‘Majangili’ wapewa majukumu mazito Idodi

Rai - - MAONI / KATUNI - NA JIMMY CHARLES, ALIYEKUWA

MUONGO mmoja uliopita halikuwa jambo la ajabu kusikia taarifa mbalimbali zinazohusu mauaji ya Tembo yaliyokuwa yakitekelezwa na majangili.

Wanyamapori hasa Tembo na Faru walikuwa katika wakati mgumu kutokana na majangili kuzipigia hesabu zaidi pembe zao.

Ripoti ya mwaka 2015 ya African Wildlife Foundation (AWF) ilionesha kuwa kuanzia mwaka 2009 hadi 2014, Tanzania ilipoteza Tembo 65,721 kati ya Tembo 109,051 waliokuwapo.

Takwimu hizo zilimaanisha kuwa hadi kufikia mwaka 2014 Tanzania ilisaliwa na Tembo 43,330 tu, katika mbuga na hifadhi zote nchini, hali iliyokuwa inatishia uwapo wa wanyama hao kwa vizazi vijavyo.

Katika kuhakikisha Tembo na vizazi vyake vinalindwa kwa maslahi ya Taifa, Serikali ya awamu ya nne iliongeza nguvu ya kulinda tembo na wanyamapori wengine kwa kushirikiana na marafiki zake.

Mwaka 2014, mtoto wa bilionea wa Marekani Howard Buffet, Warren Buffet aliisaidia Tanzania Helkopta maalum aina ya Robertson R44 yenye thamani ya Dola za Marekani 500,000

Alipofika nchini , Howard, alikutana na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Ikulu, Dar es Salaam na kuahidi kuchangia helikopta katika kukabiliana na ujangili hususani wa tembo kwa kile alichosema ameguswa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili.

Mbali ya helikopta hiyo, Buffet pia alikusudia kusaidia vifaa vyenye thamani ya Dola za Marekani milioni tano katika kuimarisha ulinzi dhidi ya wanyamapori na uhifadhi kwa ujumla.

Jitihada hizo na hizi zinazoendelea sasa kwa kiasi kikubwa zimesaidia kukamatwa kwa idadi kubwa ya majangili na kufikishwa mahakamani na kuadhibiwa, huku wengine waliokuwa wakitumika waliamua kushirikiana na vyombo vya dola kuwafichua watu waliokuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu.

Moja ya Hifadhi zilizokuwa zikikabiliana na vita ya ujangili ni Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ni hifadhi kubwa kuliko zote nchini.

Katika kushiriki harakati za kulinda mazingira, wanyamapori na kukemea usafirishaji haramu wa wanyamapori, Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) chini ya mradi wake wa PROTECT, lilifika Hifadhi ya Taifa Ruaha.

JET ilizunguka kwenye baadhi ya vijiji vilivyoizunguka hifadhi hiyo, lengo likiwa ni kujua ni kwa namna gani jamii inashiriki kwenye mapambano dhidi ya ujangili.

Safari ya umbali wa zaidi ya Kilomita 119 kutoka Iringa mjini, iliyozongozwa na milima, miteremko mikali, matuta mengi madogomadogo barabarani, misitu minene nay a kati, madaraja na vipande vidogo vya lami iliifikisha JET kwenye Tarafa ya Idodi, ambayo inajumuisha vijiji 11, huku vijiji 10 vikipakana moja kwa moja na hifadhi hiyo.

Kiujumla hifadhi hiyo imezungukwa na vijiji 21, vinavyojumuisha Tarafa mbili za Idodi na Pawaga.

Katika tarafa ya Idodi, ndipo JET ilipobaini kuwa wapo baadhi ya watu waliokuwa wakijihusisha kwa namna moja au nyingine na ujangili, wamepewa kazi nzito ya kuwalinda wanyama.

WAMEPEWAJE KAZI HIYO?

Haikuwa rahisi kuwapa ‘majangili’ kazi hiyo ya kushiriki kuwalinda na kuwahifadhi wanyama bila kuwazuru.

Juhudi kubwa za kuwaelimisha na kuwaweka karibu na rasilimali za nchi zilifanyika ili watambue kuwa wanachokifanya si sahihi na badala yake kitawagharimu.

Miongoni mwa juhudi hizo ni hifadhi kwa kushirikiana na wadau wake kwa nia njema wamekuwa wakirejesha mapato ya hifadhi kwa wananchi kwa kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu na hata ulinzi.

Tayari hifadhi imejenga madarasa kadhaa ya shule ya msingi kwenye kijiji cha Kipera kilichopo kwenye kata ya Nzihi, Tarafa ya Kalanga ambako ndiko kulikuwa kukitajwa kuwa chanzo na maficho makubwa ya majangili.

Mbali na ujenzi huo wa madarasa, lakini pia hifadhi imeweza kujenga nyumba inayotumiwa na askari polisi kuishi katika kijiji cha Idodi.

Jitihada hizo pamoja na ushirikishwaji wa moja kwa moja wa wananchi kupitia asasi ya kiraia wa Mbomipa inayojihusisha na kulinda mazingira na wanyamapori nje ya hifadhi ya Ruaha, hatimae baadhi ya watu waliokuwa wakijihusisha na ujangili waliamua kuachana na biashara hiyo haramu hatua iliyowasogeza karibu na jamii yenye kujali rasilimali za nchi.

