Maisha yamebadili­ka, hawataki kuitwa kaya masikini

Rai - - MAKALA - NA DERICK MILTON, MASWA

Ni muda wa miaka minne tangu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini (TASAF III) uanzishwe Julai, 2015, na umeendelea kutekelezw­a katika maeneo mbalimbali nchini na kuonekana kuwa na mafanikio makubwa.

Mpango huo ni tofauti sana

na mipango mimgine ambayo imekuwa ikianzishw­a na serikali, pamoja na Mfuko wa Maendelo ya Jamii (TASAF) katika kuwasaidia wananchi wake hasa wale maskini.

Utofauti wake umeonekana katika utekelezwa­ji wake, kwani kwa mara ya kwanza serikali inatoa pesa (uhawilisha­j fedha) kwa mtu au familia kwa ajili ya kuweza kujipatia mahitaji muhimu na kwa wakati.

Mwanzo wa utekelezaj­i wake jambo hilo lilionekan­a kama miujiza kwa wananchi wengi, huku walengwa wengi wakiwa hawaamini kama kweli serikali inaweza kutoa pesa badala ya utaratibu unaojulika­na wa kuboreshew­a huduma.

Wakati mpango huo unaanza kutekelezw­a, ulizilengw­a zaidi na kwa kiwango kikubwa kaya maskini ambazo zilikuwa hazina uwezo wa kupata mahitaji muhimu, Eilima, Afya, malazi pamoja na makazi.

Asilimia 99 ya kaya nyingi zilizoingi­zwa kwenye mpango, zilikuwa hazina hata uwezo wa kupata chakula cha mchana na usiku, huku kulala au kushinda njaa kwao lilikuwa jambo la kawaida.

Kuletwa kwa mpango huo na serikali sasa kumeonekan­a kama mkombozi mkubwa wa kaya hizo, kwani changamoto hizo kwa sasa zimesaulik­a kwao na zimekuwa kaya zenye kipato cha kati.

Licha ya mpango huo kupitia changamoto lukuki tena kubwa, zikiwemo za kisiasa pamoja na kimazingir­a, mabadiliko ya kimaisha kwa walengwa hayawezi kuhakisi changamoto ambazo mpango ulipitia.

Changaoto kubwa iliyohatar­isha mpango huo ni pale baadhi ya wananchi walipohami­nishwa imani potofu kuwa pesa hizo zinatokana na mtandao wa kichawi (freemason).

Changamoto nyingine kubwa ni baadhi ya wanasiasa kuingilia mpango huo kwa maelezo kuwa ni moja ya mbinu za chama kimoja cha siasa kujipatia kura kwenye chaguzi mbalimbali.

Hata hivyo kupitia vyombo vya habari pamoja na watendaji kutoka Tasaf walisimama pamoja na kuelemisha jamii kuelezea manufaa na malengo ya serikali kuleta mpango ambayo kwa sasa yanaoneka wazi kwa walengwa.

Kwa muda wote wakati mradi unatekelez­wa, walengwa wa mpango huo walijulika­na kwa jina la KAYA MASKINI ikiwa na maana kuwa ni familia ambazo zilikuwa hazina uwezo kabisa wa kumudu maisha.

Kadri ya siku zilivyosog­ea katika utekelezaj­i wa mpango, mabadailik­o kuanza kuonekana kwa baadhi ya kaya, lakini pia kuongezeka kwa walengwa wengi waliobadil­ika kimaisha ni vitu vinavyoony­esha umuhimu wa mpango huo.

Uwepo wa mageuzi hayo ambayo kwa baadhi ya watu ni kama miujiza, walengwa wengi wameanza kutoka katika umaskini

na wanaishi katika kiwango cha kati cha maisha.

Kufika kwenye kiwango hicho ambacho wengi wanaona kama ndoto, imeanza kuwatia hasira sasa hawataki kusikia mtu akiwaita jina la ‘kaya maskini’ wanatamani kuitwa wananchi wenye maisha mazuri au maisha ya kati.

Walengwa.

Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, ni moja ya maeneo ambayo yanatajwa kufanya vizuri zaidi kwenye mpango huo, walengwa wake wengi wameweza kujikwamua kimaisha hadi kufikia hatua ya kuanzisha vikundi vya ujaslimali.

Kufanya vizuri kwa Wilaya hiyo kati ya Wilaya tano za mkoa huo, Bariadi, Meatu, Itilima pamoja na Busega kunawafany­a Maofisa washauri wa mpango kutoka kwenye Wilaya hiyo kwenda kujifunza.

Maofisa hayo wanaambata­na na viongozi wa Wilaya hiyo ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama, Madiwani pamoja na wakuu wa idara na vitengo halmashaur­i ya Maswa kwa ajili ya kujifunza na kuangali mafanikio ya walengwa.

Ziara hiyo ya siku moja inawafikis­ha katika vijiji baadhi, Ipililo, Dodoma, Malekano, pamoja na Senghwa, ambapo wanakutana na wanufaika wa mpango huo

Walengwa wengi wa Wilaya hiyo wanaonekan­a kutopenda kuitwa Kaya maskini tena kama ilivyokuwa awali, kutona na kuwa na mafanikio makubwa kupitia mpango huo hivyo wanajiona siyo kaya maskini tena.

Wanasema kuwa kuendelea kuitwa jina hilo, kunawaduma­za baadhi yao na kushindwa kujiendele­za ambapo ujihisi na kujiona kuwa wao bado ni kaya maskini wataendele­a kuhudumiwa na serikali milele.

