Punguza hasara, wekeza

Rai - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

KASI ya umaarufu wa uwekezaji wa pamoja duniani inaendelea kukua kila siku na kushamiri kama nguzo ya mafanikio.

Kanuni ya uwekezaji huu ambao kwa hapa nchini unasimamiwa na kampuni ya UTT AMIS, ni makubaliano ya pamoja ambayo mara nyingi huwa katika thamani ya mwanzo ya kipande, sehemu za kuwekeza, kanuni za thamani ya mali iliyowekezwa, mwangalizi wa mali au fedha

KASI ya umaarufu wa uwekezaji wa pamoja duniani inaendelea kukua kila siku na kushamiri kama nguzo ya mafanikio.

Kanuni ya uwekezaji huu ambao kwa hapa nchini unasimamiwa na kampuni

ya UTT AMIS, ni makubaliano ya pamoja ambayo mara nyingi huwa katika

thamani ya mwanzo ya kipande, sehemu za kuwekeza, kanuni za thamani ya mali iliyowekezwa, mwangalizi wa mali au fedha, wasimamizi na mambo mengine mengi yanayourasimisha uwekezaji huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba mwaka jana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa UTT AMIS, suala la msingi katika

uwekezaji huu ni kuangalia namna ya kukabiliana na hali hatarishi kwenye uwekezaji huku lengo kuu ikiwa ni kupata faida wakati ikieleweka kwamba kipande au thamani ya fedha iliyowekezwa inaweza kupanda au kushuka.

“Uwezekano wa kupata hasara hupunguzwa kwa kutawanya sehemu za kuwekeza. Mfano kwenye hisa na kwenye masoko ya fedha. Sehemu hizi

mbili peke yake ni dunia pana sana ya uwekezaji.

“Hasara pia inapunguzwa na ukweli kwamba meneja wa fedha zilizo kwenye

Uwekezaji wa Pamoja (ambaye ni UTT AMIS) ni lazima awe mtaalamu

aliyebobea, leo hii Watanzania wengi bado wanajiuliza kipande ni nini?

Hisa ni nini? Akaunti ya muda maalumu ni nini na hata hati fungani ni nini?

“Maswali haya na mengine mengi na jinsi ya kushiriki katika uwekezaji

huu ambao misingi yake ni faida huku athari za Uwekezaji zikiwa zimezingatiwa na kusimamiwa, yanajibiwa na wataalamu kama madalali wa soko la hisa, vitengo vya uwekezeji katika mabenki na kampuni yetu ya UTT AMIS,” anasema Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Daud Mbaga.

Anasema faida kubwa nyingine ni kuwa uwekezaji huu haujali kipato,

kwamba mwenye kipato kikubwa na mwenye kipato cha chini wote hupata

faida sawa kwa kipande, ila mwenye vipande vingi huvuna zaidi.

“Cha msingi hapa ni kwamba mwenye hata Sh. 10,000 anaweza kuwa mwekezaji na anaweza kuwekeza mara nyingi anavyoweza bila kujali muda.

Hivyo basi kwa wewe mwenye biashara na unapata faida kila siku unaweza kukusanya faida na kuiwekeza kila siku au ukakusanya na ukaweka japo

mkupuo mmoja kila wiki na hivyo ukaipa faida yako uwezo wa kuzaa faida nyingi zaidi,” anasema. Mbaga anasisitiza kuwa muda ndio muhimu zaidi, akisema Uwekezaji ni

jambo linalohitaji muda ili kukabiliana na mawimbi ya kupanda na kushuka kwa thamani. Ni kama mti ukipanda mbegu inaanza mizizi inaenda chini, halafu mmea unaota baadae mti wenye matawi, maua na hatimae matunda.

Kuhusu gharama za Uwekezaji, Mkurugenzi huyo anasema hupunguwa sana kwa watu kuwekeza pamoja.

“Sote tunajua kuwa huwa tunalipa nauli kubwa sana kama tukisafiri peke

yetu kwa teksi kuliko tukisafiri pamoja kwa daladala, pia tunapata punguzo dogo sana tukijadili bei kwa bidhaa chache kuliko tunapojadili manunuzi ya bidhaa nyingi.

