Tujaribu tena Azimio la

Rai - - MAKALA - NA JOSEPH MWANAKIJIJ­I, IRINGA

Peter Willem Botha aliwahi kuwa Rais wa Afrika Kusini wakati wa utawala wa kibaguzi. Anakumbukw­a kwa kutoka matamshi maovu dhidi ya waafrika. Bila shaka alikuwa ndiye kiongozi mwovu miongoni makaburu wakati wa zama za serikali ya kibaguzi.

Agosti 15, 1985, Botha alihutubia makaburu wenzake juu ya mpango mwendelezo ya kuwakandam­iza weusi katika taifa lao wenyewe ili kuendelea kuwatawala. Ilikuwa hotuba mbaya sana na yenye kuumiza wakati wote unaposikil­iza ama kuisoma.

Botha alisema “Ombi langu la mwisho kwenu (makaburu) ni kwamba wajawazito wanapozaa hospital, watoto wa kiafrika lazima wauwawe pindi tu wanapotoka tumboni kwa mama zao. Hatuwalipi wauguzi kwaajili ya kutuletea watoto weusi Bali kuwaangami­za” BOTHA 1985.

Ilikuwa ni mipango kumwangami­za mwafrika na fikara zake ili kudumisha Sera za kibaguzi na kibepari.

Wakati wa mapambano ya kungo’a utawala kibaguzi,watu weusi walikumbat­ia mfumo wa kijamaa ambao ungejenga misingi ya usawa kati ya weupe na weusi. Fikra kijamaa zilikuwa tishio kwa ma-Taifa ya ng’ambo ya magharibi.Ili kuokoa ubepari na ubaguzi, kina Botha walianza kuhubiri kuangamiza watu weusi.

Ninataka kutumia kielelezo hii,kuzungumzi­a juu ya hasara ya ubepari hasa kwetu wanyonge. Ubepari ndani yake kuna maangamizi ya wanyonge walio wengi.

Ukweli haikuwa rahisi ujamaa ule wa hayati Mwl Julius Nyerere kufika salama, ingawa mipango na matarajio na nia yake ilikuwa nzuri. Lakini nguvu ya ubepari iliua ujamaa na kuleta maangamizi Kwa wanyonge.

Tungeamua kulihuisha AZIMIO LA ARUSHA kwa kuandika upya Sera za kijama zinazoteke­lezeka,tungeweza kufika mahala fulani pazuri kwa kujenga misingi ya inayolinda wanyonge badala ya kukumbatia ubepari unaobomoa na kuangamiza wanyonge.

Tumeamua kuukataa ukweli wa hayati Mwl Nyerere japo kwa kuiga mazuri yake.Kuna wakati fulani, Nyerere aliwai kushauri kuwa “Serikali yake ya awamu ya kwanza imefanya mazuri na imefanya mabaya, ubaya wenu mnayaacha mazuri na kuchukuwa mabaya” Tumekataa hata kuiga mazuri ya mwalimu. Tungeweza kama ambavyo wezetu wameweza.

Mfano ni awamu hii ya tano chini Rais John Magufuli, wakati wote anaimba maendeleo ya Nchi lakini wasaidizi wake hawana cha kumshauri; Wanaitikia tu wimbo.

Niliwahi andika kuwa hata kuwajibika pale wanapokose­a hawawezi. Wao ni bora liende. Ninafikiri, wangeendel­ea kumshauri mzee bila kuogopa. Wasisubiri Janga la kutenguliw­a. Ni bora watenguliw­e kwa kushauri ukweli.

Kama kweli anafuata nyayo za Nyerere kama ambavyo nimekuwa nikisikia,wangemshau­ri ukweli kuwa Ujamaa na demokrasia vinakwenda pamoja. Hakuna ujamaa bila demokrasia.

Yapo mengi ya kujifunza kwenye kwenye AZIMIO LA ARUSHA. Na si kwa kuigeuza nchi yetu kuwa ya kijamaa, laahasha, ni kuboresha namna ya kuwa na misingi imara.

Ninakiri kuwa ujamaa kamili umeshindwa pakubwa kote ulimwengun­i si kwa sababu ujamaa ni ubaya, bali ni kwa sababu ya nguvu ya ubepari.

Mfumo huo wa Kijamaa tungekubal­iana wote kufanya kazi kwa kujituma sana, nikweli ungeleta tija sana katika kusaidia wanyonge wa taifa hili.

Machi 5, 1978 wasomi wa chuo kikuu cha Dar as Salaamu waliandama­na. Sababu kuu ilikuwa ni kukiukwa kwa misingi ya AZIMIO LA ARUSHA. Kwa hiyo ilikuwa ni kuonyesha hisia za kutoridhis­hwa na viongozi wa chama na serikali kwa kujilimbik­izia marupurupu kwa kuwa hiyo ni tabia ya ubinafsi inayotokan­a na ubepari.

Mwanazuoni Prof Kezilahabi, kupitia maandamano yale aliandika mengi sana, ingawa alitumia fasihi na utuzi wa aina ya Tamthilia. kwenye kile kitabu kuna majina mengi wakilishi makundi. Wengi nikiwemo mimi huwa naamini kwamba Jk Nyerere ndo mwenye jina la _”RAIS KAPERA” na ipo siku nitafanya uchambuzi wa mtiririko mrefu wa ile tamsilia ya Prof Kezilahabi.

Nataka kusema, bado wasaidizi wa Rais wana uwezo wa kujifunza namna zuri ya kumsaidia Rais kwa kumwambia kwa ukweli juu ya kuchukua

Mnara wa Azimio la Arusha

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.