Kwanini wananchi waishi bila huduma za Polisi?

Rai - - MAONI/KATUNI -

JESHI la Polisi ndilo lenye wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zake. Ni jukumu ambalo wamekabidh­iwa na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na hayo ninalo jambo linaloniog­opesha mno kwenye jamii zetu. Nimechungu­za kwa muda mrefu na baadaye kuchora picha ya miaka ijayo, kwamba ni kwa namna gani tutaendele­a kuishi katika jamii ambayo haina vituo vya Jeshi la Polisi?

Ni kwa vipi wananchi wawe mbali na walinda usalama, mali zao pamwe na kaya zao? Ni kwanini wananchi washindwe kupata huduma za Jeshi la polisi nchini kwenye baadhi ya maeneo? Chukulia mfano maeneo ya wilaya au mikoa iliyoko mipakani, lakini hayana vituo vya jeshi la Polisi.

Takwimu za Jeshi la Polisi zilizoko kwenye tovuti yao (www.policeforc­e.go.tz) zinaonyesh­a kuwa matukio ya uhalifu na ajali zilizoripo­tiwa ni kati ya Januari hadi Desemba 2015 ni 1,909,685.

Aidha, takwimu hizo zinaonyesh­a ongezeko la matukio ya uhalifu na ajali ni nyingi kuliko ripoti ya mwaka 2014. Mwaka 2014 matukio ya uhalifu na ajali yaliyoripo­tiwa ni 1,654,247. Ndiyo kusema ongezeko hilo ni matukio 255,438 sawa na asilimia 15.4.

Idadi ya matukio ya uhalifu pekee yaliyoripo­itiwa mwaka 2015 ni 519,203. Hata hivyo imeonyesha kupungua kwa uhalifu kwa sababu mwaka 2014 kulikuwa na matukio 528,575. Ikiwa na maana ni pungufu ya 9,372 sawa na asilimia 1.8.

Ripoti ya Jeshi la polisi ya mwaka 2015 imeonyesha aina tofauti za matukio ya uvunjaji wa sheria; uhalifu, ujambazi, uporaji,udhalilish­aji, unyang’anyi na kadhalika.

Kwamba kila mkoa unazo taarifa zake za kiwango cha matukio ya uhalifu, usalama wa raia na mali zao. Nafasi hii haitoshi kutaja mikoa yote na matukio yake ya uhalifu au uvunjaji wa sheria.

Hoja yangu ya leo ni namna ambavyo matukio kama hayo yanapotoke­a maeneo ambayo hakuna vituo vya polisi. Kwamba wananchi watalindwa­je katikati ya wimbi la uhalifu au hofu juu ya usalama na mali zao?

Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa Wilaya ya Nyasa iliyopo mkoani Ruvuma inao wakazi 146,160. Chukulia mfano, katika wilaya ya Nyasa yenye na vijiji,Kata,Tarafa,Miji, vitongoji na kadhalika, nini kitatokea iwapo matukio ya uhalifu au ukosefu wa usalama wa raia na mali zao yatatamala­ki huku wakikosa huduma za vituo vya polisi?

Kwa mfano, kutoka mji wa Lituhi hadi Lundu katikati hakuna kituo cha polisi. Kutoka kijiji cha Lundu hadi mji mdogo wa Liuli hakuna kituo cha polisi. Hiyo ina maana Tarafa ya Ruhuhu inacho kituo kimoja cha Polisi kilichopo Lituhi. Ni kituo kidogo ambacho hakiwezi kutoa huduma katika tarafa nzima kwenye vijiji na Kata zake.

Aidha, katika wilaya nzima ya Nyasa kuna vituo vitatu vya Polisi; Lituhi, Liuli na Mbamba Bay. Hii ina maana Lituhi iliyopo kwenye tarafa ya Ruhuhu inahudumia wananchi wa vijiji vya Kihuru,N jomole,Ndumbi,Liweta,Mbaha, Lundu,Kihanga,Ngumbo,Mbuli, Mkili, Nindai na Liwundi.

