Hivi ndivyo benki za Kiisilamu zinavyofanya kazi bila riba

Rai - - MBELE - NA AMANA ABDALLAH

Haijalishi sana iwapo huduma za benki zinazotolewa ni zile zinazofuata misingi za Kiisilamu au zile za kawaida,

lakini malengo makuu ya mabenki yote yanabakia yale yale – kuhamasisha uhamishaji wa fedha za ziada kutoka kwa

Haijalishi sana iwapo huduma za benki zinazotolewa ni zile zinazofuata misingi za Kiisilamu au zile za kawaida, lakini malengo makuu ya mabenki yote yanabakia yale yale – kuhamasisha uhamishaji wa fedha za ziada kutoka kwa watu walizo nazo ili kuziweka katika benki (deposits) na pia kuzihamisha kwenda kwa watu wengine

ambao wanazihitaji kwa ajili ya shughuli zao mbali mbali.

Mchakato huu wa mabenki wa kukutanisha watu wenye fedha na wale wenye mahitaji ya fedha kwa shughuli zao mbali mbali huwezesha mnabenki kuwa chombo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.

Lakini tofauti na shughuli za mabenki ya kawawaida, mabenki ya Kiisilamu hufanya kazi kufuatana na misingi ya Shariah – na hufanya hivyo kupitia mifumo mikuu kama sita hivi - Murabahah, Mudarabah, Musharaka, Ijara, Salam, na Istisnah.

Hapa Tanzania miongoni mwa mabenki ambayo yana vitengo vinavyotoa huduma za kifedha kufuata misingi ya Shariah ni pamoja na Amana Bank, People’s Bank of Zanzibar (PBZ), NBC na Kenya Commercial Bank (KBC).

Uchaguzi wa mfumo ambao mteja anauhitaji hutegemea sheria zinazosimamiwa na mamlaka husika za kila nchi (regulatory bodies) pamoja na sheria mama zinaziosimamia huduma za kifedha za Kiisilamu (Islamic finance).

Hata hivyo mifumo hii imebuniwa ili kuhakikisha kwamba haina kitu chochote ndani yake kinachoweza kuitwa riba, kitu ambacho kinakiuka misingi ya huduma za kifedha za mabenki ya Kiisilamu, na pia njia hizi lazima zitii matakwa ya Shariah.

Lengo kuu la makala hii ni kuangalia iwapo mabenki yanayotoa huduma za Kiisilamu hufanya kazi kwa umahiri ipasavyo na iwapo mabenki hayo yanaweza kushindana na yale mabenki mengine ya kawaida hasa katika ulimwengu huu wa sasa wa masoko ya kiutandawazi.

Makala hii pia itajaribu kubaini wahusika wakubwa katika tasnia nzima ya huduma za mabenki ya Kiisilamu kwa wakati huu na watu gani ambao wanaweza kushawishika katika huduma hizo hapo baadaye.

Murabahah ni njia ya kale kuliko zote katika huduma za biashara ya mikataba iliyokuwa ukitumika hata kabla ya kuja kwa Uisilamu. Kwa maana yake rahisi kabisa Murabahah ni uuzaji wa kitu chochote kwa bei ambayo mwuuzaji alinunulia kitu hicho na nyongeza kidogo ya fedha kama faida.

Sharti la lazima la Murabahah katika shughuli za mabenki ya Kiisilamu ni kwamba mnunuzi na muuzaji lazima wawe na ufahamu wa bei ya awali ya kitu husika ambacho kinatakiwa kiuzwe tena ama kwa njia ya papo kwa papo au hata kwa njia ya kulipa baadaye – yaani kwa mkopo.

Muamala wa Murabahah unahusisha mfanyabiashara (yaani mteja wa Benki ya Kiisuilamu) ambaye huenda kwa taasisi ya fedha na kutoa agizo kwa benki hiyo ya Kiisilamu kununua bidhaa kwa niaba yake.

Baada ya mchanganuo na kujiridhisha hasa kuhusu athari (risk), Benki hiyo ya Kiisilamu hununua bidhaa hizo kwanza kwa jina lake (benki) – yaani kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnununzi – yaani hiyo benki ya Kiisilamu.

