K na miaka mitatu ya Magufuli

Rai - - MAKALA -

ni mengi ambayo yamekamilika lakini bado tuliyoahidi ni mengi zaidi kwa hiyo niseme inardhisha. Kwa mfano kwenye usafiri wa anga kwanza ni viwanja vya ndege tulianza kazi sisi ya kuboresha viwanja vya ndege nchini,viwanja vingi vya ndege Kigoma, wapi, wapi ile kazi tumeianza na vingine vimekamilika kipindi change na vingine kazi inaendelea hadi sasa.

Kiwanja cha Dar es Salaam tulisema jambo kubwa ni kujenga terminal ile mpya, nadhani miongoni mwa mawe ya msingi ya mwisho niliyoweka lilikuwa ni lile la kiwanja cha ndege hapo, sasa kinakaribia kwisha, vile vile tumeweka mawe ya msingi kipindi changu mimi lakini kazi ambayo unategemea itakuja kuendelea na awamu nyingine wangeamua kusimamisha lakini hakikusimama na kiwanja kile kanaelekea kukamilika kwa sababu kiwanja kile tulichokuwa nacho sasa hakina uwezo, kuimarisha shirika la ndege mimi nasema Rais jasiri, sisi tumeshughulika sana na ATC tumetumia fedha nyingi za Serikali kuendesha lile shirika maana ni kama vile shirika la biashara mnaliendesha kwenye bajeti ya serikali ni kazi ngumu kweli inafika mahali mnakata tama maana mnapeleka fedha kama vile unachota maji unapeleka kwenye pipa kama vile limetoboka hii kazi haishi, sasa Rais huyu amekuwa Rais jasiri kununua ndege mpya, kazi ngumu sasa pale ni kusimamia uendeshaji wa shirika la ndege maana shirika lile kazi kubwa ni usimamizi nakumbuka wakati ule wa mzee Nyerere lilifikia ndege 14 lakini zimekwenda zimepungua mpaka tukawa tena hatuna, kipindi hicho tukanunuia ATR hizi lakini tatizo kubwa pale ni management.

Matumaini yangu ni kuwa kwa uwekezaji huu mkubwa ambao serikali imewekeza pia italitazama suala la management, tusipotazama suala la management tutarudi kule kule maana tulifika mahali hata mafuta yalikuwa yanawashinda hata kununua, kwa hiyo mnatenga milioni 500 kila mwezi kwa ajili ya ATC kununua mafuta ili ndege ziwqe angani.

Ndiyo maana nasema uwekezaji mzuri ni Rais mzuri tunampongeza lakini usimamizi wa management ya ATC ndiyo changamoto kubwa. Mzee Nyerere akaacha ndege nyingi zimekwenda zinapungua moja na nyingine, nyingine na nyingine mpaka kufikia kipindi chetu tukawa tunaishi kwa ndege za kukodi.

Wakati fulani wakakodi ndege ya Ethiopia Air way nakumbuka Boeing ikawashinda kulipa kukawa na madeni kila wakati wanasukuma madeni serikalini kwa hiyo ni kuangalia management otherwise ni Rais jasiri na ni uamuzi wa kijasiri, maneno mengi yamekuwapo lakini ingekuwa ametumia fedha kununua mambo yake mwenyewe, lakini ametumia fedha kununua ndege za Serikali hata zogo lenyewe sikulielewa.

Unasikia watu wote duniani hawatumii fedha zao kununua ndege kwani lazima, kama una uwezo wa kununua kwanini usinunue? Zimenunuliwa ndege ni uharibifu watu wote wanakodisha kama tuna uwezo wa kununua kwanini twende tukakope, kama tumeweza kununu, unajua kupanga ni kuchagua ukipanga sasa nataka kutumia hizi fedha kwenda kununua ndege zimenunuliwa zipo.

Suala kubwa mimi ninasema ni management, nimesema la kwanza ilikuwa ni kupambana na umaskini, la pili ni ajira kwa vijana, maana kuna yale mambo ambayo CCM imeyaahidi la kwanza kupambana na umaskini la pili ajira kwa vijana kwamba suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazolikabili Taifa letu.

