ATCL chungu kwa vigogo

» Wasomi wawachongea zaidi kwa JPM » Wapendekeza waletwe wataalamu kutoka nje

Rai - - MBELE -

Kwa sababu ni hela ya walipa kodi, na wanaturudisha zamani tulikotoka… nadhani hata agizo la rais kuwa warudishe hizo fedha kutoka kwenye mishahara yao haitoshi, ingetakiwa iende na barua ya onyo.

Wale wasiosoma [na kujifunza kutokana na] historia, wanakabiliwa na janga la kuiingia d`unia kichwa kichwa na kwa madhara makubwa; wale wanaoshindwa kujifunza kutokana na mema au makosa ya watangulizi wao, wanakabiliwa na janga la kurudia makosa ya zamani”.

Haya ni maneno ya kihekima ya Mwanafalsafa wa zama zetu, George Santayana, katika kitabu chake “Life of Reason” akiwatahadharisha watawala juu ya hatari ya kubeza historia ya Mataifa yao. Nasi kwa madhumuni ya makala haya tunaongezea kwa kusema, “Wale wasiothamini utamaduni wa Mataifa yao na masaibu unayopitia, hawafai kuongoza umma”.

Tanzania na Korea Kaskazini zilianzisha harakati za kusaka maendeleo kwa kujenga Ujamaa mwaka mmoja, 1967 kwa azima na mazingira yanayofanana. Leo, Tanzania bado ni moja kati ya nchi masikini sana duniani [LDC], wakati Korea Kaskazini inaingia katika kundi la nchi za dunia ya kwanza na ni tishio duniani kijeshi. Wapi tulikosea na kuzidi kubaki nyuma?

Ukiondoa dhana ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, hakuna dhana nyingine iliyotuchukulia muda na fikra nyingi katika kipindi cha miaka 52 ya Uhuru kama dhana ya Ujamaa na Kujitegemea. Hadi leo tungali tunaimba “Ujamaa” wakati tukicheza ngoma ya kibepari

Misingi ya utekelezaji wa “Ujamaa” imefafanuliwa vyema katika Azimio la Arusha. Madhumuni ya Azimio hilo, yanashinda ukinzani wowote, kama linavyosema kwa kifupi: “Tumeonewa vya kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Ni unyonge wetu ambao umefanya tuonewe, tunyonywe na tupuuzwe. Sasa tunataka Mapinduzi kuondoa unyonge wetu, ili tusinyonywe, kuonewa au kunyanyaswa tena”.

Madhumuni haya yalivuma kwa umaarufu dunia nzima, si kwa sababu yalikuwa ya kipekee na ya aina yake, bali ni kwa jinsi ambavyo yalipaswa kutekelezwa. Lakini kwa nchi masikini kama Tanzania yenye uchumi unaotegemea nguvu ya soko la nje, jaribio lolote la kutaka kujitegemea lilivuta hisia tofauti na mshangao wa dunia kiasi cha Watanzania kuonekana kama “wendawazimu”, kwa kuthubutu kufanya lisilowezekana.

Ilivyoonekana ni kwamba, kulikuwa na kutoelewana pamoja na ukinzani kwa kiwango kikubwa ndani ya Uongozi wa nchi, juu ya na maana halisi ya “kujitegemea” na kusababisha zoezi zima kugeuka ajali ambayo haikutarajiwa.

Ukinzani mkubwa ulikuwa juu ya njia sahihi ya maendeleo ndani ya Uongozi wa Serikali, kati ya wale wa kambi iliyotetea mfumo wa kibepari [Rightists] na kambi ya Kijamaa [Leftists], ambapo kambi ya Kibepari iliwakilisha fikra za “Usasa” [modernization] ambazo ndizo zilizotawala wakati huo. Na Kambi ya Kijamaa, ya “ukale”, iliwakilisha mshikamano, umoja na upendo kwa misingi ya “ujima”.