“Kilo moja hupunguzwa kwa asilimia mbili lakini kuanzia kilo 10 hupunguzwa kwa hadi asilimia nne! Hivyo pesa zikiwa nyingi zinaongeza

nguvu ya majadiliano. Pia pesa zikiwa nyingi zinakupa nafasi ya kufanya Uwekezaji ambao peke yako usingeweza kwa pesa chache kuwekeza katika hati fungani, hisa na akaunti za muda maalumu kwani huko huhutajika kuanzia kiasi fulani cha fedha,” anasema mtaalamu huyo.

Faida nyingine ni unafuu katika kodi kwani serikali kote duniani waliamua kwa makusudi kuweka kiasi kidogo cha kodi katika mfumo huu wa Uwekezaji ili kumpa unafuu mwekezaji.

Taarifa inaendelea kusema kuwa zaidi ya hapo, mwekezaji anapewa fursa

ya kuchagua mfuko kutokana na malengo yake. Mfano Mfuko wa Umoja lengo lake ni kukuza mtaji; Mfuko wa Jikimu huwa na gawio mara nne kwa

mwaka; Mfuko wa Watoto ni kwa ajili ya elimu na maisha baada ya kufuzu

wakayi Mfuko wa Ukwasi humpa mwekezaji kipato cha muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.

Pamoja na faida za Uwekezaji wa pamoja changamoto pia zipo, kwani

wawekezaji humpa fedha meneja, meneja anaziwekeza kwa niaba yao.

Meneja anatakiwa awe amebobea, awe na ufanisi wa hali ya juu, awe

mkweli na mwenye kufuata masharti ya Uwekezaji. Kampuni ya UTT AMIS inayomilikiwa na serikali, ipo tangu mwaka 2003 na ilianzisha Uwekezaji wa Pamoja mwaka 2005. Katika kipindi chote hicho imekuwa ikifanya vizuri sana.

“Kumbuka kuwa mojawapo ya sehemu fedha zinakowekezwa ni kwenye hisa, hisa hupanda na kushuka na hisa ni kioo cha vipande kwa mifuko yenye asilimia fulani ya hisa katika Uwekezaji wake, hisa zikishuka, thamani ya mfuko inashuka! Hii kwa kiasi fulani ni changamoto kwenye uwekezaji.

“Pia thamani ikishuka mwekezaji na hata meneja wanapata kidogo. Hivyo

meneja ni lazima awe makini kwenye kuchagua ni hisa zipi anunue.

“Kwa kawaida serikali au mtu binafsi ndiye mwanzilishi, halafu fedha

zitakazowekezwa zitatoka kutoka kwa wawekezaji, mwanzilishi atapata faida na mara nyingi haizidi asilimia mbili ya thamani ya kiasi kilichowekezwa.

“Jitihada na juhudi za kuwashawishi wawekezaji kuwa kila jambo litakuwa sawa zinahusika pale mwanzoni na kadri Uwekezaji unavyosogea mbele ni lazima kutoa taarifa sahihi za ukuaji wa Uwekezaji ili kuvutia wawekezaji,” anasema Mbaga.

Wawekezaji wakiwa wengi, anasema, fedha huwa nyingi na kuweza kufidia gharama za lazima na gharama nyingine za uendeshaji. Kama kuna madeni ni lazima uwiano kati ya mtaji na madeni uwe mzuri.

Changamoto nyingine ni kama kuna kufilisika, hii inaweza kusababisha kutoa mali zote zilizowekezwa na inawezekana kukawa bado kuna Uwekezaji ambao ulikuwa bado haujaiva. UTT AMIS inasimamia takribani

Sh. bilioni 280 na kila siku inazidi kupanuka. Pia muda wa kwanza wa kuwekeza ukiisha inabidi Uwekezaji uendeleee na pengene riba kwa wakati huo zinakuwa zimeshuka aidha kwa soko la awali au soko la pili. Changamoto nyingine ni kupungua kwa thamani ya fedha, mfumko wa bei na vitu kama bivyo.

