KIMATAIFA: TELEVISHENI KUTUMIA UBONGO WA MWANADAMU

Rai - - MBELE - NA HILAL K. SUED

KAMPENI dhidi ya ufisadi inayofanywa na Rais wa sasa wa Angola,

inaendelea kushangaza na kufurahisha, ndani ya nchi hiyo na nje pia – ikiwa umetimia mwaka mmoja kamili tangu ashike madaraka.

Kinyume cha matarajio ya wengi wakati alipochaguliwa, rais huyo (maarufu J-Lo nchini mwake) ameanzisha uchunguzi dhidi ya vigogo wa serikali na wafanyabiashara ambao walikuwa wanafanya watakavyo kwa miongo mingi chini ya utawala wa Rais Jose Edouardo dos Santos.

Walengwa wakubwa wa vita hii ya Lourenço ni wanafamilia na maswahiba wengine wa karibu zaidi wa zamani. Katika kipindi cha miaka 39 cha utawala wake Dos Santos alikuwa analea ufisadi ambao ulikuja kuzagaa sana na aliwasimika wanafamilia na maswahiba wake katika nyadhifa kubwa kubwa zenye ushawishi. Watu wengi walitarajia familia ya Dos Santos ingebakia kuwa na nguvu pamoja na kuachia kwake madaraka kwa Lourenco. Walikosea.

Mwishoni mwa mwezi September mwaka huu, Jose Filomeno dos Santos, mtoto wa kiume wa rais wa zamani na mkuu wa mfuko wa hazina ya taifa (sovereign wealth fund), alitiwa mbaroni pamoja na swahiba wake wa kibiashara Jean Claude Bastos de Morais.

Wawili hawa wnakabiliwa na tuhuma za utakatishaji fedha, matumizi mabaya ya fedha na madaraka na udanganyifu. Jose Filomeno pia anakabiliwa na mashitaka ya ziada kuhusiana na kilichoitwa “mpango wa utajiri wa harakaharaka Dola za Kimarekani 500 milioni uliobuniwa katika wiki za mwisho mwisho za utawala wa baba yake.

Naye Isabel dos Santos, binti mkubwa wa rais wa zamani pia yuko chini ya uchunguzi mkali wa tuhuma za mihamala ya utata iliyofanyika wakati akiwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya taifa ya mafuta – Sonangol.

Isabel anahesabiwa kama ni miongoni mwa wanawake tajiri zaidi Barani Afrika na aliondolewa kwenye wadhifa wake Novemba 2017 – wiki chache tu baada ya Lourenco kuapishwa. Lakini si familia ya Dos Santos tu ndiyo inayofuatiliwa.

Septemba mwaka huu aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo Valter Filipe kuanzia 2016-17 alifunguliwa mashitaka ya uzembe na utakatishaji fedha kuhusiana na suala la Jose Filomeno. Na mwezi huo huo, Ismael Diego, aliyekuwa mkuu wa mfuko maalum wa rais alitiwa mbaroni kwa kuhusiana na upotevu wa Dola za Kimarfekani 20 milioni. Katika tuhuma hizo, Augusto Tomas, waziri mmoja wa zamani naye alikamatwa.

Aidhanjeyamipaka,mamlaka za Angola zimefanikiwa kupata amri za kukamatwa mali zake zilizotoroshewa nchini Uingereza, Uswisi, Mauritius dhidi ya Quantum Global taasisi ya Uswisi inayosimamia mfuko wa fedha za Angola zinazokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani 3 bilioni. Serikali ya sasa ya Angola inaituhumu taasisi hiyo kwa usimamizi mbaya na kuizidishia maradufu ada za huduma zake.

Mwenyekiti wa mfuko huo Jean Claude Bastos de Morais, anashikiliwa na mamlaka za serikali ya Angola.

Ufisadi nchini Angola uliota mizizi mirefu, ambayo ilienea hadi kona zote za uchumi wa nchi uliokuwa unathibitiwa kwa karibu sana na utawala. Matatizo yaliongezeka baada ya kumalizika kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002 pale ongezeko wa mafuta yasiyosafishwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa zilisukuma kuwepo kwa miradi mikubwa ya kuijenga upya nchi.

Ni kweli ujenzi umekwenda kwa kiwango cha kuridhisha, lakini fedha nyingi zilitapanywa au kuibiwa. Inakadiriwa zaidi ya Dola za Kimarekani 28 bilioni kutoka bajeti ya serikali hazijulikani zilipo.

Kama vile ilivyo kwa nchi nyigine nyingi Barani Afrika, nyingi ya fedha hizi zimevuka mipaka na kwenda nje. Vigogo wanasadikiwa kuhamisha fedha hizo kwenda nje ili kufuta nyayo na pia kuzihifadhi iwapo upepo wa kisiasa ungebadilika nyumbani – kama ilivyotokea.

Chini ya utawala wa zamani wa Rais Dos Santos, ari ya kupambana na ufisadi ilikuwa ndogo sana. Kashfa kubwa kubwa za ufisadi zilipoiubuka mara moja zilikuwa zinasukumwa chini ya mazulia.

Mfano mmoja ni kuanguka kwa BESA Bank – iliyokuwa benki ya pili kwa ukubwa nchini humo mwaka 2014 kutokana na mikopo isiyolipika ya thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani 5.7 bilioni, au asilimia 80 ya fedha zilizokuwa mikopo za benki hiyo.

Mamlaka za nchi hiyo walijitahidi sana kuifunika kashfa hiyo hata ilipobainika sehemu kubwa ya mikopo hiyo ilitolewa kwa wanafamilia na mswahiba wa Dos santos.

Katika vitabu vyao hivyo wanadokeza kuwa uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan hauhusiani kwa vyovyote na ugaidi, wala na Osama bin Laden, wala na Taliban wala na kuangushwa kwa majengo ya World Trade Center (WTC). Waandishi hao wanadokeza kuwa tamaa ya mafuta na gesi

Isabel santos

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.