Mhimili mkuu wa fikra za “kimodenaizesheni” ulikuwa kwanza, ni kuanzisha mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka nje; na pili, kuhamasisha na kuimarisha uuzaji wa mazao ghafi nchi za nje. Kwa kambi hii, wazo la kujitegemea lilionekana la kihayawani, lisilowezekana au kutekelezeka. Na kwa sababu hiyo, kwao Azimio la Arusha lilikuwa kichekesho na mzaha wenye hatari kubwa.

Kwa kambi ya Kijamaa, Azimio la Arusha lilipokewa kwa shangwe, nderemo na vifijo na kuwa sera rasmi ya “Ujamaa na kujitegemea” kama mwanzo mzuri wa safari ndefu kuelekea kwenye maendeleo ya uchumi wa kitaifa unaojitegemea kwa manufaa ya wote.

Mvutano wa kambi hizi mbili ulikuwa mkali na mkubwa kiasi cha kupunguza mwendo kuelekea kwenye nchi ya ahadi, “Kanaani” ya Tanzania [Ujamaa], lakini kwa mateso tele “jangwani”. Na pale Nyerere alipoombwa kugeuka nyuma kutazama tulikotoka ili kuona tuendako kwa lengo la kujirekebisha, alisema asingethubutu kufanya hivyo kwa hofu ya “kugeuka jiwe”, mithili ya mke wa Luthu wa Biblia.

Vuguvugu na mirindimo ya kambi ya “Ujamaa” ilikuwa mikubwa na yenye ushawishi mkubwa kiasi kwamba Nyerere, ambaye sasa alikuwa amechukua msimamo thabiti kwa kuihama kambi ya Kibepari taratibu na kwa uangalifu mkubwa, alifika mahali “jangwani” akakataa kwenda kushoto zaidi [ujamaa] wala kwenda kulia [ubepari], akabakia njia panda.

Hatua yake hiyo ya makosa na upopo, haikuweza kutoa suluhu kwa kambi hizi kinzani zilizokuwa zikiendelea kutafunana na kuhujumiana kimya kimya, kwa adha kubwa kwa Umma. Na kwa kufanya hivyo, haikumaanisha kwamba Mwalimu alikubali “kugeuka jiwe”, kwani harakati za mapambano ya “Ujamaa” usio wa kisayansi ziliendelea.

Pengine kwa kuhofu ambacho kingetokea, Mwalimu alicheza vizuri karata zake kupata jibu la fumbo la ukinzani huo, huku akielewa kwamba sehemu kubwa ya jamii ilimuunga mkono; lakini wakati huo huo moto wa kambi ya kibepari ukiwaka na kutoa tishio lisiloweza kupuuzwa. Kambi ya Kibepari ilihofu Mapinduzi ya Wakulima na Wafanyakazi kama yale ya Oktoba, 1719 nchini Urusi, kutokea.

Aliona jibu lilifichika katikati ya “Ubepari” na “Ujamaa”; hivyo aliamua kuunganisha mawazo ya pande zote mbili, ndani ya mfumo wa “Ujamaa”, na kuzaliwa kile alichokiita “Sera ya Mapinduzi kwa njia ya mageuko” [A policy of Revolution by Evolution] ili kuleta suluhu kwa ukinzani uliotishia kuleta mpasuko wa kisiasa nchini.

Wakati kambi ya ubepari iliona “kujitegemea” ilikuwa ndoto ya “mwendawazimu”, kwa kambi ya “Ujamaa” “kujitegemea” kulimaanisha kujitegemea kwa misingi ya kijadi kwa kuifanyia marekebisho ya hapa na pale, tofauti na dhana ya kujenga ubepari kwanza ili kufikia Ujamaa.

Na huo ndio mtizamo wa watetezi wa dhana ya “teknolojia ya kati” [intermediate technology] ya kina Profesa Rene Dumont; na wa itikadi ya “Maendeleo Vijijini”. Ukweli, kitabu cha Rene Dumont, “Afrika inakwenda Kombo” [False Start in Africa], kilifanywa dira ya maendeleo kwa Tanzania ambapo kila Waziri na Msomi yeyote mwenye madaraka, alitakiwa awe nacho na kukisoma.