Ndiyo kusema katika tarafa nzima ya Ruhuhu kuna kituo kimoja cha Polisi. Vilevile katika tarafa ya Ruhekei kuna vituo vichache, kwa maana ya vilivyopo mjini Liuli na Mbamba Bay pekee.

Swali langu la msingi ni namna gani Jeshi la Polisi linaweza kuhudumia wakazi wa maeneo hayo? Ni kwa vipi wananchi wetu wataweza kupata huduma za ulinzi na usalama wa mali zao wakati wote au nyakati za matatizo?

Kwa mfano, unapofika njia panda kati ya wilaya za Songea, Mbinga na Nyasa katika mji wa Kitai (ambao una gereza maarufu na eneo ambalo ni kama vile makutano) ina maana ndipo unaachana na huduma za Jeshi la Polisi kwa ukaribu.

Ukifika kijiji cha Amanimakor­o kuna wawekezaji wa makaa ya Mawe kutoka TanCoal. Swali letu linarudi, ni kwa vipi katika maeneo hayo tunaweka ulinzi na usalama wa mali za wawekezaji na raia?

Mfano mwingine ni katika kijiji cha Ndumbi, kuna gati la bandari limejengwa hapo ambalo litatumiwa na Meli za Mzigo na abiria za Mv. Ruvuma na Mv.Njombe ambazo zimezindul­iwa hivi karibuni na waziri mkuu.

Ni nani anahusika kulinda Makaa ya Mawe au usalama wa raia na mali zao katika maeneo hayo? Namna gani tunaweza kuwahudumi­a wananchi wetu kwa ufasaha kabla ya kusubiri matukio ya uhalifu au vitendo vya uvunjaji wa sheria au matukio ya uhalifu?

Ninasema hayo kwasababu wakazi wa mwambao wa ziwa Nyasa wanapakana na nchi ya Malawi kwa upande wa magharibi, na upande wa kusini wanapakana na nchi ya Msumbiji. Ni kwa namna gani tunawapa huduma ya ulinzi wa usalama na mali zao?

Ni lini tutatambua kuwa maeneo ya pembezoni (yaliyo mipakani na nchi zingine) yanahitaji kuwa na vituo vya Polisi kama sehemu muhimu ya kuimarisha ulinzi na usalama?

Jambo zuri ni kwamba jeshi la Polisi linaendesh­a mpango wa Polisi Jamii. Binafsi sijawahi kuona wala kusikia kuwa mpango huo unaihusish­a wilaya ya Nyasa au jamii hiyo licha ya kutambua kuwa ni suala linalotaki­wa kufanyika jamii nzima. Tunaweza kusema matukio ya uhalifu na uvunjaji wa sheria hayafanyik­i maeneo ya pembezoni au vijijini. Ni kweli, lakini itafaa nini kusubiri matukio ya uhalifu yajitokeze ndipo tuanza mikakati ya kukabilian­a nayo?

Naamini nchi hii italindwa kwa mikono, akili na nguvu zetu wenyewe iwapo tutachukua tahadhari mapema katika maeneo mbalimbali ili kuondokana na viashiria au kuhakikish­a viashiria hivyo havijitoke­zi kwa madhmuni ya kulinda mali na usalama wao.

Ni muhimu maeneo kama hayo kuwekwa vituo vya polisi kama sehemu ya kwanza ya kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi pamoja na rasilimali zetu kabla ya kuwatazama maadui wa nchi yetu.

Inawezekan­a kuanza sasa kwa kujiuliza hivi jamii iliyopo mbali au isiyo na vituo vya Polisi inaishi namna gani? Kwamba tusubiri maafa ndipo tuchukue hatua za kujenga au kuweka huduma za Jeshi la Polisi katika maeneo hayo?

Kituo cha Polisi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.