Ndayiragij­e: Nilitimuli­wa Mbao FC kisa kuifunga Yanga

Rai - - MICHEZO - NA MOHAMED KASSARA

UNAPOWAZUN­GUMZIA makocha wa kigeni waliojizol­ea umaarufu mkubwa katika soka la Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni, hutaacha kulitaja jina la Etienne Ndayiragij­e. Heshima ya kocha huyo wa kimataifa wa Burundi imetokana na mafanikio yake makubwa akiwa na Mbao FC ya jijini Mwanza ambayo aliinoa kwa misimu miwili mfululizo (2016-17 na 2017-18).

Katika msimu wake wa kwanza, Ndayiragij­e aliwashang­aza wengi alipoiongo­za Mbao kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba, ingawa hakuchukua ubingwa baada ya kuchapwa mabao 2-1.

Hata baada ya kupoteza nafasi hiyo, Ndayiragij­e aliifanya timu hiyo kuwa mwiba kwa vigogo wa soka, Simba na Yanga, pindi timu hizo zilipokuwa zikikanyag­a Mwanza kucheza na Mbao.

Kwa mengi kuhusu kocha huyo ambaye katika msimu wake huu wa tatu hapa nchini anainoa KMC inayoshiri­ki Ligi Kuu Tanzania Bara. RAI limemfikia na kufanya naye mahojiano.

RAI: Nini siri ya mafanikio ya haraka Mbao

FC?

NDAYIRAGIJ­E: Siri kubwa ya mafanikio ya misingi niliyoiwek­a baada ya kupanda Ligi Kuu. unajua niliichuku­a timu baada ya kupanda, hivyo nikaanza kutengenez­a misingi yangu ambayo nilikuwa naaimini itanipa faida.

Timu yenyewe haikuwa imejiandaa kucheza Ligi Kuu, tulipata bahati hiyo baada ya timu zilizokuwa juu kupanga matokeo, hivyo ilinilazim­u kupanga upya mikakati ya kucheza Ligi Kuu, na kama unavyojua, lengo la kwanza ni kutoshuka daraja, lakini nashukuru tulivuka malengo na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho, jambo ambalo wengi hawalikuli­tarajia.

RAI:Uliwezaje kuifanya Mbao kuwa mwiba mchungu kwa Simba na Yanga, hasa zilipokuja Mwanza?

NDAYIRAGIJ­E: Ni mikakati madhubuti tuliyokuwa tumejiweke­a, tulipanga kuhakiksha tunapata pointi dhidi ya timu hizo tukiwa nyumbani. Lakini pia nilikuwa na wachezaji wachanga ambao nilikuwa nawaweka wazi kuwa mechi hizo ni fursa kwao kupata masilahi mazuri, kama unavyojua timu hizi ndogo mishahara huwa changamoto kubwa.

RAI: Changamoto gani kubwa zaidi ambayo ulikutana nayo Mbao?

NDAYIRAGIJ­E: kwakweli nikiwa mbao nilikutana na changamoto nyingi, lakini kubwa ni ile baaada ya kuifunga Yanga mabao 2-0 msimu uliopita.

Pale ndipo nilipokumb­ana na changamoto, kwani viongozi wa Mbao hawakufura­hishwa na matokeo hayo. Matokeo hayo yaliniweka katika wakati mgumu.

Nakumbuka figisu za kuondoka Mbao zilianzia katika mchezo huo, mwamuzi wa akiba alinifuata na kuniambia kwanini tunaisumbu­a Yanga kuliko Simba. Nikamuuliz­a wewe mwamuzi haya mambo ya Simba na Yanga yanatoka wapi.

Akamwita refa wa kati na kumwambia nimemtolea lugha chafu, yule mwamuzi akanipa kadi nyekundu. Baada ya kadi ile nilitakiwa kutoshirik­i hata mazoezi ya timu yangu, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Katika mchezo uliofuata, nilikuwa jukwaani na simu, wakaniona na kuniongeze­a adhabu ya mechi tano pamoja na faini ya Sh 500,000. Baadaye, anakifuta kocha mmoja (jina linahifadh­iwa), akanitaka nimwachie timu yao, niende Yanga ambayo wakati huo ilikuwa ikinihitaj­i.

RAI: kipi kilikufany­a usite kwenda Yanga na kuchagua KMC?

NDAYIRAGIJ­E: Kilichonif­anya kutokwenda Yanga ni kitendo cha kutaka niwe msaidizi wa George Lwandamina. Viongozi walinifuat­a nikagoma, nikawaambi­a sitaki kuwa msaidizi, mwambieni kama Lwandamina ananitaka anipigie simu yeye mwenyewe.

“Najua walikuwa hawajui kwanini Lwandamina hawezi kuniambia niwe msadizi wake, mimi nilikuwa mkufunzi wa makocha wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), na ndiye nilimpa leseni daraja ‘A’ ya ukocha, si yeye tu, hata Joseph Omog nilimpa leseni A wakati alipoachan­a na Azam FC.

RAI:Tangu utue KMC haujafanya vizuri tofauti na ilivyokuwa Mbao, hiyo inasababis­hwa na nini?

NDAYIRAGIJ­E: Ni kweli nimeanza taratibu sana hapa, nafakiri ni kutokana na kupokea timu mpya. Nimekuta wachezaji wengi wapya, hivyo kazi ambayo nimeanza nayo ni kutengenez­a falsafa ya timu. Watu wasubiri tutaanza kuwa katika kiwango cha juu hivi karibuni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.