Kauli ya JK na miaka mitatu ya JPM

Rai - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

HivikaribuniRaismstaafu Jakaya Kikwete (JK) alitoa tathmini yake kuhusu miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli na kufafanua changamoto mbalimbali alizokutana nazo wakati wa uongozi wake.

JK aliyasema haya siku chache kabla ya kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Magufuli, alipohojiwa na moja ya televisheni za mtandaoni.

Kutokana na uzito wa uchambuzi huo wa Rais mstaafu Kikwete RAI tumeiona haja ya kuchapisha mazungumzo hayo ili jamii iweze kupata kwa kina hasa kile kilichozungumzwa. Endelea… KAZI YA URAIS Kazi ya urais ni kazi ya namna gani: ni jukumu la uongozi tu wa taifa ambalo kuna mtu amekabidhiwa kuongoza taifa kwa niaba ya watu wote, kwanza ni kazi yenye dhamana kubwa, kazi yenye heshima kubwa lakini kazi ngumu.

Ni kazi ngumu kwa maana kwamba unajua kuna kazi ambazo kuna shughuli ambazo unachoweza ukasema ni kwamba kuna mtu mwingine unaweza kumwachia lakini hii haina mtu unayeweza kumwachia, wewe ndiye wa mwisho,

Adam hapa akipata kazi anaweza akawa na matumaini kwamba kuna mtu mwingine wa kumwachia lakini kazi ya urais huna mtu mwingine wa kumwachia yani wewe ndiyo wa mwisho kwa hiyo kila kitu kinakuja kwako ni namna gani umejipanga sasa kwa sababu kwanza mambo yote yanakuhusu.

Yakiwa ya hospitali yanakuhusu, ya jeshi yanakuhusu, ya barabara yanakuhusu, ya umeme yanakuhusu ya maji yanakuhusu ya maradhi yanakuhusulakini wewe ni mtu ambaye huna ujuzi wa yote lakini hayo yote uamue wewe, lazima hayo yote uyafanye wewe. Sasa inategemea sasa ni kiasi gani wewe mwenyewe umetengeneza mfumo wa ushauri wa kukusaidia kuyatambua.

Changamoto za Serikali awamu ya nne

Sisi tulipoingia tumeingia tatizo letu la kwanza likiwa ni ukame, ukame mkubwa, watu chakula hawana, ukame mkubwa umeme hakuna, mara ya kwanza ndiyo unaingia sasa hata wakati ule tunazunguka kwenye kampeni kila mnakopita ni jua kali kwelikweli.

Tunaingia sisi sasa nchi haina chakula kwa hiyo kukawa na watu, sisi tumeshughulikia chakula cha watu 3,776,000, vinginevyo unawaacha watu wangekuwa wanakufa njaa, na kwa bahati wakati ule tukawa na SGR baadae ndiyo ikabadilishwa ikawa National Food Reserve Agency, lakini wakati ule Strategic Game Reserve ilikuwa na tani 200,000 na bahati nzuri mzee Mkapa alikuwa ameacha fedha za kigeni zilikuwapo na hali ilikuwa nafuu tukaagiza na chakula kingine kutoka nje katika kipindi kile tukaweza kuvuka salama.

Kukawa na tatizo kubwa la mgao wa umeme, ukawa ni mgogoro kweli kweli, tukaingia kwenye mgogoro wa umeme ikawa sasa mnaupataje ndiyo kukawa na ushauri wa mashine za kukodi zingine zikatuletea migogoro ya Richmond, lakini umeme hakuna, mnafanyaje mnaiacha nchi kwenye giza?

Sasa katika jitihada hizo ndiyo na makosa yanafanyika humo ndani tukaingia kwenye mgogoro mkubwa tumekaa na mawaziri bahati nzuri Mwenyezi Mungu akaleta Elinino, ikatokea Elinino nakumbuka nilikuwa kwenye mapumziko wakati ule Desemba, nilikuwa Serengeti, Waziri Mkuu ananipigia simu anasema huku mabwawa yanajaa kuliko unavyoyatamani, tukaja tukapata nafuu tena.

Kwa hiyo kama ni changamoto ya kwanza hiyo ni kubwa kwelikweli kwamba unapokea urais na unapokea na njaa, na unapokea urais umeme hakuna kwa hiyo, hiyo ilikuwa hivyo. Ukitaka kuangalia kwenye umeme tu lakini ukija kuangalia kwenye hili kuna changamoto hii, hii na hii lakini kubwa zaidi tulipoanza tulianza na hiyo problem kubwa ya njaa na umeme ya aina yake.

