilizotumika ndani ya Serikali, Mashirika ya Umma na Taasisi nyingine za Serikali kwa safari za nje kati ya mwaka 2013/14 na 2014//2015. Jumla ya shilingi bilioni 356.324 zilitumika kwa ajili ya safari za nje kama ifuatavyo:

t 5JLFUJ [B OEFHF "JS UJDLFU

zilitumia shilingi bilioni 183.160;

t .BGVO[P OKF ZB ODIJ 5SBJOJOH 'PSFJHO [JMJUVNJB TIJMJOHJ CJMJPOJ

68.612;

t 1PTIP [B LVKJLJNV 1FS %JFN 'PSFJHO [JMJUVNJB TIJMJOHJ CJMJPOJ 104.552;

Wizara na Taasisi zinazoongoza kwa matumizi ya safari za nje ni pamoja na Bunge, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

XB )FTBCV [B 4FSJLBMJ /"05 Wizara ya Mambo ya Ndani, n.k.

Hizi fedha zingeweza kutumika vizuri kuboresha huduma za wananchi wa maisha ya chini, kama afya, maji, elimu, umeme n.k.

Mfano; fedha hizi zingetosha kutengeneza kilometa 400 za barabara za lami, tujiulize zingeweza kutengeneza zahanati ngapi?, nyumba za walimu ngapi?, madawati mangapi? n.k. Hivyo tunapodhibiti safari za nje tunawaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote mtuelewe na mtuunge mkono.”

#Mwisho wa Kunukuu kipengele cha hotuba hii ya Rais ambayo kwangu ni Hotuba bora kabisa kuwahi kuisikia toka kwa kiongozi mkuu wa nchi.

."6%)6* :" ,*1&/(&-& HICHO yalikuwa ni kuwataka watanzania kuheshimu fedha na hasa Kodi za wakulima na wafanyakazi wa taifa hili katika kufanyia mambo ya msingi.

CHA KUSHANGAZA.

Inawezekana bado hatukumwelewe Rais kwa kuwa kwa mwelekeo ulivyo tunaweza kwenda kuvunja Rekodi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma. Nitaongelea eneo moja tu la fedha tunazochezea kwa hizi chaguzi ndogo.

Mpaka kufikia tarehe 4/9/2018 Zaidi ya madiwani 146 walikuwa tayari wameshahama vyama. Kwa upande wa wabunge hadi sasa tumeshuhudia wabunge watatu XB $IBEFNB %L (PEXJO.PMMFM 4JIB .XJUB 8BJUBSB 6LPOHB +VMJVT ,BMBOHB .POEVMJ BNCBP wamehamia CCM ambako wameteuliwa tena

kugombea majimbo hayo katika uchaguzi mdogo. Wabunge wengine ni Maulid .UVMJB ,JOPOEPOJ OB ;VCFSJ .PIBNFE -JXBMF XPUF LVUPLB $IBNB DIB 8BOBODIJ $6' ambao wamehamia CCM huku Lazaro Nyalandu toka CCM akihamia chadema na kufanya jumla ya wabunge sita ambao wameturudisha kwenye uchaguzi.

UCHAGUZI NI GHARAMA

Ukiona uchaguzi mahali ujue VNFUVNJB HIBSBNB (IBSBNB hizi hujumisha uchapaji wa karatasi, wasimamizi, walinzi wa Kura ambao ni vyombo vya Dola, Mawakala, kampeni nk.

Aliwahi kukaririwa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi aliyepita ndugu Kailima kuwa uchaguzi mdogo wa Novemba 26, 2017 kwenye kata 43 tulitumia Sh2.5 bilioni. Ukichukua kata hizo 43 ukazigawia uwiano sawa wa hizo shilingi bilion 2.5 kila kata ilitafuna shilingi milioni 58.

Kama hali ndio hiyo chukua kata zote 146 ambazo zimerudiwa uchaguzi zidisha kwa milioni 58 tayari tutakuwa tumeshatupa shilingi bilion nane na miloni mia

OOF 1PJOU

Fedha hizi za madiwani tu zingetosha kuanzisha vikundi vya vijana vya watu 50 vikundi zaidi ya 146 na kuwapatia mikopo ya kila kikundi milioni 100 ya kuanzisha saccos na hivyo kupunguza ajira kwa vijana. Hapa madiwani pekee wangeweza kugusa maisha ya vijana 7500 hadi 10,000 hiki ni kiwanda tumekizika tukiwa tunaona kwa kisingizo cha Demokrasia ambayo hata wamarekani hawathubutu kufanya aina ya Demokrasia hii tunayoifanya.

#Hapa sijaingiza gharama za Majimbo ..... huu ndio mwelekeo tunashona kiraka huku tunatoboa upande wa pili na bado kuna watu wanashangilia.

Tunafanya nini au ni matumizi gani tunabana kama tunahangaika kuzuia watumishi hewa lakini tunapoteza fedha kwa ajili ya uchaguzi usiokuwa na maana tunafanya nini au tunajipongeza kwa kubana matumizi yapi?

Kitendo cha CCM kuendelea kuwapa nafasi za kugombea wanaohama wanachochea upotevu huu wa fedha.

#Aidha mimi ndio sikumwelewa Rais au kina Dr Bashiru Ally ndio hawajaelewa dhana ya kubana matumizi. Mpaka tufikie 2020 tunaweza kuifikia Serikali ya awamu ya nne kwa matumizi mabaya fedha za umma. Ccm yangu ielewe kuwa fedha hizi zingeweza kugusa maisha ya wafanyakazi wa nchi hii kwa kuwaongezea mishahara ambayo kwa miaka 3 hawajaongezewa. Tungeweza kuzitumia kusomeshea wanachuo wangapi ambao walikosa mikopo?

Nini tunafanya kama wananchi watajibana hivi na kinachopatikana tunakitupa? Tungepeleka kwenye afya fedha hizi si zingetusaidia?

ETI NI TAKWA LA KISHERIA.

Sheria inayotufilisi ni sheria ya Kushangilia? Ni mara ngapi tumekuwa tukibadili sheria zetu ili zituhudumie ipasavyo? Kwa nn tusiibadili ili anayehama ahame na Ubunge wake? Kwa nini kwa sasa tusiwazuie kwa kufuata katiba yetu ya Ccm? Tunafanya hivi kwa manufaa gani? Sheria zetu zinatakiwa zituhudumie sio kutufilisi. Ole Mushi 0712702602

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.