Hizi ndizo mechi hatari 16 bora Uefa

Rai - - MBELE - HASSAN DAUDI NA MITANDAO

MWA N Z O N I mwa wiki hii ilichezeshwa droo ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi za kwanza zikitarajiwa kuanza kuchezwa Februari, mwaka huu. Hafla ya upangaji ratiba ilifanyika mjini Nyon, Uswis, ikihusisha pia droo ya hatua ya 32 bora ya Ligi ya Europa ambapo Arsenal ilipangwa kucheza na BATE Borisov, Chelsea ikapewa Malmo, huku mechi kali zikiwa

MWANZONI mwa wiki hii ilichezeshwa droo ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi za kwanza zikitarajiwa kuanza kuchezwa Februari, mwaka huu.

Hafla ya upangaji ratiba ilifanyika mjini Nyon, Uswis, ikihusisha pia droo ya hatua ya 32 bora ya Ligi ya Europa ambapo Arsenal ilipangwa kucheza na BATE Borisov, Chelsea ikapewa Malmo, huku mechi kali zikiwa ni Celtic dhidi ya Valencia, Lazio na Sevilla, Fenerbahçe watakapomenyana na Zenit, na Galatasaray kwa Benfica.

Tukirejea Ligi yaMabingwa, Real Madrid wameangukia kwa Ajax, Manchester City wamepangiwa Schalke 04, Man United wataburuzana na PSG, Roma dhidi ya FC Porto, Tottenham watakwaruzana na Borussia Dortmund, Atletico Madrid na Juventus, Barcelona wamepewa Lyon, huku Liverpool wakiwekewa Bayern Munich.

Licha ya ugumu unaoonekana kwa mechi zote hizo, makala haya yanakuibulia mechi za kuifukuzia robo fainali zinazotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi barani Ulaya na ulimwenguni kote.

Tottenham v Dortmund

Dortmund kutoka Ujerumani inakutana na Totteham ambayo katika miaka ya hivi karibui imeonekana kuimarika, hasa katika mikimiki ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Ieleweke kuwa tishio kwa Dortmund ni kwamba Tottenham licha ya kupangiwa Barca, Inter Milan, na PSV, bado iliweza kumaliza mechi za hatua ya makundi ikiwa kileleni.

Tottenham iliweza kuichapa Inter bao 1-0 na kutoa sare ya bao 1-1 na Barca, na kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, ikizipa wakati mgumu Liverpool na Manchester City zilizo juu yake.

Ugumu wa mchezo huo ni kwamba Dortmund nao msimu huu wamecharuka, wakiwa waaongoza kweye msimamo wa Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’. Pia, walimaliza mechi za makundi wakiwa kileleni, mbele ya timu ngumu kutoka Hispania, Atletico Madrid.

Kikosi cha Dortmund kina nyota wanaoitikisa Bundesliga msimu huu na hapo utawataja Marco Reus, Paco Alcacer, Axel Witsel, beki wao wa kulia raia wa Poland, Lukasz Piszczek.

Uhondo wa mtanange huo ni kwamba Tottenham na Dormund zimekutana mara nne tu, kila moja ikiibuka na ushindi mara mbili.

Atletico v Juventus

Huo nao ni mtanange unaotazamiwa kutolewa macho na mashabiki wengi wa kandanda. Atletico inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga (Ligi Kuu ya Hispania) dhidi ya mbabe wa Serie A.

Ni vita ya Juve yenye Cristiano Ronaldo, Paolo Dybala, Giorgio Chiellini, na Leonardo Bonucci, mbele ya Atletico ya Antoine Griezmann, Diego Costa, Diego Godin, na Saul Niguez, wanaotamba La Liga kwa sasa.

Juve wamecheza mara mbili fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kipindi kifupi tu cha miaka minne iliyopita, na hiyo ni kabla ya kukiongezea nguvu kikosi chao kwa ujio wa Ronaldo.

Lakini je, unafikiri itakuwa rahisi kutinga robo fainali mbele ya Atletico inayosifika kwa uimara wa safu yake ya ulinzi chini ya kocha wa kimataifa wa Argentina, Diego Simeone? Patachimbika.

Timu hizo zimeshawahi kuvaana mara saba, mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya na zilizobaki Ligi ya Europa.

Kwa ujumla wake, Atletico wameshinda mbili, wamepoteza nne, na michezo iliyobaki ikimalizika kwa wababe hao wa Hispania na Italia kushindwa kufungana.

Liverpool v Bayern

Bayern wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Bundesliga lakini linapokuja suala la Ligi ya Mabingwa Ulaya kuna stori tofauti kidogo kwani walimaliza mechi za hatua ya makundi wakiwa kileleni licha ya kundi lao kuwa na timu zisizotabirika za Ajax na Benfica.

Wababe hao mara tano mfululizo wa Bundesliga wanatambia uwepo wa mastaa wake, Franck Ribery, Arjen Robben, na Robert Lewandowski wanaoiongoza safu ya ushambuliaji.

Hata hivyo, kinachoupa mchezo huo mvuto wa kipekee ni kwamba hawana safu yao ya ulinzi si ya kuaminika sana, hivyo inatabiriwa kuwa na wakati mgumu mbele ya Mohamed Salah, Xherdan Shaqiri, na Sadio Mane.

Kama walivyo Bayern, Liver nao ni mabingwa mara tano wa michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo ni mchezo utakaovikutanisha vigogo wenye historia kubwa.

Ukiacha mchezo wao ujao wa Februari, mwakani, ni mechi saba pekee zimeshawahi kuzikutanisha timu hizo, Liver ikishinda mbili, sare nne, na Bayern wakiambulia ushindi mara moja.

Kikosi cha Liverpool

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.