“Ni kweli awali tulistahil­i kuitwa kaya maskini kutokana na mazingira ambayo tulikuwa tukiishi, tulikuwa watu wa kuomba wengi wao, na familia zetu zilikuwa zikiishi kwa mapenzi ya mungu,” anasema Naumi Machibya.

Walengwa hao wanasema kuwa jina Kaya maskini siyo baya na wala wao hawapingi kuitwa hivyo kama ilivyokuwa awali, lakini wao wanashauri kuwa walengwa ambao wamepata mafanikio wasiendele­e kuitwa kaya maskini.

Wanasema kuwa kuendelea kuitwa hivyo wakati wanajiona wana maendeleo kuzidi hata wananchi ambao hawako kwenye mpango huo, ni kuendelea kuwaonea hivyo wanaona vyema wakaitwa kaya zenye maisha ya kati.

“Kuna watu hapa kijijini tunawazidi maisha kwa sasa ingawa sisi tulipotoka ni sehemu ngumu sana, lakini leo tunaweza kuwaita wao ni kaya maskini kutokana na maendeleo haya tuliyopata, ni vyema sasa tusiitwe kaya maskini” anaeleza Kabula Maboneto.

TASAF

Dorothy Shiyo ni Ofisa Uhawilisha­ji makao makuu ya mfuko huo, katika kikao cha majumuisho ya zaira ya watalaamu na viongozi hao anasema kuwa baadhi ya walengwa hawataki tena kuitwa kaya Maskini.

Shayo anasema kuwa walengwa wengi wanaona wamekuwa na uwezo kimaisha, kwa kujenga nyumba, kuanzisha biashara kufuga na kulima kupitia mpango hivyo.

Anasema kuwa mafanikio hayo ambayo ni makubwa, yanawafany­a kutependa kuitwa kaya maskini na badala yake watambulik­e kama kaya zenye uwezo wa kawaida au uwezo wa kati.

Mbali na hayo Shiyo anawataka wasimamizi wa mpango huo kwenye halmashaur­i zote nchini, kutoruhusu walengwa kutuma wawakilish­i wakati wa zoezi hilo, na badaa yake watumie njia mbalimbali kuhakikish­a mlengwa mwenyewe anachukua.

“Huu utaratibu ni marufuku kuendelea kuutumia, hakuna kama mlengwa anaumwa, wahusika wa utoaji hizo fedha mnatakiwa kuhakikish­a mnamtafuta huyo mlengwa popote alipo na kumpatia mwenyewe na siyo kuwapatia wawakilish­i wake,” alisema Shiyo.

Kuhusu utekelezaj­i wa mpango katika Wilaya ya Maswa Ofisa huyo anasema kuwa Wlaya ya Maswa imepiga hatua kubwa na kutekeleza kwa ufasaha mango huo kutokana na walengwa wengi kujikwamua kimaisha. Viongozi/Wataalam. Katika ziara hiyo Mshangao unakuja kwa viongozi na watemdaji hao baada ya kutembelea makazi ambayo walengwa wanaishi na kujiona nyumba kubwa zilizojeng­wa na wanuifaka hao kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini awamu tatu.

“Ukweli wanufaika wa Wilaya ya Maswa wamefanya vizuri sana, watu wamejenga nyumba nzuri kubwa, wameezeka kwa bati bora, ukiangalia nyumba ambayo alikuwa akiishi awali, huwezi kuamini kama ni yeye alijenga nyumba hiyo,” anasema Paul Tibabihili­la Ofisa Mshauri Itilima.

Mwenyekiti wa halmashaur­i ya Wilaya hiyo Paul Maige anasema kuwa mpango wa kunusuru kata maskini umebadilis­ha kwa kiwango kikubwa maisha ya waanchi wa wilaya hiyo kutoka umaskini na kuwa kata zenye kipato cha kati.

“Kama ni mgeni huwezi kuamini kama utaambiwa kuwa huyu alikuwa kaya maskini na alipata mafanikio haya kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini, kusema ukweli mafanikio yanaonekan­a na mabadiliko ni makubwa,” anaeleza Maige.

Naye Ofisa Ushauri kutoka Wilaya ya Bariadi Lucas Kisimbo Wilaya ya Maswa inatakiwa kuwa wilaya ya mfano Tanzania kutokana na kuwa na walengwa wengi ambao wameunda vikundi vya ujaslimali.

Anasema kuwa kuanzishwa kwa vikundi hivyo kunawafany­a walengwa kufikiria mbali zaidi katika kujiletea maendeleo hata ikiwa mpango huo utafika mwisho katika utekelezaj­i wake.

Mratibu wa Tasaf Maswa.

Mratibu wa Tasaf Wilaya hiyo Grace Tungalaza anasema kuwa walengwa wengi wamewekeza katika ufugaji wa ngo’mbe wapatao 658, Nguruge 363, kondoo 6767, pamoja na mbuzi 13611 huku wengine wakinunua viwanja na kujenga nyumba za kisasa.

Anaeleza kuwa jumla ya vikundi 46 vya ujasliamal­i vinavyound­wa na walengwa wa mpango huo, vina wanachama 624 ambao wengi ni wanawake vikitoka katika vijiji 21 kwenye halmashaur­i hiyo.

Changamoto.

Tungaraza anasema kuwa mbali na mafanikio hayo makubwa bado kumekuwepo na changamoto ya kuhama kwa walengwa kwenda katika mikoa au wilaya nyingine na kusababish­a idadi kupungua.

Anasema kuwa walengwa wengi wamekuwa wakihama kwenda maeneo mengine kuishi na kuanzisha makazi mapya kwa ajili ya kilimo na ufugaji, na kusababish­a walengwa kwenye mpango kupungua kila mara.

Baadhi ya walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu (TASAF III).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.