Si ajabu jeshi kutumika kuokoa uchumi

Rai - - MAONI/KATUNI -

HATUA ya Serikali ya awamu ya Tano ya kulitumia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika baadhi ya oparesheni zake unaonekana kupokea tofauti na baadhi ya wananchi na wanasiasa.

Katika siku za hivi karibuni serikali imewatumia JWTZ kwenye oparesheni ya kupakia, kusafirish­a na kuwalipa wakulima fedha za korosho pamoja na ile ya ukaguzi na udhibiti wa biashara haramu ya fedha za kigeni na ukiukaji wa sheria katika kuendesha biashara ya ubadilisha­ji fedha ‘bureau de change’.

Tulio wengi tunaamini oparesheni hizi huenda hazipaswi kufanywa na jeshi, ambalo kazi yake kuu ni kulinda Katiba, Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mipaka ya nchi.

Ni kweli kabisa, jeshi hilo lilianzish­wa Septemba 1, 1964 likiwa na majukumu hayo muhimu, hata hivyo kadiri siku zilivyoson­ga ndivyo jeshi hilo liliongeza majukumu mengine ikiwa ni pamoja kushirikia­na na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa, kutoa huduma mbalimbali za kijamii, kukuza elimu ya kujitegeme­a na uzalishaji mali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kushiriki ulinzi wa amani Kimataifa.

Ukiangalia majukumu hayo hapo juu utabaini kuwa haya yanayofany­wa sasa na jeshi letu ni miongoni mwa majukumu yao kupitia kipengele cha kutoa huduma mbalimbali za kijamii.

Jeshi limesimami­a oparesheni hizi pasi askari wake kuwa na mitutu mikononi, hatua inayoonesh­a kuwa kazi hizo ni za amani.

Uamuzi wa Rais kulitumia Jeshi la Ulinzi wakati huu wa amani kufanya kazi ya kusimamia ununuzi na usombaji wa korosho katika mikoa ya Kusini, ni uamuzi sahihi kabisa, usio na mawaa.

Wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya Kwanza iliyokuwa chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Jehsi kupitia JKT lilitumika kuwahamish­a wananchi kwenye vijiji vya ujamaa wakati wa Operesheni Vijini.

Lengo la oparesheni ile lilikuwa ni kuleta maendeleo ya pamoja na kuiwezesha Serikali kutoa huduma za kijamii kwa ufanisi zaidi kama ambavyo inafanya sasa kuwasaidia wakulima wasipate hasara kutokana na zao la kukosa wanunuzi.

Tunatoa rai kwa maofisa wa jeshi wanaopewa majukumu ya kusimamia oparesheni hizi za kijamii, kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu stahiki, ili kuepusha kwa namna yoyote ile matumizi mabaya ya dhamana waliyopewa na Amiri Jeshi Mkuu.

Aidha ni vema wananchi wakatoa ushirikian­o kwa askari wanaosimam­ia oparesheni za namna hiyo hasa hii ya korosho, ili iwe rahisi kwao kutekeleza kile wananchopa­swa kukifanya bila kusababish­a madhara.

Aidha tunaamini upo umuhimu wa wananchi kufahamish­wa mapema uwapo wa jeshi kwenye oparesheni zile zitakazosi­mamiwa na wao ili kuepusha taharuki.

Si suala la ajabu na kushangaza kwa askari wa jeshi kutumika katika masuala nyeti na muhimu kama haya ambayo yanaugusa moja kwa moja uchumi wan chi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.