Off cause ni dunia nzima na ninakumbuka watani wetu wanasema unajua hili la vijana kukosa ajina ni timing bomb lakini sina hakika walikuwa majawabu sahihi zaidi ya kulizungumza kwa maana ya kujenga dhana kwamba sisi ndani ya CCM hatuna majawabu nalo.

Lakini kwenye ilani ya uchaguzi imelieleza vizuri sana na kusema ni tatizo kubwa na baada ya kupanuka kwa elimu ya sekondarina ya vyuo vikuu limekuwa sasa tatizo kubwa la wasomi kutokuwa na ajira, zamani lilikuwa

tatizo la waliomaliza darasa la saba lakini sasa limekuwa la waliomaliza sekondari na waliomaliza vyuo vikuu.

Kwenye ile ilani ilikuwa inaagiza Serikali yake kufanya kuanzisha viwanda katika kipindi cha miaka mitano ijayo, maana nataka miwasomee ili mjue jitihada za kulipatia ufumbuzi tatizo la ajira nchini zitaendelezwa kipaumbele kitakua katika kukuza na kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vilivyo na uwezo wa kuajiri watu wengi.

Kwa sababu unaweza ukawa na viwanda vya teknolojia ya kisasa vinavyotumia roboti ukawa na kiwanda kikubwa lakini hiumo ndani ukiingia watu wanaofanya kazi ni kidogo wafanyakazi ni mashine tu lakini ilani inaagiza hivi.

Kwa hiyo matumaini yangu ni kwamba wanapowasiliana na wale wanaojenga viwanda wanalizingatia hili, maana unaweza ukazungumza tumejenga viwanda 1000 lakini wameajiri watu wangapi?

Unaweza kujenga viwanda 1000 vya kuajiri watu 2,000 tu, ujue kuna tatizo la aina ya teknolojia iliyotumika maana kama ni Capital intensive au labour intensive na hapa sisi ilani ya CCM inachoitaka serikali yake iwe na viwanda ambavo vinavyoweza kuajiri watu wengi, maana yake iwe ni labour intensive technology iwe adopted.

Sasa hili limekuwa kitu kama unaweza kusema ni signature project platform ya Rais tangu wakati wa kampeni. Kwenye mkutano wetu pale Ikulu kabla ya siku ile ya kampeni mambo gani tuliyatilia mkazo na kwenye CCM nasema Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda na hili limepata msukumo mkubwa, linatekeleza ilani hii ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwamba tushughulikie na tatizo la ajira la vijana hakuna manma lazima tukazania viwanda viwanda vitakapoongezeka ndipo tutaweza kuajiri vijana wengi.

Kwa hiyo mimi ninachosema Serikali inafanya vizuri, Serikali ya awamu ya tano inatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, mie mwenyekiti niliyekabidhi ilani niko poa kabisa.

Haya maneno haya midomo imeumbiwa kusema haitaacha kusema mimi siku moja simtaji mbunge mmoja wa upinzani nikamuuliza lakini nyie rafiki yangu mbona kila kitu tunachokifanya kibaya, akasema kwani sisi hatujui, tunajua lakini tukikaa na kuwasifia watu watauliza kwanini tuko upande huu. Kwa hiyo hata mkijenga barabara tutatafuta pale penye shimo tutasema ile barabara wamejenga lakini ile kona wamekosema magari yanapinduka sana pale, mimi nasema kitu kikubwa ni kutambua kwamba kuna kitu ambacho tuliwaahidi wananchi tuwaongoze tutimize ahadi zetu hakuna mtu wa kutunyooshea kidole.

Kwa hiyo ndiyo pointi nilikuwa nasema hata mimi wanasema unajua hili halipo, hili halipo nikasema hilo ni lako wewe lakini kwa niliyoahidi mie ni haya wanakwenda vizuri wabaki na msimamo huo huo wanaokwenda nao changamoto haziishi na kila siku zinajitokeza.

Mikakati iliyokuwapo na dhamira ya Rais mwenyewe na Serikali yake tutafika tunapopakusudia miaka mitano ijayo tutakuwa tumefika mahali pazuri nasema kwamba tathmini ya siasa unapoitazama kwa hali ya amani na utulizu nchi iko shwari shughuli zinakwenda, haina maana kwambba hakuna haja ya kuboresha hili na lile.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.