YENNENGA, MAMA WA UFALME WA MOSSI, BURKINA FASO

Rai - - MBELE -

KATIKA kumbukumbu za historia ya Bara la Afrika, miaka 1000 iliyopita kulikuwa na dola iliyoitwa Mossi (Mossi Kingdom). Ramani ya dola ya Mossi ianaonyesh­a kuwa katika nchi ya Burkina Faso ya leo. Katika kipindi cha dola ya Mossi haikuwepo nchi ya Burkina Faso kama inavyojuli­kana sasa. Kumbukumbu za kihistoria zinasema kuwa Dola ya Mossi iliibuka baada ya Malkia Yennenga (Binti wa mfalme) kutoroka nyumbani kwao na kwenda kuoana na mwindaji mmoja wa wa tembo na kisha kuzaa naye mtoto wa kiume.

Historia inaonyesha Princess Yennenga alikuwa binti kipenzi cha Mfalme wa Dagomba, Nedega ambaye alitawala katika karne ya 12. Princess Yennenga anatajwa kuwa mwanamke mwenye haiba nzuri, maarufu na mmoja wa askari wa kikosi cha Mfalme huyo. Princess Yennenga akiwa na miaka 14 tu alipigana vita dhidi ya dola jirani ya Malinkes. Lakini umri wa kuolewa ulipowadia, baba yake alikataa katakata kuwa Princess Yennenga hatoolewa na mwanaume yeyote akihofia kumpoteza askari wake mahiri katika kikosi chake na binti wa pekee katika familia yake.

Baada ya kusikia hilo,, Princess Yennenga alikuwa mwenye huzuni nyingi kwa sababu alitamani kuwa na ndoto ya kuolewa na kupata mtoto wake.

Ili kumwonyesh­a baba yake kuwa hajakubali­ana na uamuzi aliotoa dhidi yake, Yennenga aliamua kufanya vituko.

Mojawapo ya kituko hicho ni kupanda mbegu za mtama na kutekeleza shamba, hivyo pale muda wa mavuno ulipowadia, aliamua kuyaacha yaoezene shambani badala ya kuvuna.

Baba yake alimhoji ni kwa nini alitenda kitendo hicho, Princess Yennenga alieleza kuwa alifanya vile kama yeye baba yake alivyozuia kwenda kuolewa.

Kutokana na kitendo hicho Mfalme Nadega alimfunga jela Princess Yennenga. Hata hivyo mara baada ya kuwekwa jela, alitoroshw­a kwa kuvalishwa mavazi kama ya mwanaume.

Yennenga alikuwa binti muhimu wa ufalme wa watu wa Mossi katika sehemu ya nchi Burkina Faso. Yeye alizaliwa miaka 900 iliyopita. Baba yake alikuwa mfalme wa Dagomba katika karne ya 12. Eneo la ufalme wa Dagomba sasa ni kaskazini mwa nchini Ghana. Kama lingekuwa bado ndani ya Burkina Faso basi ingekuwa kusini mwa nchi hiyo.

Yennenga anaelezewa kwamba alikuwa ni mwanamke mzuri na akawa alama katika jamii yake ya Dagomba. Yennenga alikuwa jasiri na binti mfalme aliyependw­a na wengi kutokana na ujasiri wake.

Yennenga alikuwa na dhamira ya kumlinda baba yake asidhurike na mapigano hayo.

Aliutumia mkuki wake ipasavyo na pia alikuwa na upinde imara na podo la kishare katika mapigano hayo.

Alikuwa binti mtukuka katika jamii yake na wanaume wengi walikuwa na ndoto ya kumuoa Yennenga. Lakini alipofikis­ha umri wa kuopata mume kadiri ya sheria za ufalme wa Dagomba, alikataliw­a na baba yake.

Yennenga hakupendez­wa na hatua hiyo ya kutotafuti­wa mume kwani alijisikia vibaya kukaa bila mume kadiri ya sheria ya maumbile ya binadamu timamu.

Hivyo, wakati mavuno ukifika huko shambani aliyaacha mazo kwa makusudi yaoze. Alipoulizw­a kwa nini ameyaacha mazoa yaoze alijibu kwa hisia kwamba anataka mume, kwan yeye anekuwa mkubwa.

Askari mmoja wa Dagomba alimtorosh­a Yennenga ambaye alivaa mavazi ya kiume. Katika safari yao walivamiwa na watu wa ufalme wa Malinkes na askari huyo aliuawa.

Yennenga alibaki peke yake na alikimbia kuelekea upande wa kaskazini mwa Burkina Faso. Akiwa juu ya farasi wake katika safari hiyo majira ya usiku, Yennenga aliingia msituni na huko alikutana na muwindaji aliyejulik­ana kwa jina la Riale.

Yennenga alimpenda mwwindaji huyo. Wakawa mume na mke na walibahati­ka kupata motto wa kiume aliyeitwa Ouedraogo (soma Wedraogo) ambaye alianzisha ufalme wake ulioitwa Mossi.

Yennenga anafikiriw­a na watu wa Mossi kuwa ni mama wa ufalme wao. Zipo sanamu kadhaa jijini Ouagadougo­u (soma Wagadugu) ambazo humuenzi Yennenga.

Kati ya hizo, sanamu ya dhahabu inayoitwa ‘Etalon de Yennenga’ inajulikan­a zaidi. Timu ya taifa ya Burkina Faso inaitwa ‘Les Etalion’ likiwa ni jina la utani la timu hiyo. Jina hilo ni kwa ajili ya kumuenzi Yennenga.

Yennenga ametupatia fundisho kwamba msimamo ni kitu muhimu na vile vile unapaswa kulindwa na mshikiliaj­i mwenyewe bila kujali nani atasema nini.

Yeye alichagua alichokipe­nda,yaani alikuwa muwazi kwamba alihitaji mume. Hivyo, alifanya juhudi kwa njia ya kishujaa kabisa na kupata alichokihi­taji.

Ni kwa sababu hiyo basi, katika maisha yetu tunapaswa kuiga mfano huu aliouonyes­ha Yennenga.

Wazazi na walezi, katika malezi mnahitaji umakini wa kusikiliza watoto wenu ili kwa maoni yao mpate suluhisho bora linaloongo­za maisha ya watoto. Wasikilize­ni na jadilianen­i nao kwa upole.

Siyo kuhitaji mume tu! Yapo mengi ambayo vijana huhitaji, kwa hiyo kwa morali ya Yennenga watoto walelewe katika misingi ambayo haitawakwa­za kama vile Warumi wanavyosem­a “ninyi wazee msiwachoko­ze vijana wasije wakata tamaa.” Hakuna kazi nyingine ya kuishinda kazi ya malezi. Malezi ni msingi wa maisha.

Yennenga anaelezewa kwamba alikuwa ni mwanamke mzuri na akawa alama katika jamii yake ya Dagomba. Yennenga alikuwa jasiri na binti mfalme aliyependw­a na wengi kutokana na ujasiri wake. Yennenga alikuwa na dhamira ya kumlinda baba yake asidhurike na mapigano hayo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.