Kambi ya Ujamaa, wa Kisayansi ilitafsiri “Kujitegemea” kama sera ya kuuondoa taratibu uchumi wetu kutoka kwenye udhibiti wa masoko ya nchi zilizoendelea. Ilitetea kujitegemea kwa chakula na kuzalisha kingi kwa kuuza nje kwa njia ya kubadilishana bidhaa [Barter Trade] na nchi za Kisoshalisti ili kutuwezesha kuanzisha Viwanda vya msingi kama vya chuma, makaa ya mawe na Viwanda vya kutengeneza vipuri; viwanda vya kati kama vile vya nguo, kusindika vyakula; na mwisho, kuanzisha mashamba makubwa ya Serikali na kuboresha kilimo ili kuwatoa wakulima kutoka kilimo cha mtu mdogo kufikia kilimo cha mashamba makubwa kwa njia ya kisayansi, kwa maana ya “Mapinduzi ya Kijani”.Profesa Abdulrahman Babu, aliyewahi kuwa Waziri wa Uchumi, Mipango na Maendeleo nchini, alikuwa wa kambi hii.

Sasa ni dhahiri kwamba, kama msimamo wa kambi ya Ujamaa wa Kisayansi, ungezingatiwa, badala ya Ujamaa wa kiujima, bila ya shaka tungepiga hatua kubwa kimaendeleo kama ilivyo Korea Kaskazini leo, na kuacha kuwa Taifa “omba omba” kama tulivyo sasa. Korea Kaskazini ilichukua mkondo huu na imefanikiwa kama ambavyo tu China ilivyoanza na kusonga mbele chini ya sera ya “The Great Leap Forward” – Mruko Mkuu kwenda Mbele, mwaka 1948.

Sasa tuangalie kwa kifupi mitazamo ya kambi hizi mbili kinzani kuona jinsi ziolivyoathiri nafasi ya maendeleo kwa nchi na sera nzima ya Ujamaa na kujitegemea. Mtizamo wa kambi ya ubepari nchini ulishabihiana na nadharia ya “Modenaizesheni” ya nchi za Kibepari za Magharibi kwa kuziona nchi zinazoendelea kuwa zimebanwa katika kile kinachoitwa “mzingo hatari wa umasikini” [Vicious Circle of Poverty] ambamo haziwezi kujinasua ila kwa kusaidiwa tu na nguvu kutoka nje, hasa kutoka nchi za Magharibi. Na kwa ujinga wetu tumekubali kuamini hivyo.

Kwa mujibu wa mtizamo huu, nchi zetu ni masikini kwa sababu zinakosa mitaji, na hivyo kukosa uwezo wa kuendeleza rasilimali za kuzalisha ziada inayoweza kugeuzwa kuwa mtaji. Na kwa sababu hiyo, eti zinataka tukiri kuwa “sisi ni masikini kwa sababu tu masikini”. Na eti kwamba, ili ziweze kujinasua kutoka katika mzunguko wa umasikini huo, nchi masikini hazina budi kukaribisha uwekezaji ili mtaji huo usaidie kuamsha rasilimali zilizosinzia.

Nadharia hii inataka kuwekwa masharti na mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji, na kwa kuomba misaada kutoka Serikalini na Mashirika ya Kimataifa kama vile Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa [IMF] ili kujenga miundombinu ya kijamii na kiuchumi kwa lengo la kuwapunguzia wawekezaji gharama za uwekezaji waweze kuvuna faida kubwa kwa mitaji yao na bila ya kubughudhiwa.

Tulidanganywa kwa njia hii kwamba, uchumi wetu ungeweza kuzalisha utajiri, na kudondosha matone ya “mvua ya neema” na kupunguza kiu kwa mafukara; na kuwa eti uchumi huo ungeweza kukata minyororo ya umasikini na kuwa uchumi ulioendelea, wa kula na kusaza kama zilivyo nchi tajiri za Ulaya, Japani na Amerika ya Kaskazini. Na hivi ndivyo tunavyojaribu kuaminishwa hadi leo na mawakala wa ubepari wa kimataifa hapa nchini, kutufanya kufurahia kutembeza bakuli la “ombaomba”.

Wakulima wakilima pamoja

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.