Baada ya kutwaa umiliki wa bidhaa husika, Benki hiyo ya Kiisilamu huuza bidhaa hizo kwa mteja kwa bei itakayokubaliwa na pande zote hizo mbili – kwa njia ya papo kwa papo au kwa mkopo.

Wanazuo wengi wa Kiisilamu na Maulamaa wengine wa dini wanaunga mkono njia ya Murabahah kwani haina chembe chembe za riba. Uhalali wa Mrabahaha kutobeba chembe chembe za riba unatokana na na matakwa ya misingi ya sheria za Kiisilamu – yaani Shariah – ya kutokuwepo kwa riba.

Maana yake ni kwamba kwa faida yoyote ile inayohitajika, mhusika lazima ashirikishwe katika athari (risk) inayotokana na muamala husika.

Aidha, hii inatokana na Shariah (Qurani na Sunna) – yaani ni pale ambapo Allah ameruhusu biashara na kukataza riba (Quran 2:275). Na mbali na hili, njia hii pia huridhia mikataba ya mauzo katika huduma za Kibenki za Kiisilamu ambapo muuzaji lazima awe na umiliki wa bidhaa anayotaka kuuza pamoja na athari (risk) zitokanazo.

Kutumia njia hii ya Murabahah hufanikisha kuzifanya benki za Kiisilamu kutii matakwa ya Shariah, kwani mabenki hayo hupata faida zake kutokana na faida inayozalishwa kutoka kwa uuzaji wa bidhaa.

Msingi huu wa Mabenki ya Kiisilamu wa kwanza kuchukua umiliki wa bidhaa kwa jina lake mara moja huifanya benki hiyo kuwa katika athari (risk) itokanayo na bidhaa hiyo – kama vile bidhaa kupotea au kuharibika, vitu ambavyo mchuuzi hatahusika navyo kamwe.

Hatua ya Benki ya Kiisilamu kubeba athari kuhusu bidhaa ndicho kinaifanya benki hiyo kuchukua fedha za ziada kama zilivyokubaliwa kutoka kwa mfanya biashara ambaye kwa hiari yake huzilipa, zaidi ya bei ya awali iliyotumika kununulia bidhaa.

Tofauti na mabenki ya kawaida ambayo hutoza riba kwa fedha zinazokopeshwa kwa wachuuzi ambao hawana kauli yoyote kuhusu viwango vya riba vilivyowekwa, mabenki ya Kiisilamu hukubaliana na wafanya biashara kuhusu kiwango cha faida (profit margin) ambayo hupatikana kutokana na fedha za ziada zinazolipwa na mfanya biashara juu ya bei ya awali ya bidhaa. Kiwango kinacholipwa hakibadiliki kama vile katika huduma za mabenki ya kawaida kinachotokana na kubadilika kwa viwango vya riba.

Isitoshe mfumo wa benki za Kiisilamu kukumbatia mali halisi katika huduma za kibenki zinazotolewa kwa wafanya biashara hutoa ubora zaidi kuliko ile mifumo ya kibenki za kawaida.

Hata hivyo, mfumo wa Murabahah katika huduma za mabenki ya Kiisilamu hauhalalishwi kubadilisha tu jina ‘riba’ na kuwa ‘faida’. Kitu cha lazima hapa kimo katika masharti yaliyoorodheshwa ndani ya misingi ya Shariah.

Hivyo basi kutokana na misingi yake ya uendeshaji, siyo tu kwamba mabenki ya kiisilamu yanaweza kufanya kazi bila ya kutoza riba, lakini pia yanaweza yakawa mabenki yanayoaminika.

Lengo kuu la makala hii ni kuangalia iwapo mabenki yanayotoa huduma za Kiisilamu hufanya kazi kwa umahiri ipasavyo na iwapo mabenki hayo yanaweza kushindana na yale mabenki mengine ya kawaida hasa katika ulimwengu huu wa sasa wa masoko ya kiutandawazi.

Wafanyabiashara hupatiwa mikopo isiyo na riba

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.