HAILE SELAISE NA DHANA YA UJIO WA PILI WA YESU

Rai - - MBELE - NA NDATAMA HASSAN

Watu wengi wamekuwa wakiwaona marasta pasipo kuwafahamu kiundani wao ni nani. Wapo wanaoamini kila aliye na misokoto ya nywele kichwani ni Rasta mpaka kufikia aina hizo za nywele kuitwa Rasta. Naomba leo ifahamike ‘Dreadlocks’ kichwani haimaanishi mtu ni Rasta na sio kila Rasta ana ‘dreadlocks’ kichwani.

Rastafarian ni Imani (Dini) ya ki Abrahamic. (Dini za Abrahamic ni dini zinazoamini katika kizazi cha Ibrahim) iliyoendelezwa Jamaica miaka ya 1930. Wasomi huiita dini mpya wengine huiita harakati za kijamaa/Kijamii.

Neno Rastafar limetokana na majina ya Haile selassie. Ras ikiwa ni cheo chake na Far imetokana na jina lake kamili Tofar Makonen.

Rasta wanaamini Haile Selaise ni ujio wa pili wa Yesu na ni chaguo la Mungu. Wao huamini Haile Selaise anamuwakilisha Mungu duniani.

Salamu ya Marasta ni moja nayo ni peace and love (Amani na upendo).

Mtoto anapozaliwa katika familia ya kirasta hubarikiwa na wazee ndani ya jamii katika kipindi cha Ibada au sherehe za ki Nayahbing.

Rastas hawaamini katika kufa (Rasta never die) wao huamini watenda dhambi pekee ndio hufa. Rasta roho huacha mwili na kwenda sehemu salama huku mwili ukibaki kurutubisha ardhi.

Rasta wanaamini wafu huzikana ‘book of wisdom’ . Hivyo Rasta huwa haziki wala hana msiba. Na moja ya sheria zake ukishika maiti unatakiwa unyowe nywele kwa muda wa miaka saba.

Rasta wana miiko mikuu miwili. 1. Mpende Mungu 2. Mpende jirani yako Rasta wanaamini mwanamke ni kiumbe aliyezaliwa kumuhudumia mwanaume. Wanawake wa Kirasta hujistiri kwa mavazi marefu yanayofunika vichwa vyao na mwili mzima.

Rasta wa kiume wanaruhusiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa kitu ambacho wanawake hawaruhusiwi. Mwanamke wa kirasta anatarajiwa kumuhudumia mumewe tu.

Rasta hawana ndoa za kisheria ingawa wapo wengi wenye ndoa za kisheria pia. Rasta wa kiume humwita mkewe Malkia huku rasta wa kike humwita mumewe Mfalme.

Bangi ni dawa kuu duniani kwa imani ya kirasta. Vile vile huitumia wakati wa sherehe na kuabudu kwa kuamini huwafanya kuwa karibu na Mungu. Matumizi ya Bangi kwa marasta yanapewa nguvu na baadhi ya maandiko kwenye Biblia kama vile Mwanzo 1:29, Zaburi 18.8 na Ufunuo 22:2.

Rasta huamini umimi ni dhambi hivyo binadamu wote ni sawa, kufanya hili sheria hutumia neno *I and I* wakimaanisha sisi.

Mfano wa maneno hayo ni I ikimaanisha Mimi I and I ikimaanisha sisi I- Ceive- receive I- sire- desire I- Rate- create I- Men Amen Overstand ikimaanisha understand.

Rasta ni imani yenye vikundi vingi ndani yake kama isemavyo biblia *Yohana 14:2*. I. Bobo Ashanti II. 12 Tribes of Israel III. Nyahbing Tutaendelea kuchambua sababu ya kufuga Rasta na mengine mengi usiyoyajua kwenye Imani hii.

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa simu namba 0788029033

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.