Hoja ya Nkamia itakavyopita na hofu ya CCM mpya

Rai - - KUTOKA MTANDAONI - Heri ya Mwaka Mpya 2019. Ole Mushi 0712702602

Labda Rais tu aamue kutokukubali hoja ya miaka saba ya Juma Nkamia isipite. Vinginevyo hakuna wa kuizuia na hapa tujiandae tu kwenye uchaguzi wa 2022.

Kumbukeni kwamba si kwamba hoja hii imebeba tu maslahi ya Rais bali imebeba maslahi ya wabunge wenyewe. Kama ikipita ina maana wabunge wamejiongezea miaka miwili ya kuongoza majimbo yao.

Ni mbunge gani toka upinzani au CCM ambaye hataki kulipwa mishahara na marupurupu ya kibunge kwa miaka miwili zaidi? Kwa maana hiyo kama hoja hii ikipita mbunge uliyenaye atakuwa mbunge wako hadi 2022. HESABU Kama hoja hii itaamuliwa kwa kura ndani ya bunge na kura hiyo ikawa ni ya siri hoja hii itapitishwa kwa asilimia zaidi ya 90.

Kura za kwanza kabisa za ndio zitatoka kwa wabunge wa viti maalumu ambao hawaijui kesho yao kama watachaguliwa tena au hawatachaguliwa tena katika uchaguzi ujao. Tukumbuke idadi ya wabunge wa viti maalumu huamuliwa kwa idadi ya wabunge na kura za rais chama husika kitakachopata katika uchaguzi mkuu. Nani anayejua kama CCM au UKAWA itapata wabunge wengi au kura nyingi za kuwarudisha wabunge hawa wa viti maalumu bungeni ? Kwa kuwa hawana uhakika huo hoja ya Nkamia hadi sasa ina kura za Ndio za wabunge wa viti maalum 113.

Hizi za CCM za wabunge wa majimbo sina shaka nazo hizo zipo zote 188 ukichanganya na hizi za viti maalumu unapata 231.

Chukua kura zote za wabunge wa kuteuliwa na Rais mpaka sasa wapo 9 jumla yake inafika 240.

Kura hizo zinatosha kabisa nimekuachia kura zote za wabunge wa CUF na CHADEMA za majimbo ambazo hazifiki hata 80. Na hizi nazo zitapigwa kwa kutafakari hali aliyonayo mbunge huyo jimboni kwake.

Hesabu hizi nimezipiga kabla ya kina Mtolea hawajahama. HOFU YA CCM MPYA Kuna wakati niliwahi kusema kuwa ili mtu awe rais wa nchi lazma awe amejiandaa au ameaandalia. Hii nikiwa na maana kuwa ni lazma mtu huyo awe amejitambulisha kwa jamii vya kutosha na jamii inamjua.

Mfano kilichoturahisishia kazi sisi kwenye kampeni za 2015 ni umaarufu aliokuwa nao Magufuli, ni kazi zake zilimtambulisha, nani aliyekuwa hajui kazi za Magufuli kabla ya kuwa Rais?

Kila wizara aliyopangwa aliifanyia mageuzi na akatambulika haswa. Alikuwa ana uwezo wa kusomamia sheria hata kama mkubwa wake wa kazi alikuwa anataka kuitengua Sheria hiyo kinyemela. Aliwahi kusuguana na Waziri mkuu kisa uzito wa Malori lakini yeye alikuwa sahihi kabisa.

Angalia hii; kipindi cha nyuma si yeye tu aliyekuwa ni Presidential Material. Kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wameshajitambulisha ndio maana 2015 walijitokeza zaidi ya watu 40 na kila mtu aliyejitokeza alikuwa akionekana tishio.

Tafsiri yake ni kwamba ndani ya CCM kwa kutumia tu viongozi waliokuwepo tulikuwa tuna hazina ya watu wengi ambao wangeliweza lupeperusha Bendera ya CCM.

Najiuliza; kesho tutaanza mwaka wa nne katika awamu hii ya tano, ukiangalia mawaziri ambao walianza na awamu hii wamebakia wachache sana. Wale vijana ambao walitakiwa wapate malezi kwa ajili ya kuja kupeperusha bendera yetu huko siku za usoni nao walishaondoka na waliobaki hawaonekani wakifanya kazi zinazoweza kujitambulisha.

Kwa mbali nilimuona Waziri Mkuu akijaribu 2016, na 2017 mwanzoni, lakini siku hizi maamuzi mengi yanamruka yanafika hadi Ikulu. Mfano swala la korosho na hata hili la kikokotoleo lingepaswa kuishia kwake ili apate Credit na limjenge.

Juzi nilisema kuwa kila tatizo sasa hivi wananchi wakilipata wanalikimbizia kwa Rais ina maana huku chini hakuna uwezo wa kutatua au wanaogopa kukosea kwenye kufanya maamuzi.

Hili ni tatizo la kimfumo na ndipo hofu inapoanzia. Lazma turuhusu sasa mifumo yetu ifanye kazi ili talenti za watu zionekane kwa maslahi ya chama ya baadaye.

Kama ni timu tumeitengeneza kumzunguka mtu mmoja, yaani hakuna mtu mwingine anayeweza kufunga. Pasi zote za mwisho zinakwenda kwa mtu mmoja, na hata kubuild mashambulizi anaanza yeye.

Ndio maana tuna hofu na umri wa madaraka ya Rais yeye ameshakataa, lakini hajajua hofu waliyonayo kina Nkamia na wenzake. Wanaona hakuna mtu anayeweza kuziba nafasi.

Mfumo wa uchezaji umeaamua hivyo tutafanyaje? Labda tubadili mfumo pale mbele tuweke hapo watu wanne wanaoweza kufunga wote.

Juma Nkamia

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.