Tuisahau Taifa Stars, tugeukie Serengeti Boys

Rai - - MBELE - NA AYOUB HINJO

INAWEZEKANA Novemba 18 ilikuwa siku mbaya zaidi kwa Watanzania kuliko nyingine yoyote katika kipindi cha hivi karibuni. Ndio, kila Mtanzania alikuwa na matumaini makubwa kuiona timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inafanya vizuri na hatimaye ...

INAWEZEKANA Novemba 18 ilikuwa siku mbaya zaidi kwa Watanzania kuliko nyingine yoyote katika kipindi cha hivi karibuni.

Ndio, kila Mtanzania alikuwa na matumaini makubwa kuiona timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inafanya vizuri na hatimaye kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika maarufu AFCON baada ya kuikosa kwa miaka 38.

Lakini haikuwa vile kama ilivyosubiriwa na wengi kwa hamu kubwa. Kila mmoja aliondoka sehemu walizokuwa wakiangalia mpira wakiwa na nyuso za majonzi, hakuna aliyetamani kuongea. Hakukuwa na tabasamu lolote usoni.

Akina mama, watoto na wazee walikusanyika maeneo mbalimbali kufuatilia mchezo huo uliopigwa jijini Maseru nchini Lesotho lakini mwisho wa siku walihisi kama walikuwa na gundu ikiwa wengi wao si wafuatiliaji wa soka. Taifa Stars bado nafasi ya kusonga mbele wanayo kama watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Uganda na wakati huo huo Cape Verde amfunge Lesotho.

Hatukutakiwa kufika huku kote kwa kuombeana dua mbaya zaidi ya kushinda mchezo ule muhimu, tusubiri tuone huko mbele kitakachotokea katika barabara hii ngumu.

Kwa hali ilivyo, inabidi tukubali kurudi kwenye misingi ya soka ili kuwa na kikosi bora cha timu ya taifa, hakuna njia nyingine zaidi ya kuitunza Serengeti Boys.

Matumaini ya Watanzania yamebebwa na Serengeti Boys ambao wanapikwa taratibu ili kuwa nyota wa baadaye wa taifa hili ambalo ni dhahiri limekata tamaa katika mchezo wa soka. Angalia jinsi Serengeti Boys wanavyotengenezwa, waswahili huwa wanapenda kutumia msemo mmoja maarufu ‘Samaki mkunje angali mbichi’. Hicho ndicho kifanyike kwa vijana hao.

Naamini kupitia Serengeti Boys kila historia mbaya kwetu itageuka ndoto sababu tutakuwa na timu iliyojengwa katika misingi ya soka kwa ukamilifu zaidi.

Mwakani michuano ya Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 itafanyika hapa nchini, ndio ni Serengeti Boys waliofanikisha hilo bila uwepo wao sidhani kama fursa hiyo ingepatikana.

Fainali hizo zinatarajiwa kupigwa hapa nchini kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ilipopata nafasi ya kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Tayari vijana wetu wameonyesha picha nzuri baada ya kutwaa taji la vijana la CECAFA chini ya miaka 17 iliyofanyika nchini Burundi huku wakionyesha kiwango kizuri.

BAADA ya misimu mitano kupita, hatimaye klabu ya Simba imefanikiwa kurudi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wataanzia kibarua hicho dhidi ya Mbabane Swallows ya Estwaini. Itakuwa ni mara ya pili hivi karibuni Mbabane Swallows kuingia hapa nchini baada ya kucheza dhidi ya Azam FC kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Itakumbukwa katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, wageni hao walifungwa bao 1-0 kabla ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 mchezo wa marudiano na kuiondoa Azam FC.

Simba ikifanikiwa kuiondosha Mbabane Swallows itakwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kuingia katika makundi ya michuano hiyo kwa kucheza na mshindi kati ya UD Songo ya Msumbiji na Nkana FC ya Zambia, anayochezea beki wa zamani wa Yanga, Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy ambaye pia aliwahi kuichezea Simba.

Wawakilishi wa Zanzibar, JKU watamenyana na Al Hilal ya Sudan ambayo hivi karibuni straika wa timu ya taifa ya Tanzania, Thomas Ulimwengu, alivunja mkataba nao ambapo mshindi atacheza na mshindi wa mechi nyingine baina ya APR FC ya Rwanda na Club Africain ya Tunisia michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitachezwa kati ya Novemba 27 na 28 na marudiano ni Desemba 4 na 5 mwaka huu, wakati mechi za kwanza za raundi ya pili na ya mwisho ya mchujo zitachezwa kati ya Desemba 14 na 16 na marudiano Desemba 21 na 23 mwaka huu.

Katika Kombe la Shirikisho Afrika, Mtibwa Sugar iliyofanikiwa kukata tiketi hiyo kwa kutwaa taji la Shiriksho la Azam itaanza na Northern Dynamo ya Shelisheli na ikivuka mtihani huo itakutana na KCCA ya Uganda.

Wawakilishi wa Zanzibar, Zimamoto wamepewa kigogo wa soka la Afrika Kusini, Kaizer Chiefs, na mshindi baina yao atakutana na mshindi kati ya El Geco ya Madagascar na Deportivo Unidad ya Equatorial Guinea.

SIMBA v MBABANE SWALLOWS

Ni moja ya michezo inyosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka hapa nchini. Baada ya ratiba hiyo kutoka, kocha wa Simba, Patrick Aussems, alisema anaamini ubora wa kikosi chake unaweza kuisaidia timu hiyo kupata matokeo ya ushindi na kusonga mbele.

Lakini si mchezo rahisi kama mashabiki wa soka wanavyodhani kwasababu Mbabane Swallows ni moja ya timu zenye wachezaji wa viwango vya juu. Miongoni mwa wachezaji waliotokea timu hiyo ni Asante Kwasi anayekipiga Simba na kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi.

Kwa maana hiyo huo mchezo si mwepesi, inabidi mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wajipange vizuri kuikabiri timu hiyo.

MTIBWA SUGAR v NORTHERN DYNAMO

Mabingwa Kombe la Shirikisho la Azam, Mtibwa Sugar, watatupa karata hiyo yao michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Northen Dynamo ya Shelisheli. Huo si mchezo mwepesi pia.

Northern Dynamo inapatikana katika kisiwa cha Mahe ambacho ni kikubwa kilichopo nchini Shelisheli ambacho kinakadiliwa kuwa na wakazi 77,000.

Imepita miaka zaidi ya 10 tangu Mtibwa Sugar iliposhiriki michuano ya kimataifa, swali ambalo lipo kutoka kwa wadau wa soka hapa nchini kama watafanikiwa kusonga mbele baada ya mchezo huo kumalizika.

Licha ya kutofanya usajili wa wachezaji wa kigeni, bado kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila, anaamini wataweza kuwapa raha mashabiki wa soka hapa nchini.

Kikosi cha Serengeti Boys

Kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo viwanja vya Boko Veterans jijini Dar es Salaam. Picha ya maktaba

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.