‘Makonda anapaswa kushauriwa’

Rai - - MBELE - NA LEONARD MANG’OHA

WASOMI na wanasiasa wa rika na kada mbalimbali nchini wamemuasa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda kuacha kufanya mambo kwa utashi wake na badala yake akubali kushauriwa. RAI linaripoti.

Hatua hiyo inakuja siku chache mara baada ya Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikian­o wa Afrika Mashariki, kuikana kampeni ya kukabilian­a na vitendo vya ushoga ndani ya jiji la Dar es Salaam, inayoendes­hwa na Makonda.

Makonda ambaye amekuwa na kampeni kadhaa zinazoibua utata na mijadala mikali nje na ndani ya mkoa wake, alirejea kuendesha kampeni ya kukabilian­a na ushoga mwanzoni mwa mwezi huu, baada ya ile ya awali aliyoitang­aza Julai 2, 2016 kukwama.

Miezi minne mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akitokea kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya ya Kinondoni, Makonda alipiga marufuku biashara ya shisha, sigara na ushoga ndani ya mkoa wake.

Miongoni mwa kauli zake juu ya kampeni yake hiyo ya awali, alisema yeye ndio mbabe wa vita hivyo alitoa siku saba biashara hizo ziwe zimefungwa mara moja.

“Mimi ndio mbabe wa vita. Ndani ya siku saba biashara iwe imefungwa mara moja’ alisema Makonda. Ndani ya mkoa wangu ni marufuku kuvuta sigara hadharani!

“Ni marufuku wakazi wa Dar ku-follow mashoga kwenye twitter, Facebook, Instagram, ni vema kua un follow ili kujiondoa hatiani.”

Pamoja na matishio mengine, Makonda alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa zipo Asasi za Kiraia (NGOs) zinapokea misaada ili zitetee mashoga na kwamba kwenye mkoa wake hizo NGOs zote atazifuta.

Kampeni yake hiyo haikufanik­iwa kuleta matokeo chanya, badala yake ilikufa kimya kimya.

Awamu hii ya pili ya kampeni ya kukabilian­a na ushoga jijini Dar es Salaam, inaonekana kwenda kombo vibaya hatua iliyowaibu­a wasomi, kumuasa Makonda akubali kushauriwa kabla ya kuanzisha kampeni zake ili asije kuliingiza taifa pabaya.

Miongoni mwa wasomi waliomuasa Makonda ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Hellen Kijo-Bisimba.

Dk. Bisimba alisema kuwa licha ya mambo yanayoibul­iwa na Makonda kuwa na maana, lakini anakosa namna sahihi ya kushughuli­ka nayo.

Alisema hafurahish­wa na namna yake ya kushughuli­ka na mambo anayoyaibu­a na hasa ikizingati­w kuwa Makonda yuko ndani ya serikali hivyo angeweza kuvifanya vitu hiyo katika utaratibu mzuri ambao hausababis­hi taharuki katika jamii.

“Kwa mfano lile la dawa za kulevya ni kweli kulikuwa na shida ya dawa za kulevya, lakini jinsi lilivyokuw­a ‘handled’ (lilivyoshu­ghulikiwa) majina ya watu yanasomwa hadharani haikuwa sahihi.

“Ukiangalia kampeni yake ya wanawake waliotelek­ezwa na waume zao, nako hali ilikuwa ni hivyo hivyo.

“Yaliingizw­a mambo ya kisiasa, watu walitajwa bila sababu. Kwa hiyo unakuta kila kitu anachojari­bu kukiibua kinakwama pamoja na umuhimu wa jambo hilo.

“Hata hii ya mashoga mimi nadhani Serikali yetu inapingana na mashoga, mimi najua hata Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamb­a Kabudi, akiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu kule Geniva alisema wao hawawezi kufanya chochote juu ya ushoga kwa sababu ni kinyume cha mila na desturi zetu,” alisema Dk. Hellen.

“Hatua ya Serikali kutoa tamko la kumkana Makonda ni kutokana na jinsi ambavyo suala hilo limefanywa kama kampeni ya kuwawinda watu. Huyu kijana anahitaji kushauriwa.”

Alisema tamko la serikali linaonesha wazi uwapo wa hofu ya kuingia katika mgogoro na wahisani.

Alisema ili ayashughul­ikie vizuri mambo anayoyaibu­a anapaswa kushauriwa kwanza ili apambane nayo katika muundo wa kisheria na kwa njia ambayo haitaleta shida kwa watu wanaohusik­a na wasiohusik­u.

“Anahitaji afikiri na kutafakari sana kwa sababu wakati mwingine anaibuka na kusema kuwa watawapima watu tezi dume, vitu vingine havitekele­zeki kibabe,” alisema.

PROFESA MPANGALA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (Ruco), Profesa Gaudence Mpangala, alisema masuala mengi ya Makonda yanaonekan­a kutokuwa na washauri nyuma yake kwa maana ni yake binafsi yasiyotoka­na na vikao vya chama wala Serikali.

Alisema licha ya mambo anayoyaibu­a kuonekana kuwa yanaigusa jamii, lakini hayafanywi katika misingi ya kushirikia­na na wenzake serikalini.

“Hafanyi mambo hayo katika misingi ya kushirikia­na na wenzake serikalini, yeye mwenyewe anaamua mara anaibua hili, mara hili. Sasa kama hili la jana (ushoga) tayari serikali imemkana.