Kwa hiyo ndio maana pale baada ya uzoefu ule nikasema bwana kumbe hii akiba ya Taifa ya tani 200,000 haitoshi tukasema lazima sisi tuiongeze hadi ifikie akiba ya Taifa ya tani 400,000 hadi mimi naondoka tukawa tumeshajenga uwezo wa kiasi hicho kwa sababu tulisema tusipokuwa na akiba mtapata tabu sana ingekuwa wakati ule wa mzee Mkapa hakukuwapo kwenye maghala yale na tani 200,000, mfikie mahali sasa muagize maana nchi nzima ni ukame, tulikuwa na ukame ambao Waingereza wanasema Unprecedented, mazao hayapo unatembea kule Shinyanga unakuta watu wameweza viuele kidogo juu ya matenbe yale, wakati ule tulikuwa kwenye reli ka maana ya Afrika Mashariki kwamba tutoke kwenye reli hii ya Mjerumani twende sasa kwenye reli ya kisasa tukaendelea na mipango wakati ule Waziri Sitta akaja na mpango ambao tulikuwa twende tukaweke jiwe la msingi lakinisikuuona kama umekamilika sawa sawa wakasema ni vizuri ukamilike kabla ya uchaguzi nikasema lakini tukianza na kitu ambacho hakikukaa sawa sawa tutakuja kuwapa matatizo wenzetu wanaokuja nilasema hili tuliache.

Nafurahi sasa mradi wa standard gauge umeanza ujenzi na walichofanya awamu hii kwenye mradi huu zaidi ya kile tulichokifikiria sisi ni kuweka umeme, na sisitulifikiria kujenga reli ya standard gauge lakini bila umeme, lakini ambacho awamu hii imekifanya ni kujenga standard gauge na kuweka umeme ambao unafanya sasa treni iwe na spidi kubwa zaidi kwa sababu sisi tulikuwa tunafikiria treni zile za dizeli tu.

Wenzetu wameenda hatua moja zaidi mbele ambayo itaongeza kasi ya usafiri na itafupisha sana. Kwa hiyo hili ni jambo jingine ambalo tumelianzisha wameliendeleza lakini wameliendeleza katika njia bora zaidi kuliko ambavyo tulifikiria sisi. Sisi tulilianza kwa maana ya kulifikiria tu lakini halikuwapo kwenye mpango uliothabiti, wizara iliniletea lakini sikuafiki. Awamu ya tano iko poa Awamu ya tano iko poa kabisa kwamba ahadi na nadhiri ya CCM kwa Watanzania Serikali inayatekeleza maana haya ndiyo tuliyokuwa tunasema tunaacha mzigo ambao tunawaachia wenzetu, tunasema sasa ni kukuza sekta za uzalishaji mali, kilimoufugaji, uvuvi viwanda vikubwa na vidogo zote hizo zinaongeza fursa za ajira lakini kubwa kwenye viwanda ambayo kwangu mimi Serikali hiiinatekeleza maelekezo, ahadi ya Watanzania na nadhiri ya CCM kwa watanzania awamu hii.

Jambo la tatu ilikuwa ni vita dhidi ya rushwa na CCM inasema kwenye ilani hii jitihada hizi za kuinua uchumi kukuza ajira na vitu gani na maendeleo hizi zitakwamishwa kama hatutafanikiwa katika kupambana na rushwa ndiyo maana inali inasema Serikali inayokuja hiyo tunaiagiza kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote ambao watakaobainika kuendeleza rushwa serikalini na katika sekta binafsi.

Hii ni kuimarisha vyombo na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa ikiwa ni pamoja na kuanzishwa Mahakama maalumu ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na ndiyo maagizo sasa specific ya chama sasa ninapoangalia utekelezaji sina shaka kwamba jambo hili linatekelezwa.

Kwamba ile ahadi na nadhiri ambayo CCM imeiweka kwa Watanzania kuhusu kupambana na rushwa Serikali ya awamu ya tano inaitekeleza kwa vitendo, mkakati wa Mahakama maalumu nadhani uko kwenye hatua nzuri.

Yanayofanyika kupambana na wale wote wanaoendeleza rushwa sisi sote ni mashahidi ni kiasi gani yanaendelea ni tatizo kubwa hatutegemei kuwa litakuwa limeisha kabisha lakini ni lazima tuonekane tunapambana.

Serikali hii imejipambanua kwamba inapambana na tatizo hili, kwa hiyo kwangu mimi nadhani wana…, mengine ambayo CCM imesema, pamoja na kupambana na rushwa Serikali inatakiwa kushughulika kwa ukali zaidi na tatizo la ubadhirifu na wizi wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka ambalo nalo tuna ushahidi Serikali inaendelea kutekeleza jambo hili.

Kwa maana Serikali ukitaka kufanya tathmini mambo ni mengi ambayo ambayo yametekelezwa humu kwa sababu hata madaraja la Kigamboni limekamilishwa na awamu hii, la Kilombero limekamilika na la Kilombero ndiyo katika mawe ya msingi niliyoweka ya mwisho tena tuliweka jioni lile, tuliweka Jumamosi usiku lile maana tulitua kule kwa helkopita kule Mbuga Mahenge alafu tuka-drive nalo limekamilika.

Ndiyo maana tunasema mambo

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kulia akiwa amemkumbatia Rais John Magufuli

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.