KIMATAIFA: DUNIA YAINGIA KWENYE VITA YA MIAMALA YA FEDHA TASLIM

Rai - - MBELE - NA HILAL K SUED NA MITANDAO

Wakati ambapo kila mbonyezo wa kibodi (keyboard) unakuwa sehemu ya kumbukumbu mtu isiyofutika, wakati ambapo vifaa vyote vya ki-electroniki vinafuatilia kila jambo mtu analolifanya, uwezo wa kufanya malipo kwa pesa taslim kupitia muamala wa kifedha ndiyo unabakia njia pekee isiyoweka kumbukumbu yoyote ambayo mtu anaweza kufanya.

Labda iwapo muamala huo umerekodiwa kupitia kamera za usalama (CCTV) zilizowekwa kwenye eneo husika. Lakini pia dalili ziko kila mahali kwamba ‘uhuru’ hu wa mwisho nao oia umedhamiriwa kutokomezwa, kwani siku hizi njia zote zinaelekea kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa ambao kila manunuzi na mauzo, kuanzia majumba ya maghorofa hadi peremende, yanarekodiwa ndani ya historia ya kila binadamu kwa njia ya kielektroniki.

Kenneth Rogoff, mwanauchumi aliyebobea wa Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani na aliyewahi kuwa Mchumi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) amesema sasa dunia imeanza kufikia mahali ambapo hakuna muamala ambao hautajulikana na mamlaka za kodi au mamlaka zingine za serikali.

Rogof ambaye anahusishwa katika andiko lake moja kuhusu faida na hasara za kuondoa kabisa fedha za makaratasi (noti) anasema noti zinasaidia kuifanya miamala kuwa siri, na hivyo kusaidia kuificha miamala hiyo kwa serikali, hivyo kusaidia katika ukwepaji kodi na malipo mengine.

Na katika fedha za noti, zile zenye viwango vikubwa ndiyo hupendelewa kutumika katika miamala ya namna hii. Kwa mfano, huko Marekani, asilimia 78 ya fedha zote zilizo kwenye mzunguko ni noti na dola mia mia. Na vivyo hivyo kwa noti za Euro kuhusu nchi za Umoja wa Ulaya na Yen kwa Japan.

Noti hizi za viwango vikubwa kupendelewa katika miamala ya wahalifu kama vile katika biashara ya dawa za kulevya, ukwepaji wa kodi na kutakatisha fedha ndiko kumeibua hoja kubwa ya kuachana nazo na badala yake miamala ya kielektroniki.

Rogoff si peke yake kupendekeza kuachana na matumizi ya pesa za karatasi. Wachumi wengine, kama vile waziri wa fedha wa zamani wa Marekani Lawrence Summers pia anapinga matumizi ya fedha za karatasi.

Summers anasema fedha taslimu zinapaswa kuwa historia, kwani faragha (privacy) ndiyo adui mkubwa kwa mamlaka za serikali katika kupambana na uhalifu wa miamala – na hivyo kufanya uthibiti kuwa mgumu.

Lakini kwa Marekani, falsafa yenyewe ya uwepo wa jamii isiyotumia pesa taslim ni ukiukwaji wa Marekebisho ya Nne (Fourth Amendment) ya Katiba ya nchi hiyo. Hii ni kwa sababu itakuwa vigumu kupata tafsiri halisi ya ‘ukaguzi’ ili kuwa na uhakika wa uwepo wa miamala yote ya mtu binafsi. Yaani muamala wa kielektroniki hautakuwa na maana, au thamani yoyote kwa wakaguzi/ wapelelezi wa serikali. Matumizi ya Bitcoin Halafu sasa hivi kumeibuka matumizi ya aina ya pesa – cryptocurrency, kwa mfano Bitcoin, nje ya mifumo ya benki kuu za nchi mbali mbali, fedha inayotumia teknolojia iitwayo blockchain. Miamala ya mfumo huu unafichwa (encrypted) ili kwamba kinadharia utambulisho wa mtu husika unakuwa haujulikani.

Bitcoin, kwa mfano ilianzishwa mwaka 2009 na watu wasiojulikana ila kwa jina la bandia la “Satoshi Nakamoto”. Bitcoin imetokea kuwa maarufu sana sasa hivi ingawa kuna aina nyingine ya mifumo hiyo iliyoanzishwa. Kama ilivyotajwa hapo mbele, mifumo ya fedha aina ya Bitcoin iko nje ya mifumo ya benki kuu za nchi mbali mbali. Aidha umiliki wa Bitcoin unatambulishwa siyo kwa majina, bali ni kwa anuani tu.

Hata hivyo inadaiwa ile dhana ya kwamba hakuna mamlaka zinazoweza kuhusisha anuani ya Bitcoin kwa mtu halisi haina nguvu sana kwani inadaiwa sasa hivi mamlaka ya mapato nchini Marekani (IRS) kwa mfano sasa hivi imeanza kutumia ‘software’ in ayofuatilia utambulisho wa watu wanaomiliki Bitcoin.

Waziri wa Fedha wa zamani wa Marekani Lawrence Summers.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.