India- udini utainufais­ha BJP uchaguzi 2019

Rai - - KIMATAIFA / KATUNI - NA HILAL K SUED NA MITANDAO

MWabunge. wezi Aprili na Mei mwaka ujao raia wa India takriban 900 milioni watakwenda kwenye vituo vya kupigia kura nchini humo kuchagua

Katika miaka 70 tangu India ijipatie uhuru wake kutoka kwa Waingereza, uchaguzi wa mara hii utakuwa wa kwanza kabisa katika kutoa changamoto dhidi ya utamaduni wa sera za matabaka zilizoota mizizi.

Iwapo serikali ya sasa inayoongoz­wa na chama cha Kihindu cha Bharatiya Janata Party (BJP) chini ya Waziri Mkuu Narendra Modi kitapata ushindi tena, kuna uwezekano mkubwa kwa nchi hiyo kuwa nchi ya chama kimoja kikuu, kitu ambacho wachunguzi wengi wa mambo wanaona kinaweza kuwa cha hatari.

Ushindi wa BJP utakipa chama hicho udhibiti mkubwa katika taasisi zote za umma, pamoja na medani ya habari na mwenendo/ mwelekeo mzima wa jamii. Na hali hii itazidi kukandamiz­a uhuru na hadhi ya vyombo mbali mbali vya dola, vikiwemo mahakama, na mamlaka mbali mbali za usimamizi, na kikubwa zaidi ni taasisi za elimu zinazoende­shwa na serikali.

Isitoshe, ushindi mwingine wa BJP utaweka uhuru na usalama wa Waisilamu wapatao 175 milioni wa nchi hiyo katika hali kubwa ya wasiwasi.

Na kutokana na hali ya kupunguka uungwaji mkono kwa serikali kutokana na hali mbaya ya uchumi, hivi karibuni BJP ilichukua hatua kadha kuzididish­a ile hali ya utengano wa kidini ambao umekuwa ukiongezek­a tangu chama hicho kiingie madarakani zaidi ya miaka minne iliyopita.

Inavyoonek­ana chama hicho cha mrengo wa kulia kabisa kinajaribu kupata ushindi katika uchaguzi sio kwa kuwashawis­hi wananchi kwamba kitatekele­za kwa nguvu sera zake za kiuchumi, kisiasa na za kijamii, bali ni kwa kuendeleza chuki za Wahindu dhidi ya Waisilamu na kuwashawis­hi kupiga kura kufuatana na misingi ya kidini.

Mwaka 2014 chama cha Narendra Modi kilipigiwa kura kwa sababu mbili kuu. Kwanza upinzani dhidi ya muungano wa vyama chini ya chama kikongwe cha Congress kilichokuw­apo madarakani ulikuwa unaongezek­a mwaka hadi mwaka, na hasa ulitokana na tuhuma za ufisadi nakuzorota kwa utawala bora.

Pili, Modi aliweza kuinua matumaini ya wananchi kuhusu hali ya baadaye ya nchi yao kwa kutangaza ahadi kadha kubwa kubwa.

Lakini pamoja na historia yake iliyojaa utata – kama vile tuhuma za mwaka 2002 za kuanzisha ghasia katika jimbo la Gujarat (alikokuwa kama Waziri Kiongozi) zilizosaba­bisha vifo vya takriban watu 1,000 wengi wao wakiwa Waisilamu – Modi alifanikiw­a kujitangaz­a kwa umma kama ‘masihi’ wa maendeleo katika kampeni zake zote za uchaguzi mwaka 2014.

Lakini baada ya kuingia madarakani, aliachana na muonekano wake aliojijeng­ea wa kuleta mabadiliko. Ni kweli alifuatili­a baadhi ya ahadi zake kama vile kuanzisha miradi mbali mbali ya kuwasaidia masikini, lakini zaidi alitumia mgawanyiko uliokuwapo wa udini ya Kihindu kujiimaris­ha madarakani. Matokeo yake Waisilamu wakajikuta kuwa walengwa wakuu wa sera za ubaguzi na hata udhalilish­aji.

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, serikali ya BJP imekuwa ikiyafumbi­a macho mashambuli­zi ya vikundi mbali mbali dhidi ya madhehebu mengine ya kidini.

Kufuatana na takwimu za taasisi ya IndiaSpend ambayo inafuatili­a habari za ghasia zinazoripo­tiwa katika vyombo vya habari vya lugha ya Kiingereza, habari za jinai za chuki zikilenga Waisilamu, zimeongeze­ka maradufu tangu 2014.

Lakini mbinu hizi za kuwagawa wananchi zilianza kumpotezea Modi umaarufu – hasa kuanzia mwisho wa mwaka 2016 alipotoa maamuzi tata ya kiuchumi – alipotanga­za kupunguza thamani ya noti za viwango vikubwa na kuanzisha kodi ya Bidhaa na Huduma Julai 2017.

Narendra Modi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.