UPINZANI HAUWEZI KUFA KWA SABABU YA SHERIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA

Rai - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

MOJAWAPO ya majukumu ya Bunge ni kutunga sheria na kusimamia utendaji wa serikali kuhusu masuala mbalimbali yanayoigusa jamii.

Hata hivyo, katika siku za karibuni kumeibuka sintofahamu kuhusu hatua zilizoanza kuchukuliwa na Mkuu wa Dar es Salaam, Mkoa Paul Makonda katika kudhibiti vitendo vya ushoga jijini Dar es Salam.

Licha ya nia njema ya mkuu huyo wa mkoa katika kudhihirisha kuwa jamii ya Watanzania na wanadar es salaama haiungi mkono vitendo hivyo, tafsiri yake imeleta picha pana hasa ikizingatiwa jamii ya kimataifa hulichukulia suala hilo kama ukiukaji wa haki za binadamu. Licha ya serikali kusahihisha kuwa tamko au hatua zinazochukuliwa na Makonda hazigusi Tanzania, bado kumekuwapo na utata kuhusu suala hilo jambo ambalo tumeona nchi kadhaa zikiionya Tanzania.

Kutokana na hali hiyo, Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo (CEGODETA), imeona kuwa sasa nio wakati muafaka kwa Bunge la kutoa tamko kuhusu msimamo wa nchi kuhusu suala la ushoga.

Mkurugenzi Mtendaji wa CEGODETA, Thomas Ngawaiya akizungumza na RAI wiki hii anasema anashangaa kuona hadi sasa Bunge ambalo ni chombo kinachosimamia serikali kukaa kimya pasipo kutoa msimamo.

Ngawaiya ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM) anasema umefika wakati sasa kwa wabunge kujadili suala hilo na kuweka wazi msimamo wa Tanzania kuhusu jambo hilo kikatiba, kisheria, Mila na Desturi za Tanzania. Ngawaiya anasema iwapo nchi itaruhusu jambo hilo kutokana na shinikizo kutoka kwa baadhi ya taasisi zisizokuwa za serikali zinazofaidika na misaada kutoka kwa makundi hayo ya mashoga, katika siku za usoni jambo hilo litakapoota mizizi litakuwa gumu kukomeshwa.

“Kwa sasa Watanzania wapo ‘dilema’ hawajui washike msimamo upi kuhusu ushoga kutokana na tamko lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Agustine Mahiga, aliyekosoa tamko la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, kupinga ushoga ambako alisema kauli ile ilikuwa yake na sio msimamo wa Tanzania.

“Jambo hilo linatuchanganya ukizingatia wanaolumbana ni viongozi waandamizi wa serikali, hivyo linahitaji ufafanuzi wa kina ili tujue kama kuna mkataba wowote umesainiwa hivi karibuni kutambua haki za mashoga nchini. Rais Jakaya Kikwete aliona bora kukosa misaada kuliko kukubali kutia saini ya kuruhusu ushoga kwa matakwa ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon.”

Mwenyekiti huyo anasema kuwa pamoja na kupigiwa kelele na nchi za Magharibi lakini Kikwete akiwa rais aligoma kusaini takwa hilo kwa sababu alitambua vitendo vya ushoga na ukahaba ni kinyume cha sheria, Mila, Desturi na tamaduni za nchi.

“Vitendo vya ushoga na ukahaba vikiruhusiwa kuendelea bila kudhibitiwa vitaathiri watoto na wajukuu zetu ambao ni Taifa la kesho na ikumbukwe hata dini zetu zinakataza ushoga na ukahaba, hivyo haki za binadamu isiwe kisingizio cha kuruhusu ushoga na ukahaba.” alisema.

Akizungumzia kuhusu kukinzana kwa viongozi katika jambo hilo aliwataka waache kutoa kauli kinzani kuhusu jambo hilo kutokana na kuhofia nchi wafadhili na kukubali kuwa watumwa wao na kusahau wajibu wao wa kulinda na kutetea mila na tamaduni ambazo ni misingi ya ujenzi wa taifa.

Pia wanatoa wito kwa wafadhili kuacha kuingilia sheria za Tanzania ikiwemo na kuingilia mila na tamaduni za taifa kwa kuitaka nchi kuwaruhusu mashoga kufanya kazi zao alizoziita chafu kwa uhuru bila ya kufuata sheria inayokataza.

Thomas Ngawaiya

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.