Changamoto nyingi zikiwemo mabadiliko katika sera za uwekezaji, hali ya uchumi wa nchi husika na mabadiliko, mfano wa kutoa fedha katika Uwekezaji wa muda mrefu na kwa ajili ya kuwekeza katika muda mfupi, au muda mfupi kwenda muda mrefu.

Ili kukabiliana na changamoto, mwekezaji wa UTT AMIS lazima ajue kuwe kampuni hii ni ya serekali na imeanzishwa kufuata taratibu za kisheria, iko chini ya Wizara ya Fedha; sheria imezingatiwa ili kumlinda mwekezaji.

Mfano lazima kuwe na mwangalizi wa fedha/mali ambapo kwa UTT ni Benki ya CRDB, lazima kuwe na wakaguzi wa hesabu wa ndani na nje ambapo

kwetu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serekali (CAG) na KPMG hufanya kazi hiyo.

Kuna waraka wa makubaliano unaoainisha taratibu mbalimbali za lazima, na kila mfuko una kitabu chake chenye kuonyesha tabia za mfuko na kanuni mbalimbali, licha ya hivyo wawekezaji wana nafasi ya kuchangia mabadiliko kwenye mkutano mkuu wa mwaka na wanaweza kumkataa meneja kama wanaona hafai. Hakuna ukomo wa kununua vipande na kwa kutumia simu unaweza kununua kila siku na hata saa ambazo si za kazi, Watanzania wengi wana dhana kuwa unawekeza mara moja tu basi halafu unasubiri. Dhana hii si sahihi, wekeza mara nyingi unavyoweza, na jaribu kuwa na subra ili kuupa Uwekezaji wako muda wa kukua. Kumbuka kiasi cha chini ni takribani shilingi 10,000 kwa kila mfuko isipokuwa mfuko wa ukwasi ambao utaanza na shilingi milioni 5.

Kumbuka tofauti na hisa, kipande unauza na kunua wakati wowote, hivyo huhitaji kusubiri kupata pesa zako, ndani ya siku kumi utakuwa umepata pesa zako katika akaunti yako uliyoainisha, na kama binadamu mauti ya kakukumba mrithi uliye mwandika katika fomu za kujiunga ndiye atakayesimamia Uwekezaji wako.

Pesa zinapatika kutoka katika Uwekezaji zinagawiwa kwa kila mwekezaji kwa asilimia sawa kutokana na idadi ya vipande vyake. Baadhi ya mifuko mwekezaji atapata gawio katika kila kipindi cha muda fulani, mwekezaji

anaweza kuacha gawio hilo katika Uwekezaji, baadhi ya mifuko mwekezaji atachukuwa faida yake pale anapohitaji na pia mwekezaji anaweza kutoka katika Uwekezaji wakati wowote. Uwekezaji wa pamoja ni Uwekezaji ambao unaweza kuwa anuwai, yaani

mseto kwenye hisa na kwenye masoko ya fedha (kukopesha), lakini pia mfuko unaweza ukawa unawekeza kwenye hisa tu, yaani kwenye kampuni zilizoorodhoshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Kwa Tanzania hatuna mfuko unaowekeza kwenye soko la hisa peke yake. Na kuna mifuko unawekeza kwenye soko la fedha tu yaani katika benki na hati fungani mfano wa mfuko huu ni Mfuko wa Ukwasi, hii ina maana kuwa mfuko huu hauna tabia ya kipande kupanda na kushuka kwa mawimbi makubwa kwani riba za hati fungani na za benki huwa na mawimbi ya wastani ukilinganisha na mwenendo wa faida kwenye hisa.

Sasa ni wakati muafaka kwa Watanzania kuchukua hatua na kuanza

Uwekezaji huu kwani ni mbadala mzuri sana wa vibubu, au kuweka fedha sehemu ambazo si rasmi, pia unafaida ukilinganisha na akaunti za kawaida za akiba, na changamoto zilizopo kwa vikoba. Kumbuka haba na haba hujaza kibaba.

Daud Mbaga

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.