WAAJIRI WAO

Taasisi ya kiraia ya Ruaha Carnivore Project (RCP) yenye makazi yake katika kijiji cha Kitesa, tarafa ya Idodi mkoani Iringa, ndio imewapa jukumu hilo baadhi ya watu waliokuwa wakijihusisha na ‘ujangili.’

Wanaofanya kazi hiyo si wale waliokuwa majangili pekee. Wapo pia watu wengine ambao hawajawahi kujihusisha na shughuli hiyo, lakini wanaijua vema mipaka ya vijiji na njia za wanyama, lakini pia wapo wataalamu wa wanyamapori.

RPC ni taasisi inayojihusisha na utafiti wa wanyamapori wanaokula nyama (Carnivore), kama vile Simba, Chui, Mbwamwitu, Chui, Duma na Fisi.

Taasisi hiii imetajwa kuwa na msaada mkubwa katika vita dhidi ya ujangili, kwani pamoja na mambo mengine imekuwa karibu sana na wananchi katika huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya uhifadhi wanakijiji wengi zaidi kwa kuwachukua na kuwapeleka hifadhini ili na wao wakashuhudie utajiri wan chi.

Mbali na hilo lakini pia imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwenye eneo la Elimu, Afya na mifugo.

RCP, imetega kamera katika vijiji 16, ambavyo vimegawanywa katika makiundi manne kwa kila kundi kuwa na kamera nne.

Kazi ya kamera hizo ni kuchukua matukio yote yanayofanywa na wanyama nje ya hifadhi na kijiji kitakachofikiwa na wanyama wengi na wote wakarejea salama hifadhini kinapatiwa zawadi maalum.

Zawadi hizo zimetengwa katika makundi manne, kundi la kwanza ni mshindi ambaye anapatiwa kiasi cha Sh. milioni nne, mshiundi wa pili milioni tatu, mshindi wa tatu milioni mbili na wa mwisho sh. milioni moja.

Hata hivyo fedha hizo hazipelekwi mkononi mwa kijiji, badala yake zinaelekezwa kwenye mahitaji muhimu ya kijiji yakiegemea kwenye elimu, afya na mifugo.

Meneja wa mradi huo kutoka RCP, Benjee Cascio, alisema tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 2009 hadi sasa wamefanikiwa kushiriki katika vita dhidi ya ujangili kwa asilimia 90.

“Huko nyuma halikuwa jambo la ajabu kusikia Tembo wameuwawa kwa kiwango kikubwa, lakini sasa ni tofauti, matukio yamekuwa machache sana, tumefanikiwa kwa asilimia 90 kupambana na ujangili kwa kushirikiana na Hifadhi na wananchi wenyewe.

“Lengo la mradi wetu ni kuhakikisha tunaondoa uadui kati ya wanyama na binadamu, unajua hapa Idodi watu wengi wanamiliki mifugo na wanyamapori wanaokula nyama, hutoka hifadhini na kuvamia mazizi ya mifugo.

“Kitendo cha kuvamia mifugo ya jamii, kinasababisha watu kuchukia na kuanza kuwaua wanyama, sasa tunachokifanya sisi ni kuisaidia jamii, kujenga maboma imara ambayo hayakuwa rahisi kuvunjwa na wanyamapori, tunachofanya ni kuwaomba wachangia sh. 75,000 tu, kwa kila mwenye mifugo, gharama nyingine zote tunabeba wenyewe.

“Ujenzi wa maboma ya kisasa ni ghali sana, lakini kwa sababu sisi lengo letu ni kuhifadhi wanyama, wala haitusumbui, tunaowashirika wetu wa kimataifa wanatusaidia kufanikisha kazi hii na hata wananchi wenyewe wanafurahi,” alisema Cascio.

Kwa upande wake mtafiti msaidizi wa mradi huo, Fenrick Msigwa, alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuwabadilisha fikra wananchi wengi waliopo pembezoni mwa hifadhi.

“Sasa wanajua kuwa wanyama hawa ni mali yao na hawapaswi kuwaua, matukio yaliyosalia sasa mengi ni yale ya mtu kuua mnyama kwa ajili ya kitoweo si kutaka kuchukua pembe ama ngzo.

“Lakini pia yapo mauaji ya kawaida ya wanyama ambayo ni ya kitamaduni yanayofanywa zaidi na watu wa kabila la Barbaig, ambao hujisikia fahari kumpiga

Kitendo cha kuvamia mifugo ya jamii, kinasababisha watu kuchukia na kuanza kuwaua wanyama, sasa tunachokifanya sisi ni kuisaidia jamii, kujenga maboma imara ambayo hayakuwa rahisi kuvunjwa na wanyamapori, tunachofanya ni kuwaomba wachangia sh. 75,000 tu, kwa kila mwenye mifugo, gharama nyingine zote tunabeba wenyewe.

Makundi ya Tembo ndani ya hifadhi ya Ruaha

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.