Modric alivyouzim­a ubabe wa Ronaldo, Messi Ballon d’Or

Rai - - MAKALA JAMDIEISEM­BA -

HATIMAYE ni Luka Modric aliyeweza kuumaliza utawala wa mastaa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao kwa miaka yote 10 iliyopita walikuwa wakipokeza­na tuzo ya Ballon d’Or, kila mmoja akiibeba mara tano.

Modric alitangazw­a kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka huu mwanzoni mwa wiki hii baada ya kubaki na Ronaldo na Antoine Griezmann katika orodha ya wachezaji watatu wa mwisho.

Safari hii, Messi aliishia nafasi ya tano (kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006), tena nyuma ya kinda wa kimataifa wa Ufaransa anayeichez­ea PSG, Kylian Mbappe, aliyeikami­lisha ‘top four’ ya mwaka huu.

Hakuna ubishi kuwa haikuwa kazi rahisi kwake kuinyakua tuzo hiyo Jumatatu kwani Ronaldo na Griezmann kila mmoja alikuwa na takwimu za kutisha.

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.