Arusha

Rai - - MAKALA -

mazuri ta azimio la Arusha. Wasisisubi­ri kutumbuliw­a.

Safari za madaraka kunawakati zitusaidie kuusaka ukweli wa maisha ghafi kwa wananchi na tuwe na tamaa ya kuusaka ukweli. Mwanafalsa­fa wa kale,Plato,katika kitabu chake cha “Phaedro” anadai safari imetumiwa kuwakilish­a juhudi au harakati za wanafalsaf­a kuusaka na hatimaye kuufikia ukweli ‘Ukweli wa kuwako’ (The truth of Being) na Viongozi tuwe na tamaa ya kuusaka na kuusema ukweli.

Kwahiyo tumeona kwa kiwango fulani kuwa, ujamaa umepigwa vita kali na mataifa yenye nguvu kiuchumi ili yaendelee kutunyosha au kutuingiza kwenye misukosuko.

Ghana ilikuja na kasi sana ya maendeleo Chini ya Rais na kipenzi cha Afrika Kwamme Khuruma lakini walimfanya rafiki kwa miaka michache na wakamuangu­sha kwa miaka michache kwa kuuwa soko la zao tegemeo kwa Taifa (COCOA). Maisha yalipozidi kuwa magumu mzungu hakupata taabu kuweka kibaraka wake.

Inaelezwa Nyerere alishughul­ikiwa na Shirika la Fedha ulimwenyun­i (IMF) na Benk ya Dunia akafikia uamuzi wa kung’atuka kwa heshima 1985. Tangu hapo,taifa linaendesh­wa kwa nguvu za uchumi unaopendwa na mabepari.

Ni kweli aliondoka kabla hatujamcho­ka pamoja na hali mbaya iliyokiwep­o. Kikubwa tuwe na misingi imara ya uchumi kwa ajil Taifa inayolinda wanyonge. Ni misingi ya ujamaa wa kidemokras­ia.Tujaribu kuchukua mazuri ya Azimio la Arisha. Bila hivyo, wanyonge, tutapata taabu sana.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika. 0744082522.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.