Biashara ya mafuta na bepari mkomavu

Rai - - MAKALA - NA DAVIDI MANGARA

Ni saa nne asubuhi, kijua cha kuvizia kikiwa kinaling’arisha anga la Marekani.

Watu makumi kwa mamia kila mmoja na pilika zake, hawa wanakwenda kaskazini, wengine kusini, mashariki na hata magharibi alimradi wanasaka tonge.

Wakati kundi kubwa la watu likihangaika huku na kule kujitafutia chochote, muda huo kikao kizito kilikuwa kikifanyika muda huo katika jengo la Trump Tower.

Ni moja ya majengo makubwa na marefu kwenye jiji la Newyork, jengo hilo ni mali ya mfanyabiashara bilionea ambaye pia ndiye rais wa taifa hilo Donald Trump.

Wafanyabiashara wakubwa walikuwepo ndani ya jengo hilo, meza kubwa iliyotawala kwenye ukumbu ilipambwa na chupa ndogo za maji.

Harufu za manukato yaliyopoa ndio ilitawala ukumbini humo. Nje ya ukumbi kuliwa na ulinzi imara wenye lengo la kuhakikisha kila aliyekwenye jengo hilo anatoka salama.

Waliokuwamo ukumbini humo ni wafanyabiashara wa mafuta, baadhi yao wakiwa ni wamiliki wa visima vya mafuta kutoka katika nchi kadhaa kutoka falme za kiarabu, urusi, India na hata Afrika.

Lengo la kikao hicho ni kujadili mikakati na mipango yao ya kibiashara.

Kampuni ya Mcklein Washington, ikiwa chini ya kijana William Washngton ndio kinara wa bioashara ya mafuta duniani.

Ukubwa wake huo umeifanya kuwa mratibu mkuu wa mikutano yote ya wadau wakubwa wa mafuta duniani.

Kwenye mkutano huo yupo kijana kutoka pembe ya Afrika Mashariki, Thomas Materu.

Matheru ni Mtanzania na makazi yake ni Tanzania, pamoja na utajiri wake, lakini hakupewa nafasi kubwa kwenye mkutano huo, ingawa alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.

Kipaumbele zaidi kilionekena kuelekzwa kwa mataikuni wa mafuta kutoka nchi tajiri. Materu, alikuwa mjumbe mweusi pekee kwenye mkutano huo, hakutazamwa sana,hata waandaji hawakumpa nafasi kabisa jambo lililomghadhibisha.

Alitamani kuongea, lakini hakupata nafasi hiyo, hatimaye alinyanyuka na kufungua kinywa chake kilichotoa sauti nene na nyoofu, iliyozungumza vyema lugha ya Kiingereza.

‘‘You don’t give me a chance to speak because I’m black ?why you lose my time to invite me here…?”

Wote waliokuwamo ukumbini walipigwa na butwaa, hakuna aliyeamini, wakati huo mmoja wa watu waliokuwa meza kuu ndio alikuwa anazungumza.

Haraka Washngton akainuka na kumtuliza Materu… ‘‘samahani sana bwana Thom, si nia yetu kukuzuia kuongea, unazo haki zote humu, tuliona tuwape nafasi kwanza washiriki wenye uzoefu na mikutano ya namna hii ili ninyi wageni muelewe vema ili hata mtakapochangia mjue mnachangia nini na kwenye eneo gani.” Alihitimisha Washngton.

Kauli ya mratibu wa mkutano huo angalau ilisaidia kupoza joto la Materu, hakusita kuomba radhi kwa alichokifanya punde.

Mkutano wao ulikuwa wa siku mbili, lakini ulibeba mambo mazito yaliyokuwa na mwelekeo wa kujinufaisha zaidi wao wenyewe.

Siku ya pili na ya mwisho ya mkutano huo ilikuwa ngumu kidogo kwa kijana huyo wa Kitanzania, kwani baadhi ya washiriki walionesha ubaguzi wa wazi wazi dhidi yake.

Alijitahidi kujichanganya bila mafanikio, wengi walimbagua, wachache waliompa ushirikiano hafifu.Kwakuwa alijua ni nini kilichompeleka pale, hakujali, muhimu kwake ilikuwa ni kuyasikia na kuyaelewa yaliyojadiliwa, kumpa ama kutompa ushirikiano kwake halikuwa jambo la muhimu tena.

Mara baada ya mkutano kwisha, haraka alirejea hotelini tayari kwa maandalizi ya safari ya kurejea Tanzania.

Alijilaumu kidogo kwa sababu hakuipata thamani anayoipata Afrika, hata hivyo alifurahia hatua ya kutambuliwa na Washngton pamoja na kujumuika na matajiri wakubwa wa mafuta duniani.

Katika kuonesha kuwa anaitumia nafasi hiyo vema kibiashara, alipanga kufanya jambo zito kabla hajaondoka Marekani.

Lengo la kupanga kufanya hivyo ni kutaka wamtambue yeye ni nani na wauone umuhimu wake na ikiwezekana wasiache kumwalika tena na tena.

‘‘kama wameweza kuniita mara ya kwanza,basi ya pili Watanifuata kabisa nchini kwangu,”

Alijiongelea, kisha akatabasamu, alipiga hatua tatu hadi kilipo kitasa cha mlango wa chumba chake, akapitisha kadi maalum ya kufungulia mlango.

Alipoingia cha kwanza alichokifanya ni kutua mkoba wake wa ngozi uliobeba makabrasha juu ya kitanda, kisha akakifuata kioo na kujitazama mara kadhaa.

0675335367

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.