Mifuko ya jamii itekeleze agizo la JPM

Rai - - MAKALA - NA AMINA OMARI, TANGA

SERIKALI ya awamu ya Tano imejikita katika kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda kwa lengo kuhakikish­a nchi yetu inakuwa na uchumi imara pamoja na kuwahakiki­sha wananchi wake ajira.

Kutokana na kutekeleza sera hiyo kumekuwa na juhudi mbalimbali ambazo serikali imekuwa ikichukuwa ikiwemo kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini, kuwahamasi­sha wazawa nao kuweza kuwekeza.

Hali hiyo imechangia kuwapo kwa wimbi kubwa la wawekezaji kuja kuwekeza nchini katika sekta ya viwanda. Kutokana na uwekezaji huo Tanzania itakuwa na hitaji kubwa la saruji kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo pamoja na miundombin­u mengine kama barabara, hospitali na mashule.

Inakadiriw­a kwamba baada ya miaka mitano hadi sita kutoka sasa hitaji la saruji kwa ajili ya matumizi ya ndani linaweza kukua kwa kasi kutoka tani milioni 4.7 hadi kufikia tani milioni 8.2 kwa mwaka.

Kutokana na hitaji hilo ndipo serikali inaweza kupokea maombi mbalimbali ya ujenzi wa viwanda vya saruji kwa ajili ya kuongeza uzalishaji pamoja na kuuza ziada katika masoko ya dunia.

Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Rhino kilichopo jijini Tanga ni mmoja ya kiwanda ambacho mwekezaji wake mkuu ni kampuni ya ARM kutoka nchi Kenya ambayo iliamua kuja kuwekeza hapa nchini.

Uwekezaji huo mwenye zaidi ya Sh bilioni 556 ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha malighafi ya kuzalishia saruji yaani klinka katika eneo la Maweni Jijini Tanga.

Mkurungenz­i Mtendaji wa kiwanda hicho, Pradeep Paunrama anasema ukuaji wa kasi ya kiuchumi wa Tanzania pamoja na utaratibu mzuri uliko wa kuwapokea wawekezaji uliweza kuongeza ushawishi wa kampuni yao ya ARM iliyoko nchini Kenya kuvutika kuwekeza hapa nchini.

Anasema kuwa kiwanda hicho uwezo wake ilikuwa ni kuzalisha clinka tani milioni 1.2 kwa mwaka lakini toka walipoanzi­sha mpaka sasa wanazalish­a tani 4000.

Kiwanda hicho ambacho kilianza uzalishaji wake mwaka 2014 kwa kuzalisha clinka na kuisambaza katika nchi za Kenya Uganda Rwanda Congo ambako hitajio la malighafi hiyo ni kubwa.

“Licha ya kutumia kiasi cha malighafi hiyo kuzalisha saruji hapa nchini lakini tunasafiri­sha clinka kwa ajili ya kuuza katika nchi nyingine ambazo zinauhitaj­i mkubwa wa malighafi hiyo “anasema

Hata hivyo, Meneja Udhibiti Ubora, Simon Kikota anasema wakati wa kiwanda kilipokuwa kinazalish­a hapo awali waliweza kukidhi hitaji la ndani kwani waliweza kuzalisha tani 400,000 kwa mwaka.

Aidha, kila penye mafanikio hapa kosi changamoto kwani ilipofika mwaka 2015/16 walishindw­a kuzalisha vizuri kutokana na kasoro ya upatikanaj­i wa umeme wa uhakika. Mwaka huo nchi ilikubwa na mgao mkubwa wa umeme hivyo kusababish­a kiwanda hicho kuzalisha chini ya kiwango hali iliyosabab­isha kupata hasara katika uwendeshaj­i.

Kikota anasema kuwa licha ya hasara hiyo mpaka sasa changamoto ya upatikanaj­i wa umeme imekuwa ni sehemu ya kero kubwa katika kiwanda hicho ambacho hutumia nishati hiyo kwa ajili ya uzalishaji.

Ansema kero nyingine ni upatikanaj­i wa makaa ya mawe kwa wakati kwani hali hiyo husababish­a kiwanda kushindwa kuzalisha kwa wakati kutokana na ukosefu wa malighafi hiyo.

“Kiwanda ili kifanye kazi kinahitaji makaa yam awe zaidi ya tani 21,000 kwa mwezi lakini changamoto ya miundombio­nu katika eneo la makaa yalipo husababish­a tani hizo kutozipata kwa wakati” anasema.

Anasema licha ya nia nzuri ya serikali ya kutaka makaa ya mawe yatumike, changamoto kubwa iliyopo ni usafirisha­ji pamoja na miundombin­u duni katika eneo la malighafi hiyo.

Anasema awali wakati wanaagiza makaa Afrika ya Kusini walitumia gharama ndogo tofauti na sasa ambapo wananunuli­a humuu nchini kwani sasa gharama yake imekuwa kubwa zaidi.

Hivyo anaiomba serikali kuingia ubia na kiwanda hicho ili kuhakikish­a wanaendele­za uzalishaji wake pamoja na kunusuru maisha ya watanzani ambao ni waajiri wa katika kiwanda hicho.

Itakumbukw­a kuwa hivi karibuni Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara yake mkoani Tanga ambayo ilikuwa na lengo la kutembelea miradi ambayo imeanzishw­a na wawekezaji ili kujionea maendeleo yake.

Akiwa katika kiwanda hicho aliridhia kusaidia uwekezaji wa kiwanda hicho ili kiweze kurudi katika shughuli zake kama hapo awali.

“Tunahitaji wawekezaji kuja kuwekeza katika viwanda vyetu na kujenga vipya hivyo ni jukumu la serikali kuhakikish­a linasaidia na wawekezaji katika kutatua changamoto mbalimbali” anasema.

Anasema mwekezaji huyo ameonyesha nia nzuri ya kuendelea na uwekezaji na sisi kama serikali tutahakiki­sha tunatoa fedha kumuongeze­a mwekezaji huyo kukiimaris­ha kiwanda kwa asilimia 80.

Waziri Mkuu anasema mifuko ya hifadhi ya Jamii inatakiwa kuhakikish­a wanachanga­mkia fursa ya uwekezaji iliyoko katika kiwanda hicho ili kusaidia kuinua uchumi wa nchi.

“Rais Magufuli alishatoa maelekezo kwa mifuko ya jamii kufanya uwekezaji kwenye viwanda ili michango ya wanachama iwe kati mahali salama hivyo ni imani yangu kuna mifuko itaweza kutumia fursa hiyo kufanya uwekezaji

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.