MFALME WA ETHIOPIA, ALIYEUAWA KISHA KUZIKWA CHOONI

Rai - - MBELE - NA MBWANA ALLYAMTU

Haile Selassie I alizaliwa Julai 23, 1892 na kufariki akiwa kizuizini, tarehe 27, Agosti 1975, huko Addis Ababa, mji mkuu wa

kutupwa kwenye choo cha chumbani kwakekweny­e Kasiri la Kifalme.

Haile Selassie alikuwa ni Kaisari au Mfalme wa 225 wa Ethiopia, au Negus Negeste au Mfalme wa mwisho kwa lugha ya Kihamarac. Mke wake

Haile Selassie I, alizaliwa katika kijiji cha Ejersa, Mkoa wa Harar. Jina lake la utotoni ni Ras Tafari Makonnen, na ndilo jina lake la shule. Baadaye, alitawazwa kuwa Mfalme Haile Selassie I. Jina hili maana yake ni “Utukufu wa Utatu (Mtakatifu)” kaatika lugha ya

wake, alifahamik­a kama Simba wa Yuda, Mfalme wa Wafalme (His Imperial Majesty, au H.IM).

Alizaliwa katika familia ya kifalme na baba yake, Ras Makonnen, alikuwa kabaila na mtawala wa (gavana) wa jimbo la Harar. Katika familia yao, walizaliwa watoto 11. Alikuwa ni muumini mzuri sana wa dini ya Kikristo, dhehebu la Orthodox la Ethiopia— ambalo limeenea sana nchini Ethiopia kwa zaidi ya miaka 1500.

Ras Tafari Makonnen akiwa na umri wa miaka 15 tu, alipewa cheo cha ugavana wa Mkoa wa Sidamo, mwaka 1907. Hii ilitokana na yeye kuonekana kuwa na akili sana, mweledi wa mambo licha ya kuwa mtoto mdogo. Na mwaka 1911, baba yake alifariki akarithi cheo cha Gavana wa Harar.

Mwanzoni mwa miaka ya 1913 mpaka 1916, Ethiopia ilitawaliw­a na mtawala kutoka jamii ya Kislamu aliyeitwa Lij Iyasu, na wakati huu kuliibuka ugomvi kuhusu Negus huyo Mwislamu. Ugomvi huo ulitokana na jamii ya makabaila kutanua maslahi yao ya umiliki wa aridhi.

Katika ugomnvi huo, Haile Selassie akiwa Gavana wa mikoa muhimu yenye ushawishi katika utawala wa Mfarme Lij lyasu, alisimama upande wa Mfalme, lakini ugomvi ulipotanuk­a na kuwa mkubwa, Ras Tafari (Haile Selassie) aliachukua upande wa kati (neutral). Hata hivyo alifaidika zaidi na uasi huo, na kulifaniki­wa kumpindua Mfalme Negus Iyasu. Makabaila hao waliomwond­oa Iyasu mwaka 1916, walimteua shangazi yake, binti wa Negus Negesti Menelik II aliyeitwa Zauditu kuwa Malkia, kwa kuwa Zauditu alikuwa binti mdogo sana wakaamua kuwa Ras Tafari (Haile Selassie) awe mwangalizi wake.

Kwa njia hii, Ras Tafari au Haile Selassiem kama anavyofaha­mika, akawa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa na wa muhimu zaidi nchini Ethiopia. Hii ni kutokana na yeye kuwa mwenye maamuzi mengi. Kimsingi nafasi hii ilimpa uzoefu sana kisiasa. Mwaka 1928, Malikia Zauditu, akampa cheo cha Naibu Negus, yaani kuwa mtawala wa chini yake. Baada ya kifo cha Zauditu mwaka 1930, Ras Tafari au Haile Selassie aka akapokea taji na cheo cha Negus Negeste (au Mfalme wa Wafalme) wa Ethiopia na kubadilish­a jina kuwa Haile Selassie I. Alijiita hivyo akijinasib­isha na ufarme wa ukoo wa Mfalme Daudi wa Wayahudi, na inaaminika kwamba alikuwa wa uzao wa Malikia Sheba na moja ya vitukuu wa Mfalme Suleiman. Baada ya kupokea taji la ufalme, akafanya ziara ya Ulaya kutafuta ushawishi wa nchi yake kimataifa.

Mwanzoni mwa miaka ya 1947, habari zake zikaenea kote duniani kuwa mwana wa Daudi na mtawala wa Ethiopia, kiongozi mwenye maono na hekima, shupavu na mkombozi wa Waafrika kupitia sauti ya Mungu. Wasifu huu ulisababis­ha kutokea kwa dini mpya ya Rastafari iliyopokea jina kutoka kwake (Ras Tafari), ingawa mwenyewe hukuwahi kuwa muumini wa dini hii na alibaki kuwa muumini wa Kanisa la Orthodox, akiwa na Daraja ya Shemasi. Lakini watu weusi wa Jamaika, waliokuwa wajukuu wa watumwa wa asili ya Afrika, walisikia kwa mara ya kwanza ya kwamba Mwafrika anaheshimi­wa na wafalme wa Ulaya, wakaona yeye ni Mungu aliyerudi duniani kwa ajili ya watu weusi, na hii ilitokana na safu ya uzao wake kutoka kwa Malikia wa Sheba alayewahi kutawala Ethiopia miaka mingi nyuma, huku ikitajwa kuwa alikuwa mke wa Mfalme Suleiman wa Jerusalem na kupitia moja ya uzao wake Ras Tafari ni vitukuu vya uzao huo. Itaendelea wiki ijayo.

+2556795555­26.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.