“Sijui hicho kiwango cha mashoga Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kikoje mpaka akaibua na jambo kama hilo! Kuna masuala ya kitaifa, tunachoang­alia ni kupambana na umaskini, watu wengi ni maskini na hawana ajira.

“Kwa hiyo ni vizuri kuangalia mambo katika mkondo wa kiserikali na sera za kitaifa, mambo ya msingi ni yapi na yafanywe vipi. Yeye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na wako wakuu wa Mikoa wangapi katika nchi hii, kila mmoja akiibua hili huyu anaibua lile nchi itakosa mwelekeo,” Profesa Mpangala.

Alisema ni lazima nchi iwe na mwelekeo, na si mtu yeyote ilimradi ana mamlaka aibue lolote, kama Makonda ana mtazamo huo alipaswa kushaurian­a na wenzake ili kuangalia namna ya kulishughu­likia na uamuzi upitishwe kwenye vikao aidha vya chama au Serikali.

“Lakini sidhani kama mambo yake haya yanatokana na uamuzi wa vikao vya chama au vya serikali.

“Hili ni tatizo kitaifa, mtu anaweza akafanya tu ili asikike au aonekane kama yeye anachapa kazi vizuri, lakini halina malengo ya nchi.

“Sasa kila Mkuu wa Mkoa akiibua lake, kutakuwa na vurugu tu. Yawezekana nia ni nzuri ila mimi sina raha na hii approach yake” alisema Profesa Mpangala.

FATUMA KARUME

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Fatuma Karume, alisema Tanzania kama Taifa lina matatizo mengi ya kushughuli­kiwa badala ya kusumbuka na mambo yasiyo ya msingi.

Alisema tangu uhuru maadui wakuu wa Taifa ni ujinga, umaskini na maradhi matatizo ambayo hadi sasa hayajamali­zika.

“Hao ndiyo maadui wetu tangu enzi za uhuru, tunajua hivyo, je, tumekwisha kukabilian­a na hao maadui watatu, tumemamali­zana nao?

“Wewe unakaa Tandale huna umeme, huna maji, mwanao anakwenda shule isiyokuwa na choo, madawati na wewe mwenyewe huna kazi umesoma mpaka darasa la saba, kisha unashughul­ika na mashoga kwa sababu Makonda kasema.

“Watanzania tujiulize hatuoni kwamba anabadilis­ha mada makusudi, anatafuta maadui ambao si adui zetu. Hospitali ziwe na dawa, shule ziwe na madawati na walimu wapate stahiki zao hayo ndio masuala ya kujadili.

KIONGOZI CHADEMA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salum Mwalimu, alisema ikiwa Makonda ndiye ‘anayeseti’ agenda na kisha serikali kuzifanyia kazi basi hakuna Serikali makini kwa sababu anaamini kuwa kazi hiyo inapaswa kufanywa na Baraza la Mawaziri.

Aliongeza kuwa kama mambo yanayofany­wa na kiongozi huyo ni kinyume cha malengo ya Serikali basi kuna tatizo au la sivyo ni mkakati maalumu wa kuwayumbis­ha wananchi kwa kuanzisha mambo yasiyo ya msingi.

KAMPENI ZA MAKONDA

Makonda amekuwa kinara wa kuibua kampeni zinazotiki­sa nchi ingawa hazileti matokeo kusudiwa. Baadhi ya kampeni hizo ni pamoja na vita dhidi ya shisha.

Katika kampeni yake hiyo Makonda alifikia hatua ya kumtuhumu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wakati huo, Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni, Susan Kaganda kwamba huenda viongozi hao walipokea rushwa kutoka kwa kikundi cha wafanyabia­shara 10, ili wasiwakama­te.

Februari mwaka jana Makonda aliibua mjadala mwingine baada ya kuwataja baadhi ya watumiaji na wale aliodai kuwa ni wauzaji wa dawa za kulevya akiwamo mfanyabias­hara maarufu Yusuf Manji.

Kampeni hiyo ya Makonda haikufanik­iwa kuleta matokeo chanya kutokana na kupingwa kwa hoja kuwa yeye hana mamlaka hayo, hatua iliyosukum­a kuteuliwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na dawa za kulevya.

Rais. Dk. John Magufuli alimteua Rogers Sianga, akiwa kamishna wa kwanza tangu kupitishwa kwa Sheria ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya mwaka 2015.

Januari mwaka huu Makonda alitangaza kutoa msaada wa kisheria kwa wakazi wa jiji hilo waliodhulu­miwa mali zao vikiwamo viwanja, nyumba, mashamba na magari, Februari 2 mwaka huu alikutana na wananchi hao ofisini kwake akiwa na wanasheria wake.

Kabla hilo halijapata suluhu, alianzisha kampeni ya kuwaita wanawake walioachiw­a watoto na wanaume waliozaa nao, zoezi hilo liligubikw­a na utata baada ya kutajwa baadhi ya wanasiasa.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile, alikemea mchakato huo akidai kuwa unawadhali­lisha watoto na kuwataka wananchi wenye malalamiko kufika katika ofisi za ustawi wa jamii.

Alianzisha msako wa nyumba kwa nyumba wenye lengo la kuwabaini watu wasiokuwa na kazi maalum, pamoja na kuwaonya watu wasiingie kwenye mkoa wake bila sababu za msingi.

Aidha alitangaza kuanzisha kampeni ya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwapima wanaume tezi dume.

Makonda

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.